Mambo gani umewahi kumuomba Mungu na akakujibu papo hapo?

Yanatokea sana. Huwa kuna nyakati nafikiri pengine sisi binaadamu bado hatujamuelewa Mungu, uwezo wake, namna anavyofanya kazi na zaidi bado sana kujielewa sisi wenyewe na ukomo uwezo wetu. Naamini tuna uwezo mkubwa sana kuliko tunavyojijua. Kaka Pascal Mayalla aliwahi kuweka uzi humu kuhusu psychic powers......ipo relevant sana.

Kuna nyakati naweza kutamani mtu atende jambo fulani (lenye maslahi kwangu), basi nikizama kwenye hizo fikra tu, nakuta mtu huyo anatenda exactly to the script niliyotaka.....ni kama nimempa maelekezo telepathically. But nafikiri nahitaji kuninvest zaidi kujua namna na nyakati nguvu hiyo (kama kweli ipo/ninayo) inavyofanya kazi na kama naweza kuwa na control nayo zaidi (maana saa nyingine hata uzame vipi, mambo hayaendi utakavyo). Inanitokea mara nyingi sana kumuwaza mtu na kisha mtu huyo akanipigia simu muda huo huo au mara nyingi unatembea tu kwa mambo mengine, lakini baada ya kumfikiria au kumkumbuka mtu fulani, mbele kidogo au baada ya muda mfupi unamuona au kukutana nae. Haya yanatokea mara kwa mara na inakuwa vigumu sana kuamini kuwa ni coincidences tu. Nahisi kuna nguvu bado hatujaielewa vizuri.

Well, pengine ni coincidences tu.

Naomba link ya huo uzi please
 
Eee jaman nyie. Mungu ni muweza. Mungu anajibu maombi.

Nimemaliza chuo, nkaenda kijijin kwanza. Baadae nkaenda kukusanya vyeti vya A-level nivitume sehemu. Baada ya kuvipata nkaingia mikoa ya pwani. Nkafika usiku saa saba Mwenyeji wangu hapokei simu na alipokua anaishi kahama mchana wake (maana nilkua napajua nilishwah kwenda). Mkosi ukawa umeanzia hapo.

Kesho yake nikalipia room...maisha yakaanza. Omba kazi..hakuna..tafuta kazi..wapi. Pesa ikakata. Nkaanza harakat za jufundisha tuition. Sh 300 kwa siku angalau za unga. Ndani ya week walkuja watoto wengi ila baadae number ikakata. Heheheh mkosi mwingne.

Pesa ya matumizi ikakata kabisa. Yaan inaamka huna mia. Basi nikkua na simu yangu nkaiweka bond nkapata 100k. Baadae hela nkawekeza kwenye boashara flan iv basi bana hela ikawa ya kula..ikakata.

Nkaanzisha kuchoma mihogo. Siku ya kwanza faida, ya pili faida kubwa...siku ya tatu wateja wakawa wanarudisha mihogo kwani ni michungu. Mikosi ikaongezeka zaidi. Biashara ikafa sikuendelea.

Basi bana hela ya kulipa deni ikapotea. Mdai anataka hela. .hela sina. Simu ikauzwa 50k. (Niliinunua 330k). Ikatakiwa niongeze 60k kulipa deni. Nkakataa.

Basi jamaa angu akaniambia tuingie shamba kulima. Nkaingia shamba nkawa nakaa huko huko kwenye vijibanda kwani town life gumu siwezi lipia kodi.

Nkawa nalima na kuchoma mkaa, jua mvua vyote vyangu. Njaa kali nkawa nang'oa visiki na kuchoma mkaa pamija na kuokota kuni na kuzileta mjini nipate angalau unga. Nkalima mahindi ekari mbili na nusu ivi nkaambulia nusu gunia. Mkosi.

Maisha yakazidi kua magumu sana. Nkawa naishi katikati ya mapori, maji ya shida, chakula cha shida, nikachakaa sana. Nakumbuka siku moja nikiwa nakata kuni nuliwahi kutaka kujidhuru baada ya stress kunizidi.

