Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 73,801
- 225,569
Very interestingNilitofautiana na mke Wangu na yeye kurudi kwao... nikakaa miezi kama sita hivi kuomba kupatana na akasema niende tukutune sehemu... nikajua basi mambo freshi... nikakata ticket ya ndege kwenda kumuona... Nikiwa ndani ya ndege na milango imefungwa, Mara mke wangu ( tuliyetengana) akatuma txt kusema hataki tena tuonane... nikamwambia niko ndani ya ndege , milango imefungwa na siwezi ahirisha safari.
Gafla akazima simu na pia kuniblock... Nikaona isiwe tabu... nikaendelea na safari hadi mwisho. Nikafika na kwenda hotelini mbali kabisa na nyumbani kwao na ambako sikumtaatifu...
Nikiwa hotelini Usiku mimi Mwenyewe Saa 9 usiku nikaamka...moyoni Kwangu nikawaza, sasa nimekuja na kilicho nileta sijakipata... asabuhi nitarudi zangu airport na basi talaka nitampa...
Nikajiuliza, ni nini haswa sijakifanya , Mara wazo likaniijia, sara...sasa nikasema, nisari sara gani ambayo Mungu atanijibu... sikujua... Nikaanza ku- google, zikawepo Sara nyingi... nilipo anza kuchagua Mojawapo na kuanzia kuisari nikahisi sina connection na ninacho kisari... nikapitiwa na usingizi, nilipokuwa ninelala nikaota kwamba nisari tena. Swali likaja ndotoni, sara gani...jibu likawa... Mungu ni baba kama baba yangu na pia ni mwenye huruma kama mama yangu...siku za utotoni, ili nimuombe baba pesa , nilikuwa either napitia kwa mama au directly . Sasa nikawaza, nitatumia njia ya direct kuongea na Mungu directly .
Nikaamuka toka usingizini, nikaa kitandani... ndani ya hotel ile kulikuwa na kabati kubwa . Nikaliangaliwa na kikahisi hofu fulani hivi... basi nikajisemezea mwenyewe huku nikiliangilia kabati like na kusema maneno haya, “ ewe Mungu, najua umo ndani yangu kama nguo zilivyo ndani ya kabati hilo. Waijua nafsi yangu na kila kilichomo ndani yangu, wajua pia ni nini kilicho nileta hapa na chanzo cha mimi kutengana na mke wangu, wazo la kupatanishwa pia lilikuja tu kichwani kama jua la asubuhi... nisamehe nilipokukosea na mapenzi yako yatimie kwa namna itakavyo kukupendeza.”
Hiyo ilikuwa kama saa 10 alfajili hivi... baada ya hapo nikalala tena na asubuhi nikarudi tena airport ...kufika aitport, ndege hakuna - cancelled hadi kesho yake...nikaamua kutafuta hotel Nyingine, hii ilikuwa saa 5 asubuhi yake... sasa nikajisemea... hotel nyingi check in ni saa nane, Hebu ngoja nitafute sehemu nipate chakula cha mchana... nikaipata restaurant - nikala chakula. Baada ya kula na kulipia nikaanza safari ya kurudi hotelini huku nikisema moyoni, usiku ule nilijihisi siko pekee na nikasari . Niliyemwomba ni baba aliye ndani ya mwili wangu, iweje anichunie hivi bila majibu? Mke wangu kani- block na simu kazima , hata kama mimi ni mkosaji , nikijirudu na kumuomba baba yangu huwa anasikiliza kilio changu...
Gafla bin vuu namuona mke wangu mbele yangu ... sote tukapatwa na msituko wa ganzi na tukasimana bila kuongea neno kwa dakika 3 hivi tunaangaliana tu ...
Baada ya hapo nikaamuliza, vipi ulikuwa unanifuatilia? Akajibu hapana, nilikuwa njiani kuelekea kanisani misa ya mchana... akaniuliza na wewe...nikamueleza story ndefu ... kama yuko tayari tutaongea baada ya kanisa lake... akasema sawa, nisubiri hapa hapa nitarudi baada ya saa moja...
Kweli akaenda na baada ya saa moja akarudi... nikamwambia twende restaurant, akagoma...akasema tu tutembee kwenye bustani huku takaongee... basi tukaenda...
Tukaongea mambo mengi, gafla bin vuu, vikongwe wawili wakapita mbele yetu sisi tukiwa tumekaa benchi... mmojapo akasema, ”you reminded us the good old days ...”
basi mimi na mke wangu tulipatana na tukaa tangu saa 9 mchana hadi saa 9 usiku kwenye bench hilo bila kuondoka...
ndege yangu ilikuwa saa 2 asubuhi...mke wangu tukarudi sote . Ni Miaka 15 toka siku hiyo hadi sasa tupo pamoja na wenye Furaha na watoto 3.
Tokea siku hiyo, nilijufunza na namna ya kuongea na Mungu. Na tangu siku hiyo , nikiomba kwa style ile, huwa najibiwa haraka Sana... na nime- conclude , sara si lazima kuomba hadi magoti yachubuke...ni style ya uombaji na namna unavyomleta Mungu karibu nafsini kwako...
sahamani -ilikuwa ndefu...
Sent using Jamii Forums mobile app