Mambo sita yanayotushangaza WanaChadema wazalendo

Mambo sita yanayotushangaza WanaChadema wazalendo

navy boi

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2014
Posts
1,520
Reaction score
483
Mimi ni mwanachama wa Chadema lakini kura yangu sitaipeleka Ukawa

1. Tumeshindwa kuamini katika mabadiliko. Kwa miaka 20 tumejenga upinzani Tanzania leo hii imekuwaje tumekabidhi chama kwa watu ambao miaka yote tulitaka waondoke?

2. Ukawa ni nini hasa? Umoja wa Katiba ya Wananchi. Je tulikuwa na lengo na mipango ya kuweza kuongoza nchi? Je kama leo hii viti vya udiwani na Ubunge tu tumeshindwa kugawana sawa sawa nchi hii tutaweza kuiongoza au tunaiweka amani ya nchi rehani?

3. Lowassa ni nani? Hivi yeye kusema sasa ni zamu ya Walutheri kutoa Rais hakuwaona Waislamu, Wakatoliki, Wapagani na watu wa dini nyingine ndani ya Ukawa? Hivi kwake yeye Ulutheri ni muhimu kuliko Utanzania?

4. Leo zimebaki siku 17 kupiga kura. Hivi sera yetu Ukawa ni ipi? Mabadiliko. Lakini mabadiliko maana yake nini? Elimu bure? Sawa, tueleze kivipi? Elimu bure, afya bure, kuondoa kodi ya mfanyakazi, kupunguza ushuru kwa wawekezaji na wafanyabiashara wadogo wadogo, kutotegemea misaada? Hivi kweli?

Fedha ya kutoa vitu bure itatoka wapi bila kodi? Kwenye gesi? Lakini hadi leo gesi hata haijaanza kutoa hiyo faida. Tunaambiwa faida ni ndani ya miaka 6 ijayo angalao, je mpaka miaka 6 inaisha hivyo vitu bure vitakuwa vinatolewaje? Kwa mkopo? Toka kwa nani? Tutalipaje huo mkopo?

SERA ZETU NI ZIPI? MBONA HAZIELEWEKI? MBONA ZIMEKAA KIJANJA JANJA NA HAZIWEZEKANI?

5. Hivi Gwajima huyu ni nani kwetu? Huyu si ndiye Yule alisema ana ndoto kwamba siku moja Misikiti yote Tanzania itageuka kuwa Makanisa na Madrasa kuwa Sunday School? Hivi lini ndoto yake itatimia? Hivi ina mahusiano yoyote na Lowassa kusema sasa ni zamu ya Ulutheri?

6. Hivi Chadema tumekosa wapanga mikakati ya kampeni? Iweje leo hii 4u Movement ambayo ni vijana wa UVCCM waje Chadema na wameiweka BAVICHA yetu pembeni? Hivi ni mabadiliko gani haya tunawaza? Tunafikiri sawa sawa kweli?

Asilimia 70% ya wajumbe wa mkutano mkuu CHADEMA wote wanatoka eneo moja la nchi. Hivi sisi tuna akili sawa sawa kweli? Nchi sio jimbo wala kata.

MIMI NI MWANACHAMA WA CHADEMA LAKINI KURA YANGU MWAKA HUU SIIPIGII CHADEMA ILI KUINUSURU NCHI NA MATATIZO. TANZANIA KWANZA, BIASHARA ZA KUJENGA NA KUUZA VYAMA BAADAYE.
 
Inapendeza kuona watu wanajitambua na hawataki kuiweka nchi rehani.
Hauko peke yako kamanda wa asili.
 
Propaganda zenu hatuzihitaji huku UKAWA.

Sisi tumeamua mwaka huu ni mabadiliko. Hagta mseme vipi. Jinsi ulivyoandika wewe dhahiri ni LUMUMBA type. Tuachieni UKAWA yetu izidi kunawiri kwani wenye akili trimamu ndio hawa wanaorudisha kadi za CCM.

Mtanzania jitambue acha kukumbatia mapanya.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!
 
CHADEMA haiwezi kuwa na watu wapuuzi hivi........watu kama wewe wanapatikana CCM tu !
 
Naona mmekariri huu msemo. Jipangeni sana, watanzania wengi sio wajinga!

Achaneni na ukawa!
Ukawa habar ya moto kwenu lumumba!
Mnahaha na hilo mnalijua!

Hamuamin kama ndo mnakabidhi nchi hivo!
***** lazima akili ziwakae sawa kuku wa maziwa nyie!
 
Nami nashanga chadema wazalendo ni nini?kwanini waje wakati huu?uongozi wao ni upi?kura yako inaumuhimu gani?nikwanini ususe wengine wakila unahoji kwanini wanakula?kwakuwa Kushanga mwisho tar 25 tuedelee kushangaa,
 
Achaneni na ukawa!
Ukawa habar ya moto kwenu lumumba!
Mnahaha na hilo mnalijua!

Hamuamin kama ndo mnakabidhi nchi hivo!
***** lazima akili ziwakae sawa kuku wa maziwa nyie!

Hamtokabidhiwa hii nchi kawme sababu hamna hoja zaidi ya matusi. Chadema asili hatumpigii kura lowassa.
 
Kwakwel bora ccm sikuwai kufikilia haya mambo

Kaka imeniuma sana
Nmeamua kuandika haya ya moyon

Chadema iliyogharimu maisha na damu zetu leo inatusaliti
Kwakweli ninampa magufuli kura yangu
 
Nami nashanga chadema wazalendo ni nini?kwanini waje wakati huu?uongozi wao ni upi?kura yako inaumuhimu gani?nikwanini ususe wengine wakila unahoji kwanini wanakula?kwakuwa Kushanga mwisho tar 25 tuedelee kushangaa,

Ni mkwel mkuu!
Wanakera sana hawa kuku
 
Nami nashanga chadema wazalendo ni nini?kwanini waje wakati huu?uongozi wao ni upi?kura yako inaumuhimu gani?nikwanini ususe wengine wakila unahoji kwanini wanakula?kwakuwa Kushanga mwisho tar 25 tuedelee kushangaa,

Chadema wazalendo ni wale waliokataa kurubuniwa na kudanganywa na dhana ya mabadiliko ambayo ni feki, ni wale ambao bado wana misimamo yao ambayo ilijenga ktk msingi wa kupinga ufisadi, ni wale ambao sio vigeu geu!
Pia baadhi yao ni wale ambao wamevuja damu na jasho mpaka kuifikisha chadema mpaka muda ule ambao lowassa alikuwa hajaingia chadema.
Umuhimu wa kura yao mtaupata baada ya uchaguzi, tarehe 28 ya mwezi huu. Suala la ofisi, ilikuwa ni kinondoni mtaa wa ufipa.
 
Propaganda zenu hatuzihitaji huku UKAWA.

Sisi tumeamua mwaka huu ni mabadiliko. Hagta mseme vipi. Jinsi ulivyoandika wewe dhahiri ni LUMUMBA type.

Tuachieni UKAWA yenu izidi kunawiri kwani wenye akili trimamu ndio hawa wanaorudisha kadi za CCM.

Mtanzania jitambue acha kukumbatia mapanya.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Sijui kwann makamanda tumelogwa namna hii
Mungu atuvushe salaama

Siamn kama ndio chadema hii ya leo iliyosababisha nikalala segerea
 
Achaneni na ukawa!
Ukawa habar ya moto kwenu lumumba!
Mnahaha na hilo mnalijua!

Hamuamin kama ndo mnakabidhi nchi hivo!
***** lazima akili ziwakae sawa kuku wa maziwa nyie!

Tuachr porojo makamanda wenzangu
Ebu tuzichanganue na kuziji hoja zangu
ili tujisahihishe na tusonge mbele
lakin nahis tumerogwa vile
sio akili zetu makamanda hizi
 
Back
Top Bottom