Basii bwana siku moja nkashikwa na msongo wa mawazo kwenye kibanda changu. Nkaanza kujilaani na kujiona sina thamani tena. Sina hata godoro. Nkalia sana. Nkapiga magoti nkimlilia Mungu sana. Nkamkumbusha jinsi navoteseka, jinsi alivoniacha niteseke. Nkamkumbusha mambo kadhaa yaliyoandikwa kwenye biblia. Nkamlilia sana kama mtoto anavyomlilia mama yake miguuni pake. Ukaongea nae pale chini kibandani kama saa nzima. Nkaongea mambi mengi sana.

Nikamwambia Mungu kwamba "eeh Mungu mimi sio mnyama wa kukaa porini, mm sio nyoka, sio swala wala mnyama yyte wa kuishi maporini. Nimechoka kuishi porini. Sitaki kuishi huku. Naenda mjini sitaki kurudi porini. Nikienda huko unipatie kazi".

Basi baada ya maombi ya muda mrefu nikapanda mjini kwa jamaa zangu flani iv na mzigo wangu wa kuni. Nilivyofika nkakodi baiskeli naktembeza kuni...nkauza na kurudi kujipumzisha kwa hao jamaa. Basi nkachaji kijisimu changu nkamtafuta mzee mmoja ivi nilipataga namba zake ktka harakati za kutafuta kazi. Ilivyompigia tu simuna kujitambulisha...akaniambia siku zote hizo ulkua wapi? Mbina tumekutafuta na hupatikani?

Dah kumbe naishi porini na kutaabika kumbe huku mjini watu wananitafuta nikaanze kazi. Basi bana yule mzee akaniambia kesho nenda ofisini ntaongea na meneja akupokee na namba ake ntakutumia. (Nikafurahi sana meno yote nje).

Nikamshukuru Mungu sana kwa kujibu maombi yangu papo hapo na tangu siku hiyo sijarud porini wala kwenye kile kibanda. Mpaka leo nafanya kazi kwenye hii taasisi.

Eeh Mungu nashukuru sana kwa yote uliyonitendea. Nimekuasi Mungu, natenda maovu mm. Eeh Mungu usinikasirikie na kunipoteza eeh BWANA. Unipe moyo mkuu wa kuenenda ktk njia zako. Uniokoe wala usiniache mbwa mwitu wakanirarua.

Eeh BWANA mm ni mkosefu na sipaswi hata kulitaja jina lako tukufu. Eeh Mola nirehemuna unifungulie njia.
 
Mungu ni mwema sana na anajibu kwa wakati wake alioupanga
 
Mie mara zote maisha yangu ni majibu tu ya Mungu hapa nilipo ni mwaka wa pili toka 2018 sina kazi ni mke na watoto watatu....ila hatujawahi kukosa mlo hata siku moja ni lakaa 3 daily.
Japo sio mlo kama ule wa zamani lkn tunapata.
Sio maisha mepesi kivile lkn tunamshukuru Mungu hata magonjwa yamepungua hakuna cha malaria wala tumbo?

Kuna kipindi nilikuwa sina kazi nilituma maombi mpaka wife akachoka kunipelekea posta office.

Sikukata tamaaa aisee niliendelea kumuomba Mungu hukunikiomba kazi mbalimbali aisee zilikuja fumuka kazi kama 5 hivi zote natakiwa nikapige interview moja sikupiga kabisa wakampa subcon aongee namini nikakataa maana salary yao niliona ndogo.

Basi wakatafuta subcon mwingine wakamwambia huyu jamaa tunamtaka jamaa wakanichukua kwa dau langu....!

Ya serikalini ndio nikuwa naitaka nikaikosa,wengine kama azam media nilipiga chini,tumbaku moro, nk...!

Kikubwa nikuomba Mungu huku unaplay part yako,kama mtaani ingia pambana,kama washikaji ndio michongo yako ilipo nenda nao sambamba nk Mungu anasikia na anajibu kwa wakati wake....!

Kila mtu ana nafasi sawa mbele za Mungu makanisani na misikitini tunaenda kufuata miongozo,tunakumbushwa,tunaonywa nk lkn hakuna maombi yaliyo bora kama yako mwenyewe badala ya kutaka kuombewa kila siku kwa wachungaji au mashehe.

Jinyenyekeze mbele ya Muumba wako lia ikiwezekana ikane nafsi yako hakika Mungu si kiziwi atajibu tu Maombi yako either sasa,baadae nk anajibu atakavyo yeye wala usimlaumu.

Na sie sote Mungu keshawahi tujibu kwa nyakati tofauti ila tunajisahau tunazani ni kwa uwezo wetu badala ya kufuata njia zake tunaenenda kwa njia zetu hata sadaka ya shukrani tunasahau kumtolea.

Nakumbuka nilipata 6M ktk madai yangu baada ya kumuomba sana Mungu hapo ni madeni lukuki, tunawaza na mwenza wangu mie nataka tutoe shukrani yeye anataka tutoe fungu la kumi. Mie shukrani nataka nitoe hata 2k yeye fungu la kumi 6K patamu hapo vimeo vya madeni vimeaimama wima hata 6M haitoshi...!

Nikampa ushindi maana ile hela alinisusia,baada ya kumpa yote akatoa fungu la kumi akalipa madeni tukawa bankrupt.

Pambana sana sana huku tukimuomba Mungu life likawa gumu kama chuma cha pua madeni hayajaisha ila kula tunakula japo kwa msuli,madogo wako private school nakoma tu maana sitaki waende kayumba...! kudadeki...

Uza gari,lipia vimeo,bado ngoma ngumu,uza ardhi madogo wakaingia school....! tena, maana niliwatupa seminari huko mikoni,..! mie nipambane mjini na mama yao mara paaaap covid_19 anza tafuta nauli warudi town.

Juzi alimanusra niuze tena sehemu maana madeni yanaandamana baada ya corona,unajua nini Mungu ni mwaminifu kanipa shavu sehemu nimeghahiri hata kuuza maana nilikuwa nipate si chini ya 10M.

But sikujiandaa kisaikilojia jinsi ya kuitumia zaidi ya kulipa madeni,now najiandaa ku utilize eneo langu kwa biashara bustani za mbogamboga!

Msichoke kuomba hata kama huoni mwanga mie nimeuona utukufu wake ktk nyakati nyingi sana!
Tatizo letu moja tunafail kumrudishia utukufu wake lazima utafail tu kama unamtegemea yeye maana anakuhitaji uwe mfano kwa wengine ila kama humtegemei yeye basi utafaikiwa ama kufail kutegemea na principle zako.

Nakipata mshiko lazima nikatoe sadaka kwa matendo mema aliyonijibu maaana sio kwa lumba nililopitia.....!

week ya pili sina sina issue job naenda hata nauli na msosia wa mezani kwa kweli ni utukufu wake tu hata ikiwa ni kqa kukopa maana ntakaa sawa tu hapa nina counter book maisha yajayo mipangu lukuki.

Tuendelee Kumuomba Mungu,kumsifu na kumshukuru.....haya mambo matatu muhimu sana....!

Shuhuda ninazo kibao hapaaa rafiki yangu alikuwa ananiombea siku akasema nimekuombea sana umefanikiwa unaleta sharau nikamjibu hata mie nilikuwa naomba akasema sitakuombea kamwe imagine hapo huna kazi,nikasimama ktk imani yangu nikamuomba Mungu kwa dhati na kukimbizana na michongo ndio hivyo kajibu....!

Sitaki hata kumuuliza ulikataa kuniombea kwani vipi mbona kanijibu?

Sifa na utukufu ni yeye aliyeziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo.....!

Thanks Almighty God for everything you did in mylife no one no one like you ni wewe pekee unayetakiwa kuabudiwa na kushukuliwa....!

Twendeleze mombi wadau tufanikiwe kimasihara,ukiona ujajibiwa kuna mtu buza mpalamba kajibiwa relax your time will come...!

Dadii.

Hongera sana umepata mke hakika
 
Daah, Mie kwa upande wangu niliwahi kukwama katika lift ilikuwa asubuhi saa moja. Watu wengi hawajafika kazini.
Nilipoliita Jina la Bwana Yesu na Kumuomba MUNGU, ghafla mtu mmoja sijui alipotokea akapanda mpaka ghorofa ya mwisho kwa miguu aka reset lift ile ikaporomoka mpaka first floor.
Hapo tukatoka tukiwa tumelowa Jasho.

