Mambo Mawili Hatari Zaidi kwa CCM

G.T.L

JF-Expert Member
Jul 15, 2012
773
1,247
Katika kipindi hiki cha tuhuma za wabunge kuhusishwa na kashfa ya rushwa,hususani wabunge wa CCM(kwa wingi wanaosadikiwa),Endapo wakithibitika kupokea rushwa.Ni Ukweli usiopingika kwamba.....
*
1.Wakifukuzwa uanachama wa CCM ambapo ni dhahiri watapoteza sifa za kuendelea kua wabunge,CCM itakua matatani kupoteza majimbo ambayo uchaguzi utafanyika.
*
2.Wasipowafukuza ni ukweli usiopingika kwamba CCM itazidi kupoteza zaidi imani kwa wananchi ambapo 2015 itakua njia laini zaidi kwa upinzani kuchukua majimbo mengi zaidi.

Hii haitaji ata ushabiki wa kisiasa ni kutumia common sense kusoma nyakati.
 
Kwa mtazamo wangu, hawa jamaa lazima watafuata hilo angalizo lako la pili. Maana walishapoteza imani kwa wananchi siku nyingi sana.
 
Hili ni tatizo la miaka mingi sana, kwahiyo uamuzi juu yake hautakuwa wa kukurupuka. Binafsi nadhani mwisho wa siku tutarudishwa kule kule kwenye siasa: Uwezekano wa Rais kuvunja bunge zima au bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali huku kila upande ukimtishia mwenzake. Sio chadema wala CCM ambao wapo tayari kurudi majimboni sasahivi, hivyo itapatikana suluhu nyingine nje ya kufukuza wabunge.
 
huu ni mwiba kwa ccm kwani wakifukuzwa hawa wataeleza chama kilivyohonga na kutoa rushwa kwa wapiga kura chini ya maelekezo toka ccm makao makuu data zipo hata kikwete hawezi kufanya lolote.
la pili lowas,chenge hakuna aliyewagusa mkiwagusa hawa mnawasha moto kwa akina sita na wenzake kazi mayo poleni sana na tunaishukuru chadema kwa hili
 
hiyo ni sawa na msemo wa kimakonde Ukichuka Nchale, Ukichimama Nchale, Ukikimbia Nchale sasa sijui wataamua lipi.
 
Katika kipindi hiki cha tuhuma za wabunge kuhusishwa na kashfa ya rushwa,hususani wabunge wa CCM(kwa wingi wanaosadikiwa),Endapo wakithibitika kupokea rushwa.Ni Ukweli usiopingika kwamba.....
*
1.Wakifukuzwa uanachama wa CCM ambapo ni dhahiri watapoteza sifa za kuendelea kua wabunge,CCM itakua matatani kupoteza majimbo ambayo uchaguzi utafanyika.
*
2.Wasipowafukuza ni ukweli usiopingika kwamba CCM itazidi kupoteza zaidi imani kwa wananchi ambapo 2015 itakua njia laini zaidi kwa upinzani kuchukua majimbo mengi zaidi.

Hii haitaji ata ushabiki wa kisiasa ni kutumia common sense kusoma nyakati.

Una maoni mazuri sana na ya kweli, lakini sio kwa tanzania, hapa watu hawatazami sera, wanatazama ushabiki tu! Hasa wale wazee wetu wa vijijini na CCM
 
CCM hawatawafukuza mtu hata mmoja!! Watawekeza katika usahaulifu wetu!!.
Silly people!!
Watakachofanya CCM ni kuleta jambo jipya litakaloelekeza focus ya Bunge na wananchi huko na kama kawaida tutasahau. Au watatumia wafanyabiashara wa Neno la Mungu (wa makanisani na misikitini) kugeuza hoja ya rushwa kuwa malumbano ya kidini na Watanzania wataunga msafara huo.
 
Kwa mtazamo wangu, hawa jamaa lazima watafuata hilo angalizo lako la pili. Maana walishapoteza imani kwa wananchi siku nyingi sana.
una maana Mh. Ole Sendeka afukuzwe??
....mbunge aliyetumia muda mwingi kupinga ufisadi lakini akajikuta 'amewekwa kati' kwa mda mfupi sana

Hii imekaa vizuri. Nape anasubiri CDM waanze. Nadhani anaombea mungu CDM wasichukue maamuzi yeyote ili na yeye akae kimya maana atasema nini kwa Ole?
 
Back
Top Bottom