ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Mambo poa...
Hivyo ndivyo wanavyoonekana kusema vijana machachari katika siasa.
Vijana hawa walikuwa Mbulu katika harakati za kujenga nchi.
Tanzania ina kila sababu ya kujivunia vijana wazalendo na jasiri kama hawa.
Mambo poa, na wataendelea kufanya bidii yawe poa zaidi.
Kama ilivyo kwingine duniani, taifa letu pia lina changamoto ya uwepo wa vijana wachache waoga, wasiojiamini. Vijana wa namna hiyo mara nyingi huwa wamejikunyata tu wakingoja kupewa maelekezo ya nini cha kufanya. Hawana ubunifu na ni dhaifa wa fikra.
Vijana wa namna hiyo ni WASALITI wa nafsi zao. Wanatamani wawe na sababu ya kusema mambo poa, lakini hawapati sababu hiyo. Wameshikiwa akili na watu wengine kwa kulaghaiwa kuwa wao ni informers au spies. Kumbe hakuna chochote zaidi ya kushikiwa akili.
Wanapoona wenzao wako mambo poa, wao roho zinawauma. Wanatamani kuwa mambo poa, lakini wamefungwa minyororo kifikra. Hawana fikra huru!
Jifungue kwenye minyororo,kijana jiunge na mambo poa...