Hakika MUNGU ni mkuu.
 
Mungu atabaki kuwa mungu hata kama hakutenda kama tunavyotaka,, mungu ameniepusha na kifo mara mbili kwa mwaka huu tuu, mara ya kwanza nilitumbukia kwenye kisima kirefu cha maji nilimwomba mungu nikajikuta Nipo juu naelea kwenye maji, ya pili nilipata ajali ya gari nilianguka kwenye lami nikaangukia kichwa mungu alivyo mkubwa sikuvunjika wala kupata shida yoyote kwenye kichwa,,, kwakweli nina kila sababu ya kuendelea kumshukuru mungu kwa zawadi ya uhai,
 
Nakumbuka mwaka flani ivi nmemaliza chuo sina mbele wala nyuma,
Nikaanza biashara ya kuuza vitu shuleni siku io nmeenda na vitu vyangu kuuza lakini sikuuza ata kimoja,na nilikua na vitu vingi vya kula na vinavyopendwa na wanafunzi,
Nilitoka pale nikakaa kwenye mti nikalia sana na nikamwambia Yesu naomba univushe apa,naomba unipe kazi na nisirudi apa tena.
Baada ya mwezi mmoja nikapata kazi nzuri sana kwa namna ya ajabu mno.
 
Nimekiweka hapo
Siku moja usiku Niliwahi umwa kichwa sanaaaa mwezi huu huu wa saba kama sikosei. Usiku ule nikashika kichwa nikaomba Mungu nikiamka naomba kichwa hiki kiwe kimepona, nikalala zangu yan apo nimepiga panado tuu. Aisee naamka asbuhi kichwa kipo fresh kabisaaaaaa yan hakuna maumivu yoyote nikasema Mungu yupo na anajibu maombi.
Mengine mengiii tu hadi ninachofanya sasa ivi ni majibu ya Mungu siaminigi katika uwezo wangu naaminigi ni Mungu tu ndo ananisaidiaga
 
Kuna muda bwana unaweza ukabanwa na mambo magumu katika maisha, na ukashindwa njia zote hatimae ukaamua kumuomba Mungu moja kwa moja na akakujibu?

Mimi kuna matukio kadhaa aisee naamini moja kwa moja Mungu ndiye alinisaidia.

1. Kukingwa na mvua kubwa
Mnamo mwaka 2008 nilikuwa katika moja ya shughuli za utafutaji katika Kijiji kimoja kinaitwa MKANYAGENI huko Tanga. Tulikuwa katika mapori fulani huko tukichana mbao. Lakini siku mbele baadae nilianza kuumwa na homa kali Sana. Jamaa zangu wakaamua kuniruhusu na kurudi mjini ili nisije nikawafia kule.

Safari ilikuwa Ni ndefu na ni ya mguu, nilitembea kilomita kadhaa na hatimae nikashindwa kabisa kutembea kutokana na kuishiwa nguvu.

Nikiwa nimekaa chini sijui cha kufanya, angani ilitanda mvua moja kubwa Sana, dakika chache baadae ikaanza kunyesha. Pale nilipo hapakuwa na nyumba wala sehemu yoyote ya kujizuia na mvua.

Kiukweli niliamua kumwambia Mwenyezimungu kana kwamba naongea na mtu. Nikasema "Ewe Mwenyezimungu, nakuomba uizuie mvua hii mpaka ntakapofika mjini kwani Kama ikininyeshea hapa hakika sitoweza hata kutembea"

Basi mvua ile ilikata na nilijikongoja mpaka kufika pale MKANYAGENI majira ya saa 2 usiku tangu saa 10 jioni.

Nilipofika tuuuu, aisee mvua iliachiwa sijapata ona... Daaah nkasema kweli Mungu yupo.

2. Chakula cha hapo kwa hapo
Mwaka 2015, siku moja nikiwa sina hata mia mbovu. Mipango yangu yote imepinda. Njaa inaniuma sijakula siku nzima mpaka nikafikia hatua ya kulegea kwa njaa.

