Mambo Muhimu kuelekea msimu wa kilimo

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
1. Maandalizi ya pembejeo, hapa inajumuisha vitu Kama mbegu,mbolea na madawa ya wadudu. Ilikufanya kilimo kiwe chenye tija maandalizi ya pembejeo lazima yafanyike kabla ya Jambo lolote.

2. Maandalizi ya shamba. Moja ya Mambo ambayo mkulima unatakiwa kuwa makini Ni kuhakikisha shamba limeandaliwa mapema na kwa umakini hi hupelekea kuongeza kwa mavuno. Na katika zoezi la uandaji was shamba lazima ukumbuke kutengeneza njia (mifereji) kwaajili ya kuruhusu maji yawe na njia maalumu.

3. Uchaguzi sahihi wa zao husika kwenye shamba unalotaka kulima . Sio Kila zao linakubali kwenye Kila aina ya udongo hivyo unashauliwa kuchagua mapema Ni aina gani ya udongo na zao gani utakalo panda.

4. Pia ni mhimu kujua ni aina gani ya zao lililolimwa msimu uliopita. Hii itakusaidia kuweza kujua zaidi a Ina gani ya zao litafanya vizuri zaidi, mfano shamba lililopandwa zao jamii ya mikunde litafanya vizuri zaidi likipandwa mahindi.

5. Jambo la mwisho nikuzingatia mda sahihi wa kupanda zao husika. Panda mazao yako kwa wakati sahihi ili kuzuia wadudu waharibifu na magonjwa ambayo maranyingi husababishwa na kutopanda kwa wakati sahihi.
 
Back
Top Bottom