Mambo nitakayopendekeza katika tume ya katiba mpya

kingfish

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
571
159
Nitapendekeza kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na maafisa tarafa.vyeo hivi ni mzigo kwa serikali na vinaleta mgongano kiutendaji na ngazi nyingine,kwa mfano kuna mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya,mkurugenzi ndiye msimamizi wa shughuli zote za maendeleo katika wilaya akisaidiwa na baraza la madiwani.sielewi mkuu wa wilaya anafanya nini zaidi ya kuambiwa na kuaminishwa kuwa yeye ni msimamizi wa usalama katika wilaya.pia napendekeza kuwa kuwe na "limit" ya idadi ya wizara,rais asiwe na mamlaka ya kuongeza wizara.
 
Rais apunguziwe mamlaka ya uteuzi wa nafasi mbalimbali kama bodi
 
Na mawaziri wawe si wabunge. Wabunge wabaki wasiasa tu si kuongoza wizara asiona taaluma kisa anatoka chama tawala. Rais apewe uwezo wa kuchagua mawaziri nje ya wabunge wenye taaluma husika ila hao wabunge waisimamie sirikali. Sio wewe mbunge hapohapo unaiongoza sirikali. Je utaihoji serikali muda gani kwa w'nch wako waliokutuma wakt wewe ni waziri?
 
Nchi nyingi duniani hasa zilizoendelea, mayor wa Halmashauri na MKURUGENZI WAKE WANATOSHA KUFAYA COVERAGE YA SEKTA ZOTE ZA KIUCHUMI NA KIJAMII NA MAENDELEO YANAONEKANA. SISI HAPA DUPLICATION/OVERLAPPING OF DUTIES KIBAO. kUONGEZA TUU GHARAMA ZA KUIENDESHA SERIKALI.
 
Mimi nitapendekeza yafuatayo.
1.Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi apatikane kwa kuomba kazi na awe anafanyiwa Interview na wataalamu maalumu wakishirikiana na Wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kila chama kinatakiwa kiwe na muwakilishi mmoja.

2. Rais wa nchi asiwe na mamlaka yeyote kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa wa uchaguzi ili kupunguza undue influence.
3. Pia rais aondolewe kinga dhidi ya makosa anayofanya pindi akiwa madarakani.

Haya ndiyo maoni yangu siku nikifuatwa n ile tume.
 
Nitapendekeza kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na maafisa tarafa.vyeo hivi ni mzigo kwa serikali na vinaleta mgongano kiutendaji na ngazi nyingine,kwa mfano kuna mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya,mkurugenzi ndiye msimamizi wa shughuli zote za maendeleo katika wilaya akisaidiwa na baraza la madiwani.sielewi mkuu wa wilaya anafanya nini zaidi ya kuambiwa na kuaminishwa kuwa yeye ni msimamizi wa usalama katika wilaya.pia napendekeza kuwa kuwe na "limit" ya idadi ya wizara,rais asiwe na mamlaka ya kuongeza wizara.

Hizi message ni vema zifike kwenye tume and its better pia hiyo tume iwe na website ambayo watu wanaweza kupost mapendekezo yao!
 
Kampuni zote za ukaguzi na ushauri hapa Tanzania zisiruhusiwe kutumia "Global names" watumie majina yaliyosajiliwa hapa nchini kama Mushi & Company, Tibazigwa & Associates etc. India wanatumia mtindo huu hivyo kuondoa ushindani usio sawa unaoletwa na "brand names" wakati watenda kazi ni wale wale waliofundishwa na Musarira, Kilagane na wengineo
 
Mimi nitapendekeza yafuatayo.
1.Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi apatikane kwa kuomba kazi na awe anafanyiwa Interview na wataalamu maalumu wakishirikiana na Wawakilishi wa vyama vyote vya siasa kila chama kinatakiwa kiwe na muwakilishi mmoja.

2. Rais wa nchi asiwe na mamlaka yeyote kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa wa uchaguzi ili kupunguza undue influence.
3. Pia rais aondolewe kinga dhidi ya makosa anayofanya pindi akiwa madarakani.

Haya ndiyo maoni yangu siku nikifuatwa n ile tume.

Mawazo mazuri, lakini kaa ukijua tume haitakufuata. Itabidi uifuate.
 
Nitapendekeza kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na maafisa tarafa.vyeo hivi ni mzigo kwa serikali na vinaleta mgongano kiutendaji na ngazi nyingine,kwa mfano kuna mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya,mkurugenzi ndiye msimamizi wa shughuli zote za maendeleo katika wilaya akisaidiwa na baraza la madiwani.sielewi mkuu wa wilaya anafanya nini zaidi ya kuambiwa na kuaminishwa kuwa yeye ni msimamizi wa usalama katika wilaya.pia napendekeza kuwa kuwe na "limit" ya idadi ya wizara,rais asiwe na mamlaka ya kuongeza wizara.

  • Majaji, dpp, CAG, mKuu wa TAKUKURU na Mwanasheria mkuu wa serikali wasiwe wateule wa Rais
  • Mahakama na ofisi ya mkaguzi mkuu wa serikali zijitegemee kwa fedha na wapate fedha kwa % inayokusanywa na TRA
  • Kuwepo na mgombea binafsi
  • Yainishwe madaraka ya waziri mkuu
  • Kuwepo na mfumo wa serikali za Majimbo
 
Back
Top Bottom