Mambo Flani Hivi Yakufurahisha Katika Maisha...

holy holm

JF-Expert Member
May 6, 2017
4,792
9,080
1. Mganga wa matunguli tena masikini unamwendea akupe utajiri.
2. Daktari wa kinywa mwenye meno mabovu na kinywa kichafu
3. Baba aliye ajiriwa kama dereva wa medium shool au kampuni yoyote, watoto wake wanatembea km 2.5 kwa miguu kwenda shule kila siku.
4. Mtoto wa mmiliki wa shule amerudia darasa zaidi ya mara 3.
5. Mtoto wa mpiga masubwi matata na hodari nchini anapigwa na kuonewa na wenzake shuleni.
6. Daktari wa mifugo anaogopa mbwa balaah.. :D:D.
7. Muuza vitabu tena masikini anauza vitabu kila kona mojawapo ya vitabu hivyo ni kile kinacho sema "How to become a billionaire-namna ya kua bilionea"
8. Mmiliki wa Gym au mwelekezaji wa mazoez huko gym ila ana kitambi flani hivi..
9. Fundi seremala ambaye anakalia viti vya plastic home kwake.
10. Manager wa Vodacom anae tumia mtandao wa Tigo (jaza ujazwe)
maisha raha sana tupia na vyako
:D:D:D:D.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom