Mambo 5 usiyoyajua kuhusu biashara ya Kichina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo 5 usiyoyajua kuhusu biashara ya Kichina

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ugaibuni, Jan 8, 2012.

 1. u

  ugaibuni Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisikia neno China China, hili linamaanisha kila kitu, siku za hivi karibuni neno hili limehusishwa sana na ufake,kutodumu nk. Binafsi nikiwa fans wa made in China, iwe kwa kukosa njia nyingine au urahisi ninaweza kusema machache ambayo nadhani yatakuwa na msaada kwa wengine. Nikiwa Mtanzania niliyeishi China kwa miaka zaidi ya sita, ninapenda kushare nawe mambo machache ambayo wafanyabiashara hawawezi kukuambia kuhusu Made In China.
  [​IMG]
  [h=2]1. Kuna Vitu China ni Ghali kuliko hata Tanzania[/h]Unaweza kusema kivipi, ila ni kweli, ukiwa Uchina na unataka kupata kitu chenye ubora mzuri, ni dhahiri unatakiwa kulipia zaidi. Binafsi nimekuwa nikipokea simu nyingi mno toka nyumbani wakitaka kunitumia pesa niwanunulia komputa nk. Ukienda sokoni kompyuta ya kawaida ambayo ni bora inaanzia yuan 2000, tena hiyo ni ile ya kiwango cha chiiini kabisa, ila ukiipeleka kwenye dola ni kama mia tatu kadhaa, ukijumlisha na utumaji mpaka inafika nyumbani ni kama dola mia tatu na nusu au mia nne. Hapo ndio unapata kompyuta ya kawaida mno kitu ambacho kwa mtanzania wa kawaida lazima aone ghali kwani akienda sokoni anaona DELL kibao kwa laki tanotano.

  [​IMG]
  [h=2]2. China kuna bei tatu[/h] Kama umewahi kufika Uchina ni dhahiri utakubaliana nami, ukienda dukani unaulizwa unataka ipi, Hao(nzuri), Yiban(Ya kawaida) Shuihuo(Dump aka fake). Kwenye kila kundi ubora ni tofauti,ingawa kwa macho zote zinaonekana sawa. Pindi ununuapo ni lazima uhakikishe unapata kulingana na mapenzi yako. Hongera kwa wafanyabiashara WENGI wa Kichina ni kuwa, atakuambia. Hii ni nzuri na hii ni mbaya. Pia hata kwenye hiyo nzuri nayo kuna makundi yake humo ndani.hehe. Hivyo kabla hujanunua ni lazima ujue nini unataka na lazima muelewani na muuzaji.

  [h=2]3.Kitu cha 100Yuan si cha 80Yuan.[/h] Kwa wale waliowahi kukutana na Watanzania au wageni kadhaa walioishi Uchina kwa miaka mingi watakubaliana nami, jinsi muda uliokaa China unavyooongezeka ndivyo uwezo na ari ya kupatana bei inavyokwisha. Binafsi ni mara chache mno ukaniona ninapatana bei. Hii ni kwa sababu tayari wanafahamu hili. Kuna siku niliambatana na dada mmoja kununua simu, alipofika kule simu aliyopewa ilikuwa ni ya mia nane, akazidi kupatana (pianyipianyipianyi) basi mwisho yule mchina akakubali, yule dada akasema nachukua hii, mchina aliwaka kama kawekwa petroli. Akibwabwaja "haiwezekani,hii ni ghali nk) mwisho ikabidi mdadaa aongeze pesa.

  [h=2]4. Kuna maduka yanayojulikana kwa ufeki na ubora.[/h] Kila sehemu wana mila na tamaduni zao, ukiwa China, kama unataka kupata kitu chenye hadhi na ubora mzuri basi unashauriwa ukanunue kwenye maduka makubwa, kwa mfano unataka kununua TV ya nyumbani basi nenda kwenye maduka kama ya Sunning, Gomao,carrefour nk kwani mengi ya maduka haya yana mkataba wa ubora na bei na serikali. Kuna kipindi Carrefour walipandisha bei kiholela kwa baadhi ya vifaa vyao, walipigwa faini na ikawacost mno. Binafsi mwaka jana nilinunua simu ya mkononi "Nokia", wiki iliyopita kilitokea kitendo kilichonisukuma kuandika makala hii.
  Nikiwa barabarani kwenye pikipiki simu yangu ilidondoka, nikasikia mchina akiita "simu imedondoka" nikasimama na kuangalia kumbe ni simu yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa katikati ya barabara hivyo sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuiangalia ikikanyagwa na basi la abiria, baada ya lile basi kupita taa nyekundu ikawaka na nikakimbia kuangalia masalio ya simu, nikaona kioo kimevunjika, nilipoishika nikaona ukiondoa kioo hakuna kingine. Niakajaribu kupiga simu ikawa inaita bila matatizo. Kesho yake nikaipeleka kwa wenyewe Nokia, wakaiangalia wakasema ukiondoa kioo hakuna tatizo. Ni kweli nimebadirisha kioo na sasa inadunda bila wasi.

