Jielewe
Member
- Jan 10, 2017
- 39
- 62
Pamoja na kejeli nyingi kwa wafanyakazi/waajiriwa wanaotegemea, bado uwezekano wa mfanyakazi kujikwamua kiuchumi upo akizingatia mambo kadhaa. Kubwa ni nidhamu. Unapokuwa na nidhamu ya mshahara, unaongeza uwezekano wa kuwa na usalama wa kifedha.
Swali linaweza kuwa, ‘Kinachomfanya mfanyakazi akose nidhamu ya fedha ni nini?’ ‘Inakuwaje mchuuzi mdogo wa bidhaa awe na nidhamu ya fedha kuliko Afisa wa Serikali?’
Majibu ni mengi. Moja ni uhakika wa kipato. Kwamba [mfanyakazi] una uhakika wa kupata mshahara mwisho wa mwezi hilo pekee linaweza kutosha kukuondolea nidhamu ya fedha.
Mjasiriamali/mchuuzi anaweza asiwe na uhakika huu. Kutokuwa na uhakika na kipato kunamwongezea umakini wa kutumia vyema kile anachokipata. Kwa mfano, lazima ahakikishe kile alichonacho kinazalisha kumpatia faida itakayomsaidia kuendeshea maisha yake.
Hapa ndipo ilipo tofauti baina ya wafanyakazi na wajasiriamali. Mfanyakazi unaweza kutumia kila senti unayopata kwa matumaini ya kupokea mshahara mwisho wa mwezi.
Mchuuzi hawezi kuthubutu kufanya hivyo. Kwake, kile alichonacho ni mbegu ya kupanda kumpa uhakika wa kesho.
Kwa hiyo utaona mazingira ya kazi uliyonayo mfanyakazi hayakulazimishi kuwa na nidhamu. Ili uweze kujenga nidhamu hiyo unahitaji kufanya kazi za ziada. Usipofanya maamuzi ya dhati, ongezeko lolote la mshahara haliwezi kukupa unafuu wa maisha.
Hapa tunapendekeza mbinu nne unazoweza kuzitumia kukabiliana na ukosefu wa nidhamu ya fedha. Mapendekezo haya manne yanadai mabadiliko makubwa ya tabia. Bonyeza hapa.