- Ni wakati wa watu kukosoa na msiogope kukosoa.
- Viongozi msiogope kukosolewa na msiwachukie watu wanao wakosoa nchi ni yetu sote.
- Wenye madaraka chukueni maamuzi mnayoona ni sahihi, siyo yale ya kumfurahisha Rais.
- Wapo watu wenye uwezo wa kusema semeni acheni woga.
- Wapo watanzania wenye uelewa mkubwa, msisubiri tupotee njia ndipo mseme.
- Naweza kuwataja hata majina watanzania wenye uelewa mkubwa, msikae kimya.
- Rais ana nia njema na nchi hii, lakini akikosea katika maamuzi mwambieni.
- Rais siyo malaika tumwombee watanzania awe na roho ya kuvumilia kukosolewa.
- Chondechode watanzania wenye weledi tafadhari semeni.
- Tafadhari semeni, ukimya ukiendelea mkamfanya Rais kama malaika tutajuta mbeleni.
- Maamuzi ya makosa yanafanyika mnakaa kimya, tunaoumia ni sote.
- Yapo mengi Rais anakosea hamtaki kusema, hili la kuzuia kuigiza sukari mlilijua mkawa kimya.
- Yapo mengi hayaendi sawa, madhara yake si ya muda mfupi kama ya sukari. Yatakapo tokea tutashindwa kuyarekebisha.
- Sukari ikikosekana tunaanza kuagiza mengine ni vigumu kurekebisha
- Tukivuruda kuwapa elimu bora kizazi cha baadae hatutaweza kurekebisha kama sukari.
- NITAENDELEA NIKIPATA NAFASI TENA KWA KUTOA MIFANO MAENEO TUSIYOENDA SAWA ILI WENYE WEREDI LABDA WANAWEZA KUSEMA, NAWATAKIA MCHANA MWEMA.