  [​IMG]
  [h=2]5. Nokia si sawa na NokIa, pia Samsung si Sunsung.[/h] NImekuwa nikisikia na kuona watu wengi wa nyumbani wakitumia simu wanazoziita Nokia ya Mchina, au Sumsung ya Mchina, hakuna kitu kama hicho huku. Wengi wanaotengeneza hizo simu ni viwanda vidogovidogo ambazo ubora wake ni hafifu mno. Wengi wamekuwa wakiongopewa kuwa inaitwa hivyo kwakuwa imetengenezwa China. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakijilimbikizia faida kwa kununua simu hizo kwa bei ya chee halafu kuwaongopea Watanzania. Chukulia mfano simu ya Nokia E72i inauzwa kuanzia 1800 hadi 2000yuan. Ila kwa zile mbofumbofu aka NoCia(NokIa) inauzwa kwa 500Yuan. Simu hizo sio tu hazina ubora bali pia ni hatari kwa afya yako kwani wakati wowote inaweza kukulipukia, inakulisha mionzi ya ajabuajabu nk.

  [h=3]Chanzo: Ughaibuni.com[/h]
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa taarifa. Ni nani anaeharibu soko la biashara la nguo na simu hapa tz esp kariakoo? Ni mchina au mtanzania mwenyewe?
   
 3. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa taarifa mkuu, uendelee kutujuza.
   
 4. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Basi kwa taarifa hii ni watanzania wanaojifanya wafanyabiashara wanokwenda huko china ndo wanaotuua kwa vitu feki.Na sijui kama serikali yetu itafanikiwa kudhibiti hili.
   
 5. DullyM

  DullyM Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Lakini hao wanaoleta vitu huku kwa bei nafuu na kuuza kwa bei mbaya si watanzania wenyewe au?? na Mkuu wewe mwenyewe unafanya nini huko? si hayo hayo ya kutuletea mafeni mabovu na mwishowe hii nchi inakuwa jalala la makorokoro ama wewe tofauti?? tujuze mkuu
  napita tuu.....
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Pamoja na bidhaa za nchi za Magharibi kuwa ghali, niko naendelea na mipango ya kuweko soko la vifaa vyao maana vina ubora, na hata vya kutoka China viuzwavyo nchi za magharibi havina kiwango cha chini kama vinavyoingizwa bongo direct kutoka China.
   
 7. u

  ugaibuni Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Dully binafsi sijuhusishi na hizi biashara. BTW ni ngumu kusema nani wa kulaumiwa, ila cha muhimu kwa wafanyabiashara wetu ni kuwa wawazi. Kwa mfano ukienda sokoni mchina anakuambia hii fake na hii nzuri kazi kwako. Bei pia ni tofaauti mno, faida yake ni kuwa hata watu wa kipato kidogo wataweza kufurahia huduma(ingawa feki) na wao wenyewe wanajua. Sasa sijui kama wafanyabiashara wetu huwa wanawaambia wateja hayo. Nimesema ni ngumu kusema nani alaumiwe kwakuwa kama ujuavyo kipato cha watu wetu, sasa kama wafanyabiashara wataleta vitu vya gharama zaidi je wangapi wataweza nunua? Sasa hili swali ni gumu mno.

  Kuhusu mlundikano wa bidhaa feki, tatizo waafrika wengi(Haswaa wale wa Guangzhou) tunapenda sana kuwin haraka bila jasho. Wafanyabiashara wengi(siwatusi) hawana elimu ya biashara so kwa wao wanaangalia CASH kwisha kazi, tena ya sasa. Hii inapelekea hata Wachina kutudharau.

  Kitu cha muhimu tukumbuke ni kuwa sio kila cha China ni fake, na sio wafanyabiashara wote wa Kitanzania ni wazushi. Kwa msaada wa Ughaibuni.com tutakuwa tunakuletea mengi. Kufuatilia mambo yanayoendelea Uchinani nenda Hapa au kama una swali la moja kwa moja unaweza Uliza kwenye kipengele cha China Hapa

  Pamojah
   
Loading...