Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama msichana unafaa kuwa mke wake

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,859
19,726
MAMBO AMBAYO MWANAUME ANAFANYA KUKUTEST KAMA MSICHANA UNAFAA KUWA MKE WAKE

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.

9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia.

nime copy na kupaste mahali ,kama haijawahi kufika humu uburudikieni
 
Kuna kidada nilikichumbia, siku moja nikamwambia njoo kwangu hata siku mbili, akaja.

Siku ya kwanza natoka kazini saa 10 nakuta anaangalia Tamthilia Star TV, namuuliza chakula tayari, ananijibu alisubiri nifike home kwanza. Dah hapo nyama mbichi hajaipika wala kuikatakata, nikamwambia poa ngoja nikale vibandani, hapo ndio nilichoka akanambia uwai kurudi basi, uniletee na Pepsi, yan hasira nilizokuwa nazo anajua Mungu.

Kesho yake nikampa nauli ndio ukawa mwisho. Alilia lakn sikumwambia kosa lake mpk leo. Wanawake wanadhan huwa tunataka kuoa lexus wakati mwingine tunataka Hiace
 
Mh!uliyo yazungumza ni mazuri sana na kila mtu anapenda kutenda na kutendewa hivyo.

Shida ni mazoea kama utamfanyia hvivyo hata kwa wiki mara mbili hatokuwa na hamu ya kuoa huyo kwan kila kitu anapata.

Wanaume ni watu wa ajabu Mungu kawaumba kwa utashi sana,unaweza ukafanya hivo na ukaishia kuwa house girl wa wanaume na wapenzi.

Na walio wengi bila hiyo namba 8 hapo juu anaona bora muachane
Mleta uzi hakuna asie jua km uzinzi ni dhambi,watu wanafanya kiroho ngum tuu.

Uliyo yazungumza ni mazuri sana lakin yanafaida na hasara.kumbuka mapenzi sio ndoa.
 
Msisahau na mtihani wa kutupa pesa eeeeeee.
Wanaume na nyie...mnanitest ili iweje?
Wanawake wengine tunashindwa kutimiza majukumu yetu/yenu maana najua tuko wengi.
Nisipokufulia mie, atakufuli Mwajuma.

NB:
We kaka unaeitwa Said Khatibu wa Mwananyamala karibu na Royal bar, nimechoka kuwa housegirl wako....kama ndio ndoa inasubiriwa hivi, sitaki.
 
Kufuliana sio wala nn nimekaa sana uswahilini wakaka wakipata kazi wanapenda kukaaa unaona mdada anajitutumua anakuja fua weekend lakini mwishowe anaolewa mbandika kucha yeye zake kuingia night kali
Haya maisha hayana fomula muoaji anayake akilini hizi ni chache na wafuatiliaji wapo kiasi chake ila wengi wao hakunaga
 
Kuna kidada nilikichumbia, siku moja nikamwambia njoo kwangu hata siku mbili, akaja.

Siku ya kwanza natoka kazini saa 10 nakuta anaangalia Tamthilia Star TV, namuuliza chakula tayari, ananijibu alisubiri nifike home kwanza. Dah hapo nyama mbichi hajaipika wala kuikatakata, nikamwambia poa ngoja nikale vibandani, hapo ndio nilichoka akanambia uwai kurudi basi, uniletee na Pepsi, yan hasira nilizokuwa nazo anajua Mungu.

Kesho yake nikampa nauli ndio ukawa mwisho. Alilia lakn sikumwambia kosa lake mpk leo. Wanawake wanadhan huwa tunataka kuoa lexus wakati mwingine tunataka Hiace
Ndugu we ulichumbia Jini huyo demu sio bibadamu.
 
Nilikuwa na mwanaume huyo. Nilijitolea kwake zaidi ya msukule. Hakuwa na kazi ya maana alikuwa anafanya kazi Gereji Ila nilimpenda kweli.
Kwangu minguo michafu imejaa ila nikifika kwake mtoto sio kujipinda huko nafua na na kuzikagua za kupasi napasi za kwa fundi napeleka.
Napiga deki na kufuta vumbi hadi inabidi aulize kama nimepaka rangi.
Alikuwa akirudi vile anakuta panawaka waka anafurahi sana yaani.
Asubuhi anatoka kama anaenda ofisini vile.
Nilimshauri vyema hadi akanunua kiwanja na hela ni Mimi nilikuwa natunza na sikuwahi kumwibia.
Ila alifanya kosa moja linalomgharimu mpaka leo.
 
Pole,usinambie aling'ata lami
 
Ila me wanaume nawashangaaga sana,unakuta eti anamtest Mpenzi wake kama anafaa au hafai,kwani mna uhakika kama na nyie mnatufaa au tunawavumilia tu,mtupumziahe bhana nyie wenyewe vimeo,ptyuuuuuuuuu

Oa sababu unampenda MTU,anakuheshimu,yupo tayari kubadirika in case ana weakness zinazorekebishika coz tumelelewa tofauti,tumekutana na mitihani mingi hadi tumekutana,mwingine hafanyi coz alishafanyaga sana before na akaishia kutumika tu na kukwopa juu....otherwise mtakuja kuoa mactress na mapretender ndo akili ziwakae sawa na itakuwa too late,msitake tufanye majukumu ya mke wakati hamjatuoa hata kishika uchumba bado,eti mnatutest,mxieewwww,shikeni adabu zenu
 
MAMBO AMBAYO MWANAUME ANAFANYA KUKUTEST KAMA MSICHANA UNAFAA KUWA MKE WAKE

1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa.

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.

9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia.

nime copy na kupaste mahali ,kama haijawahi kufika humu uburudikieni
Inawezekana uliyotaja hapo juu akayafanya yote ila ukaoa akabadilika akawa visa vesa.au itategemea unamtest kwa mda gan mwaka au miaka
 
Kuna kidada nilikichumbia, siku moja nikamwambia njoo kwangu hata siku mbili, akaja.

Siku ya kwanza natoka kazini saa 10 nakuta anaangalia Tamthilia Star TV, namuuliza chakula tayari, ananijibu alisubiri nifike home kwanza. Dah hapo nyama mbichi hajaipika wala kuikatakata, nikamwambia poa ngoja nikale vibandani, hapo ndio nilichoka akanambia uwai kurudi basi, uniletee na Pepsi, yan hasira nilizokuwa nazo anajua Mungu.

Kesho yake nikampa nauli ndio ukawa mwisho. Alilia lakn sikumwambia kosa lake mpk leo. Wanawake wanadhan huwa tunataka kuoa lexus wakati mwingine tunataka Hiace
That's the dumbest girl ever seen in TZ universe
 
Back
Top Bottom