Sergeant Stonebridge
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 573
- 5,017
L
Wana JF
Habarini!
Leo ningependa sana ni'share na nyie mambo makuu matatu ambayo yanakamilisha ndoa
Hii
ni kwa mujibu wa Biblia najua siku hizi watu wengi sana wanashauku ya kuingia ktk maisha ya ndoa!
Hili ni jambo jema
Ndoa zipo za aina nyingi sana kimila, kidini, n.k
Ndoa nyingi ni Mme na mke
Japo zipo ndoa ya Mme mmoja na wake wengi (zaidi ya mmoja)
Biblia inasema mambo makuu matatu (3) tena yanafuatana huwezi kuruka moja, ni lazima yote yaende ktk mpangilio.
Na haya hayapunguzwi ama kuongezwa!
Mambo hayo ni ili ndoa yako idumu hasa kwa mtu ambaye haukuzaliwa nae tumbo moja!
Mambo hayo ni:
1: ACHA;
Hili ni la kwanza,
Utawaacha baba yako na mama yako
Ndugu zako, marafiki na utaacha mila na desturi!
Hii ni kanuni, hapa ni lazima uache mambo yote uliyoyazoea hasa ikiwa sio dhambi kuyaacha!
Ndoa ni kazi ya kutafuta furaha ya mwenzako.
Hivyo yale mazoea yako yote ni lazima uadhimie kuyaacha hasa kwa mtu ambaye hamkulelewa pamoja.
Ili uishi ktk ndoa ni lazima ukubali kuwa hili linamuudhi mwenzako, hili halimfurahishi, hili linamkera hivyo unapaswa kuyaacha yote!
Tatizo la wanandoa wengi wanaingia ktk ndoa na makororo yake yote
Ndoa haiendi! hivyo ni lazima ubadilike na uyaache.
Ndoa nyingi ambazo wanandoa wameshindwa kuyaacha mambo yao ya kale ama wameshindwa kuwaacha wazazi wao
Ni dhahiri hiyo ndoa INA misukosuko na misuguano mingi sana tena isiyoisha.
Hivyo wanaooana ni lazima wakubali kuacha!
Ili waishi ni lazima waadhimie kuyaacha!
2: KUAMBATANA;
Hii ni kanuni ya pili baada ya kuwaacha baba na mama, kuacha mazoea, n.k
Pia ni lazima muambatane wote, mke na mme
(Mwanzo 2 : 24)
3: KUWA MWILI MMOJA;
Baada ya kuacha, kuambatana sasa mnakuwa mwili mmoja.
Tatizo la vijana wengi siku hizi wanaanza na hili la tatu
Wananzia Kuwa mwili mmoja!
Hawajaacha na wala wajaambatana!
Haya mambo hayapunguzi ama kuongezwa!
Ndoa yako itadumu iwapo tu utafuata huu mpangilio wa Biblia!
Ndoa sio majaribio, wala sio sehemu ya kuoneana, mke sio mfanyakazi bali ni msaidizi tu!
Mpende sana mke wa ujana wako!