Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,360
Ule msemo wa Mwaka mpya na mambo umekuwa kivitendo zaidi kwangu kwa huu mwaka, Namshukuru mwenyezi mungu kwa kubariki juhudi zangu na sasa nimefanikiwa kununua kagari kangu(Carina Ti) nikiwa nina miaka 24 na sina budi kumshukuru Mungu, Nina takribani miezi mitatu tangu ninunue gari langu na haya ndio mambo niliyoyashuhudia na kuyaexperience.
1. Hadhi yangu(status) Imepanda - Simanishi kusema nlikuwa nadharaulika pindi sina gari, Hapana ila nachomaanisha ni kwamba status yangu imeongezeka, Majina kama Brother, Uncle n.k nshayazoea maana haipiti siku bila kuitwa hayo majina.
2. Gharama za matumizi zimepanda - Gharama zangu za matumizi zimepanda maana Gari linahitaji mafuta na ya elfu 5 kwa siku (mizunguko michache na mji ni mdogo), Gari inahitaji service kwenye gereji na hayo ni matumizi mapya kwangu, Gari nailipia laki moja kila mwezi ili ioshwe kila siku mwezi mzima n.k
3. Usafir wa usiku sio wa mawazo tena - Sina tabia za kutoka toka nje usiku ila ikija kutokea mfano nimeenda kwenye sherehe zile za kutoka usiku wa manane sitakuwa na hofu juu ya upatikanaji wa usafiri au gharama za juu za usafiri, Nina usafiri wangu.
4. mwili umekosa mazoezi - zamani kutembea, kukimbilia dala dala, na kugombaniana siti yalikuwa mazoezi tosha, ila kwa sasa k\sitembei umbali mrefu wala kukimbia ili kuwahi sehem nayotaka kufiaka, however naconsider kuanza kwenda gym
5. Marafiki na maadui wameongezeka - Kwa sasa nimeongeza marafiki wanomiliki magari maana tunakutana sehemu nyingi hivyo tunazoeana. Pia ukiangalia kwenye huu uzi kuna watu wanaoponda sana tu aidha kwa chuki, kufata mkumbo au kutojua magari vizuri..Hawaelewi kwamba mafuta ya 5000 per day kwa gari nyingi zenye 1800cc ama kushuka chini ndo yanafaa na hayaishi yote kama upo mkoani na hauna misele mingi..