Niliamua kumwambia Mungu nisaidie, nitakufa na hii njaa mimi mja wako.

Nilitoka kuelekea nisikokujua, lakini baada ya dakika kadhaa niliamua kurudi tu geto.

Aisee kitu cha kushangaza WALLAAHI nilimkuta mtoto wa jirani pale mlangoni kwangu akinisubiri na akiwa ameshika bakuli ya wali.. kwa kudai kuwa amepewa na mama yake aniletee... Nilishangaa Sana maana huyo mama wala Sina mazoea nae wala HAKUWA jirani wa karibu...

Nkasema kweli Mungu amejibu maombi. Asante sana Mungu.

3. Kuokoka kufumaniwa na mke wa mtu

Hii ilikuwa ni mwaka 2017... Sitosahau.

Nikiwa ndani kwa mtu na mke wake.. Jamaa hakuwa mji ule kabisa alikuwa kikazi mji mwingine. Lakini hammad ghafla tukasikia sauti za honi ya gari getini ikimaanisha kuwa msela ameshafika.... Yule mama alikwenda kufungua geti nikiwa nimejificha nyuma ya friji nikisali maombi yote.

Mara mprado huo ndani mzee kaingia..

Daah kumbe alisahau simu mfuko wa mbole katika duka flan huko mjini, ikabidi awashe tena gari arudi kuchukua kwa ajili ya matumizi ya kesho.

Nafkiri mbio nilizotoka nazo pale Ni zaidi ya BOEING 787. Na ikawa mwisho wa kudate na Iile shuga mamy. Hakika mzee angenikamata Ningekufa tu.

Acheni wake za watu hata wakijirahisisha.

Ila jaman MUNGU ANAJIBU MAOMBI kwa aombae kwa dhati.
Siku moja usiku Niliwahi umwa kichwa sanaaaa mwezi huu huu wa saba kama sikosei. Usiku ule nikashika kichwa nikaomba Mungu nikiamka naomba kichwa hiki kiwe kimepona, nikalala zangu yan apo nimepiga panado tuu. Aisee naamka asbuhi kichwa kipo fresh kabisaaaaaa yan hakuna maumivu yoyote nikasema Mungu yupo na anajibu maombi.
Mengine mengiii tu hadi ninachofanya sasa ivi ni majibu ya Mungu siaminigi katika uwezo wangu naaminigi ni Mungu tu ndo ananisaidiaga
 
