Kitoabu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 11,084
- 12,326
Tunataka tuing'oe ccm kwanza wakajifunze adabu
Huwezi kuing'oa CCM kupitia kwa mafisadi.
Tunataka tuing'oe ccm kwanza wakajifunze adabu
Huwezi kuing'oa CCM kupitia kwa mafisadi.
Huwezi kuing'oa CCM kupitia kwa mafisadi.
Umesema uharo ndio umenitonesha kidonda kabisa
Yaaan uharo wa yule mgombea mliotuletea alivyokitia aibu chama chetu cha demokrasia na maendeleo huko stand ya chato?
Yaaa 4u mnaniuzi sana nyie
Wanafik wakubwa nyie
Kaka imeniuma sana
Nmeamua kuandika haya ya moyon
Chadema iliyogharimu maisha na damu zetu leo inatusaliti
Kwakweli ninampa magufuli kura yangu
Fuatilia historia ya siasa za kenye utapata majibu ya maswali yako.... kenya kwa sasa ndo nchi yenye katiba bora zaidi Africa..... jitambue...
Fuatilia historia ya siasa za Kenya utapata majibu ya maswali yako.... Kenya kwa sasa ndo nchi yenye katiba bora zaidi Africa..... jitambue...
Chadema maslahi mnajishusha sana, yaani mtu yeyote akiandika points za msingi ni wa lumumba, kwamba chadema hamna wa kuandika point?
Mnazidi kujivua nguo!
Ulikuwa CDM, baada ya kuchukua chako mapema unatuletea huu upuuzi! Hauko peke yako mpo wengi wa hivi!! Ila hatudanganyiki!!! People's power!!!!!
Mimi ni mwanachama wa Chadema lakini kura yangu sitaipeleka Ukawa
1. Tumeshindwa kuamini katika mabadiliko. Kwa miaka 20 tumejenga upinzani Tanzania leo hii imekuwaje tumekabidhi chama kwa watu ambao miaka yote tulitaka waondoke?
2. Ukawa ni nini hasa? Umoja wa Katiba ya Wananchi. Je tulikuwa na lengo na mipango ya kuweza kuongoza nchi? Je kama leo hii viti vya udiwani na Ubunge tu tumeshindwa kugawana sawa sawa nchi hii tutaweza kuiongoza au tunaiweka amani ya nchi rehani?
3. Lowassa ni nani? Hivi yeye kusema sasa ni zamu ya Walutheri kutoa Rais hakuwaona Waislamu, Wakatoliki, Wapagani na watu wa dini nyingine ndani ya Ukawa? Hivi kwake yeye Ulutheri ni muhimu kuliko Utanzania?
4. Leo zimebaki siku 17 kupiga kura. Hivi sera yetu Ukawa ni ipi? Mabadiliko. Lakini mabadiliko maana yake nini? Elimu bure? Sawa, tueleze kivipi? Elimu bure, afya bure, kuondoa kodi ya mfanyakazi, kupunguza ushuru kwa wawekezaji na wafanyabiashara wadogo wadogo, kutotegemea misaada? Hivi kweli?
Fedha ya kutoa vitu bure itatoka wapi bila kodi? Kwenye gesi? Lakini hadi leo gesi hata haijaanza kutoa hiyo faida. Tunaambiwa faida ni ndani ya miaka 6 ijayo angalao, je mpaka miaka 6 inaisha hivyo vitu bure vitakuwa vinatolewaje? Kwa mkopo? Toka kwa nani? Tutalipaje huo mkopo?
SERA ZETU NI ZIPI? MBONA HAZIELEWEKI? MBONA ZIMEKAA KIJANJA JANJA NA HAZIWEZEKANI?
5. Hivi Gwajima huyu ni nani kwetu? Huyu si ndiye Yule alisema ana ndoto kwamba siku moja Misikiti yote Tanzania itageuka kuwa Makanisa na Madrasa kuwa Sunday School? Hivi lini ndoto yake itatimia? Hivi ina mahusiano yoyote na Lowassa kusema sasa ni zamu ya Ulutheri?
6. Hivi Chadema tumekosa wapanga mikakati ya kampeni? Iweje leo hii 4u Movement ambayo ni vijana wa UVCCM waje Chadema na wameiweka BAVICHA yetu pembeni? Hivi ni mabadiliko gani haya tunawaza? Tunafikiri sawa sawa kweli?
Asilimia 70% ya wajumbe wa mkutano mkuu CHADEMA wote wanatoka eneo moja la nchi. Hivi sisi tuna akili sawa sawa kweli? Nchi sio jimbo wala kata.
MIMI NI MWANACHAMA WA CHADEMA LAKINI KURA YANGU MWAKA HUU SIIPIGII CHADEMA ILI KUINUSURU NCHI NA MATATIZO. TANZANIA KWANZA, BIASHARA ZA KUJENGA NA KUUZA VYAMA BAADAYE.