funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 38,534
- 31,198
Habari zenu wadau!
Niende kwenye mada moja kwa moja...
Inasemekana kuwa Chadema ni moja ya Chama ambacho kilipoanzishwa kiliogopewa sana hata na hayati mwalimu Nyerere.
Kuogopwa huku kulitokana na katiba na mikakati iliyojiwekea kipindi kile wakati inaanzishwa.
Ni vyema sisi wadau wa siasa za Tanzania tukajadili kwa nini Chadema imeangukia kwenye kapu lile lile la vyama laghai vya kisiasa nchini ?
Yafuatayo ni mambo makubwa ambayo sio propaganda yaliyoifanya Chadema kuwa au kuangukia kwenye vyama vya siasa ambavyo ni uchwara.
1- Chadema kushindwa kuonesha utofauti kwenye halmashauri au majimbo iliyoyashika.hapa naongelea majimbo ya moshimjini,Tarime na Karatu.
sana sana moshi mjini na hasa karatu ambapo imegeuka kuwa halmashauri ya kifisadi kuliko zote kwa mujibu wa CAG.
Ukiacha ufisadi ...bado hatujashuhudia utofauti wa kimaendeleo katika halnashauri hizi pamoja na kushikiliwa na Chadema ambao walijinadi kuwa ni mahiri katika maendeleo na udhibiti!
2-Kumpokea lowasa na kumfanya mgombea uraisi bila kufuata taratibu za chama.hili lilliwafanya waonekane kuwa ni chama kichanga kinachotegemea CCM wagombane ili wapate mgombea uraisi.
3-Kuachana na vita ya ufisadi,ubadhirifu,uzembe na ukwepaji kodi.
Baada ya kumuweka mgombea urais mwenye tuhuma nyingi za ufisadi na ubadhirifu Chadema ilipoteza uaminifu kutoka kwa jamii inayojitambua!
Baada ya kumuweka mtu waliyemtukana kwa miaka zaidi ya mitano kuwa mgombra urais basi kila anayejitambua aliwapa mkono wa kwa heri.
4-Ugomvi na Dr Slaa
Huyu alikuwa ni think tank na mtendaji wa kipekee ndani ya Chadema.Kushindwa kumshawishi abaki ndani ya Chadema pamoja na kupiga goa za anga lilikuwa ni kosa kubwa sana
5- Kutetea yale waliyokuwa wanayapinga na kuyapigia kelele
Hapa wananchi na wasomo wanaojitambua wamechanganywa vilivyo baada ya kuwaona Chadema wakitetea ufisadi,uzembe kazini na hesitationa ya kuchukua hatua.yaani chadema ina-sympathise na wakwepa kodi waliopelekwa mahakamani na wafanyakazi wazembe waliotumbuliwa.
6-Uteuzi wa nafasi ndani na nje ya Chama.Hapa malalamiko yapo kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum ambao haujazingatia weledi au uzoefu ndani ya chama.wapambanajoi wanapigwa chini halafu ndugu na vimada wanapewa nafasi.
Haya ni machache tu kati ya mengi makubwa ambayo yanaoangusha Chadema na kuifanya kuwa CCM ile ya zamani (sio hii ya Magufuli)iliyochikiwa na wananchi.
Haya ni maoni ya Mwanachadema asilia niliyeongea naye..!
Ukiwa na sababu zaidi ya hizi share with us!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA