Mambo 5 Muhimu Kujua Kuhusu Kampuni Ya Apple

Mambo 5 Muhimu Kujua Kuhusu Kampuni Ya Apple

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672

Bidhaa kutoka kampuni ya Apple si ngeni machoni mwetu aidha kwa kuzitumia,kuzishika au hata kwa kuzisikia. Apple ni kampuni ya Tarakilishi (Computer) iliyoanzishwa mwaka 1976 na watu watatu ambao ni Steve Jobs, Steve Wozniak na Ronald Wayne.


Mwaka 2016 Kampuni hii ilitimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake sasa yapo ambayo pengine huyafahamu kutoka kwenye kampuni ya Apple


1. Ronald Wayne ambae ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple aliuza hisa zake za Apple kwa dola 800 za kimarekani muda mfupi tu baada ya yeye na wenzie kuanzisha kampuni hiyo. Inasemekana kwamba alifanya hivyo baada ya kuhofia kwamba iwapo Apple wangeshindwa kibiashara basi mali zake zingebinafsishwa.


Ronald Wayne
Wasichojua wengi kuhusu Ronald Wayne ni kwamba anajihusisha na mahusiano ya jinsia moja na alimwambia habari hii Steve Jobs wakati bado wakiwa waajiriwa kabla hawajaanzisha kampuni ya Apple. Ronald anasema hajutii kuuza hisa zake wiki chache baada ya kuanzishwa.
Jamaa hakuwa mvumilivu kabisa huyu kwani hizo 10% za hisa mpaka sasa hizo hisa zingekuwa na thmani ya Bilion 60 za Kimarekani.
Anadai kwamba alifanya maamuzi hayo kwa kutegemea taarifa aliyokuwa nayo kipindi kile. Yeye ndie mbunifu wa logo ya kwanza ya Apple.



2. Steve Jobs aliuza gari lake ili aweze kutengeneza kompyuta ya kwanza ya Apple

Pesa ambazo ziligharamia utengenezwaji wa Kompyuta ya kwanza ya Apple ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la Apple Computer 1 ama Apple 1 zilitokana na pesa zilizokusanywa baada ya Steve Jobs kuuza usafiri wake wa pekee wa VW Mini Bus na Steve Wozniak kuuza calculator yake ya HP-65.


Jobs aliuza gari lake la pekee ili kulipa gharama za kutengeneza kompyuta ya kwanza. Gari hilo lilikuwa kama hili.
vw.jpg






3. Kompyuta ya kwanza ya Apple ilichukua siku kumi tu


Kompyuta ya kwanza ya Apple
Baada ya kuwa na pesa kwa ajili ya kutengeneza kompyuta iliwachukua siku kumi kukamilisha kazi. Kompyuta hiyo ikauzwa kwa dola za kimarekani 666.66 sawa na Tsh 1,466,652 za wakati huu.
Wozniak anasema hakuwa anajua chochote kuhusu mambo ya kishetani kuhusishwa na namba hiyo kwa wakati kwa wakati huo hivyo hiyo namba haina uhusiano wowote na imani za kishetani.

4. Steve Jobs aliwahi kushushwa Cheo akaamua kwenda kuanzisha kampuni nyingine.

Tarehe 16 Septemba 1985 Steve Jobs alishushwa cheo cha umeneja na bodi ya wakurugenzi baada ya kutokea kugombea madaraka kati yake na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa wakati huo.Jambo hili la kushushwa cheo lilimkera sana Steve Jobs.Baada ya ushindani wa kiutawala uliotokea baina ya Steve Jobs na John Sculley mmoja wa watu ambao Steve Jobs aliwaleta toka kwenye kampuni ya Pepsi-Cola.
Jamaa huyo alifanya kazi na Steve kama viongozi na baadae wawili hao walitofautiana na kamati kuu iliamua kuingilia kati na kumchagua bwana John Sculley kama mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo.
Jambo hili lilimuudhi Steve Jobs na akaamua kaondoka na baadhi ya wafanyakazi wakaanzisha kampuni ya NEXT.



5. Apple walishawahi kuwa na pesa nyingi kushinda serikali ya Marekani

Kwa kipindi cha mwaka 2011 Apple walikuwa wanahifadhi pesa kubwa kushinda hifadhi ya pesa za serikali ya Marekani, hii ilitokana na hasa na ukubwa wa madeni ya Marekani kwa wakati huo.


5.Vipeperushi vingi vya Apple vinaonyesha Saa 9:41
Unajua kwanini?
Hivi ushawahi kujiuliza kwanini vipeperushi vinavyotengenezwa na kampuni ya Apple 9:41?.Kama ulikuwa haujui basi hiii ndiyo sababu,mwaka 2007 tarehe 9 Januari saa 9:41 asubuhi Steve Jobs alitangaza Iphone kwa mara ya kwanza kabisa.
Now You Know...!

6.Apple Ilishawahi Kutengeneza Video Game
Kama wewe ni mpenzi wa video game umeshawahi kujiuliza kwanini kampuni kubwa kama Apple haina video game kama ilivyo kwa PS4 kwa Sony au XBOX kwa Microsoft?
Lakini kama ulikuwa haujui hapo zamani za kale mwaka 1995 kampuni hii ya Apple ilishawahi kutengeneza video Game iliyiotwa Apple Pippin,kifaa hicho hakikufanya vyema kilikufa mapema baada ya kuzinduliwa kwake.Mbaya zaidi Apple kupitia kifaa hicho kiliuzwa nakala 42,000 tu duniani kote na kilikuwa na magemu 18 tu.
Hapa Apple kweli walichemka.

7.Maneno Yote Unayosema Na Programu Ya Siri Yanahifadhiwa na Apple.

Kama wewe ni mtumiaji wa bidhaa ya kampuni ya Apple hapa namaanisha wale wanaotumia Iphone basi bila shaka utakuwa unaijua programu ya SIRI,programu hii inakusaiidia kufanya mambo yako ya siri kwenye simu yako ya Iphone kwa kutumia maneno.
Cha muhimu ni kujua kuwa kila neno unaloongea na programu hiyo jua kuna mtu kazi yake ni kusikiliza na kuhifadhi kwa muda wa miaka miwili.
Sehemu hii imeandikwa kwenye sehemu ya VIGEZO NA MASHARTI unapoanza kutumia programu hii ya siri kwa mara ya kwanza.



BONUS
Nakuongezea na hili. Ukiangalia kwa makini kwenye logo ya Apple kuna sura ya Steve Jobs.

SABABU YA STEVE JOBS KURUDI KUFANYA KAZI APPLE
Kampuni ya Apple ilifanikiwa kuinunua kampuni ya Steve Jobs ya NEXT na kuifanya iwe mali yao hii ilipelekea Steve Jobs lkurudisha tena kufanya kazi pale Apple na kupewa cheo cha Mkurugenzi Mkuu
 
Hata mimi nilitaka kuuliza hivyohivyo why pamepooza?
nadhani fanani wamechoka " hawapewi support Gus kutosha toka kwa hadhira "... hadhira tuko busy na habari za umbea na matusi tu .. ila mada fikirishi tunazikimbia"... .unategemea nini toka kwa watu wanaotawaliwa na CCM mkuu .. !!?
 
nadhani fanani wamechoka " hawapewi support Gus kutosha toka kwa hadhira "... hadhira tuko busy na habari za umbea na matusi tu .. ila mada fikirishi tunazikimbia"... .unategemea nini toka kwa watu wanaotawaliwa na CCM mkuu .. !!?
Watu wanawaza kuosha na kuoshwa na mashine zilizokula Vumbi La Kongo
 
Tecno yako na Jobs wapi na wapo? Wanaotumia Iphone hata miandiko inaeleweka.

Ni kwanini popote inapojadiliwa iphone, tecno lazima itajwe???

Tecno ni taifa kubwa eti eh[emoji1322]‍♂️[emoji1322]‍♂️[emoji1322]‍♂️
 
Back
Top Bottom