Nilitofautiana na mke Wangu na yeye kurudi kwao... nikakaa miezi kama sita hivi kuomba kupatana na akasema niende tukutune sehemu... nikajua basi mambo freshi... nikakata ticket ya ndege kwenda kumuona... Nikiwa ndani ya ndege na milango imefungwa, Mara mke wangu ( tuliyetengana) akatuma txt kusema hataki tena tuonane... nikamwambia niko ndani ya ndege , milango imefungwa na siwezi ahirisha safari.
Gafla akazima simu na pia kuniblock... Nikaona isiwe tabu... nikaendelea na safari hadi mwisho. Nikafika na kwenda hotelini mbali kabisa na nyumbani kwao na ambako sikumtaatifu...
Nikiwa hotelini Usiku mimi Mwenyewe Saa 9 usiku nikaamka...moyoni Kwangu nikawaza, sasa nimekuja na kilicho nileta sijakipata... asabuhi nitarudi zangu airport na basi talaka nitampa...
Nikajiuliza, ni nini haswa sijakifanya , Mara wazo likaniijia, sala...sasa nikasema, nisali sali gani ambayo Mungu atanijibu... sikujua... Nikaanza ku- google, zikawepo Sala nyingi... nilipo anza kuchagua Mojawapo na kuanzia kuisali nikahisi sina connection na ninacho kisali... nikapitiwa na usingizi, nilipokuwa ninelala nikaota kwamba nisali tena. Swali likaja ndotoni, sala gani...jibu likawa... Mungu ni baba kama baba yangu na pia ni mwenye huruma kama mama yangu...siku za utotoni, ili nimuombe baba pesa , nilikuwa either napitia kwa mama au directly . Sasa nikawaza, nitatumia njia ya direct kuongea na Mungu directly .
Nikaamuka toka usingizini, nikaa kitandani... ndani ya hotel ile kulikuwa na kabati kubwa . Nikaliangaliwa na kikahisi hofu fulani hivi... basi nikajisemezea mwenyewe huku nikiliangilia kabati like na kusema maneno haya, “ ewe Mungu, najua umo ndani yangu kama nguo zilivyo ndani ya kabati hilo. Waijua nafsi yangu na kila kilichomo ndani yangu, wajua pia ni nini kilicho nileta hapa na chanzo cha mimi kutengana na mke wangu, wazo la kupatanishwa pia lilikuja tu kichwani kama jua la asubuhi... nisamehe nilipokukosea na mapenzi yako yatimie kwa namna itakavyo kukupendeza.”
Hiyo ilikuwa kama saa 10 alfajili hivi... baada ya hapo nikalala tena na asubuhi nikarudi tena airport ...kufika aitport, ndege hakuna - cancelled hadi kesho yake...nikaamua kutafuta hotel Nyingine, hii ilikuwa saa 5 asubuhi yake... sasa nikajisemea... hotel nyingi check in ni saa nane, Hebu ngoja nitafute sehemu nipate chakula cha mchana... nikaipata restaurant - nikala chakula. Baada ya kula na kulipia nikaanza safari ya kurudi hotelini huku nikisema moyoni, usiku ule nilijihisi siko pekee na nikasari . Niliyemwomba ni baba aliye ndani ya mwili wangu, iweje anichunie hivi bila majibu? Mke wangu kani- block na simu kazima , hata kama mimi ni mkosaji , nikijirudu na kumuomba baba yangu huwa anasikiliza kilio changu...
Gafla bin vuu namuona mke wangu mbele yangu ... sote tukapatwa na msituko wa ganzi na tukasimana bila kuongea neno kwa dakika 3 hivi tunaangaliana tu ...
Baada ya hapo nikaamuliza, vipi ulikuwa unanifuatilia? Akajibu hapana, nilikuwa njiani kuelekea kanisani misa ya mchana... akaniuliza na wewe...nikamueleza story ndefu ... kama yuko tayari tutaongea baada ya kanisa lake... akasema sawa, nisubiri hapa hapa nitarudi baada ya saa moja...
Kweli akaenda na baada ya saa moja akarudi... nikamwambia twende restaurant, akagoma...akasema tu tutembee kwenye bustani huku takaongee... basi tukaenda...
Tukaongea mambo mengi, gafla bin vuu, vikongwe wawili wakapita mbele yetu sisi tukiwa tumekaa benchi... mmojapo akasema, ”you reminded us the good old days ...”
basi mimi na mke wangu tulipatana na tukaa tangu saa 9 mchana hadi saa 9 usiku kwenye bench hilo bila kuondoka...
ndege yangu ilikuwa saa 2 asubuhi...mke wangu tukarudi sote . Ni Miaka 15 toka siku hiyo hadi sasa tupo pamoja na wenye Furaha na watoto 3.
Tokea siku hiyo, nilijufunza na namna ya kuongea na Mungu. Na tangu siku hiyo , nikiomba kwa style ile, huwa najibiwa haraka Sana... na nime- conclude , sala si lazima kuomba hadi magoti yachubuke...ni style ya uombaji na namna unavyomleta Mungu karibu nafsini kwako...

sahamani -ilikuwa ndefu...
 
Siku moja usiku Niliwahi umwa kichwa sanaaaa mwezi huu huu wa saba kama sikosei. Usiku ule nikashika kichwa nikaomba Mungu nikiamka naomba kichwa hiki kiwe kimepona, nikalala zangu yan apo nimepiga panado tuu. Aisee naamka asbuhi kichwa kipo fresh kabisaaaaaa yan hakuna maumivu yoyote nikasema Mungu yupo na anajibu maombi.
Mengine mengiii tu hadi ninachofanya sasa ivi ni majibu ya Mungu siaminigi katika uwezo wangu naaminigi ni Mungu tu ndo ananisaidiaga
Amen
Glory to God

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom