Mambo makuu 39 yanayovunja mahusiano

Mambo makuu 39 yanayovunja mahusiano

Hazard CFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
16,625
Reaction score
38,751
MAMBO YANAYOVUNJA MAHUSIANO

1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi
wako.

2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.

3. Ubishi usiokuwa na maana.

4. Kupenda kujihesabia haki.

5. Kutokubali makosa.

6. Kutokuwa na roho ya msamaha.

7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.

8. Usaliti wa mapenzi.

9. Kuigiza kupenda.

10. Kutomheshimu mwenzi wako.

11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.

12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.

13. Kuwa na jeuri.

14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]

15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]

16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.

17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]

18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.

19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika maisha yenu.

20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.

21. Kuwa na ahadi za uongo.

22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.

23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]

24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.

25. Maudhi ya mara kwa mara.

26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.

27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.

28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.

29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]

30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.

31. Kutokuwa na shukrani.

32. Kutokujua gharama za upendo.

33. Kuwa na wivu wa kijinga.

34. Kuwa mbinafsi.

35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako.

36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.

37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.

38. Kutokukubali kujifunza.

39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.

Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku
atachoka.

Maana hana moyo wa jiwe bali ana
moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na
kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na kupendwa katika maisha yao.
 
Yote kwa yote kuna point muhimu kupita zote hujaiweka.

miss chagga tusaidie hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kushinda na kukesha whatsapp, kulala na mwenzio utadhani unalala na rafiki ako mlosoma wote seminary

41. Kushinda na kukesha whatsapp, kulala na mwenzio utadhani unalala na rafiki ako mlosoma wote seminary
 
Mh! Hiyo namba 32 yaweza kuwa kiini cha matatizo yote hayo.
MAMBO YANAYOVUNJA MAHUSIANO
1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi
wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako
katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya
nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako
[ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa
pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako
[kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa
mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika
maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa
kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira
yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi
kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara
anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako
[kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa
kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na
umuhimu wake.
Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya
watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika
maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku
atachoka, maana hana moyo wa jiwe bali ana
moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho
wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu,
vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na
kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na
kupendwa katika maisha yao.
 
Yaani vingi ulivyoongea vipo kwa manzi yangu.........dah ni shida......nitamuonyesha hii post yako best...........kuna moja haujalitaja hapo......ni swala mwanamke kuwapa kipaumbele ndugu zake sana na umuhimu kiasi kwamba mumewe anajihisi hana umuhimu......yaani unakuta jitu ni busy na kuongea na ukoo na familia yake masaa 24......hadi anasahau maneno ya bible yanayosema kuwa utaacha ndugu,jamaa na familia yako utaambatana namumeo kujenga mji wako..........sasa jitu liko busy na familia yake huo muda wa kujenga familia yake utatoka wapi...........yaani ni upuuzi wa hali ya juu sema ndio mademu wa kizazi hiki ambao hufundwa siku moja tu ya kitchen party........siku zingine ni jeuri na kuishi maisha ya kucopy na kupaste kutoka kwa manunga yembe wasiojua kesho yao wala jana yao inasemaje.........pumbavu....pumbavu sana!
 
Wakipita hapa........
 
Back
Top Bottom