Travis Walker
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 323
- 335
Habari Wana wa JF.Natumai muko sawa,
Leo nashukuru Mungu kuchukua fursa hii kwa mara nyengine tena kuwaelezea kile ninachokifahamu katika maisha.Nimekuja na mambo manne ukiwa nayo mwanamke atakupenda na utamfanya mkeo awe na furaha.
1.KUWA NA HESHIMA.
Heshima inasababisha mwanamke kukupenda kwasababu utapokuwa na heshima una-epukana na dhararu na wanawake karibuni wote hawapendi kudharauliwa.Heshima ni miongoni mwa kumsikiliza mtu,kutoongea nae kwa maneno machafu,kutompiga pasi na sababu,kutofanya vitu ambavyo yeye havipendi,kuonesha unajali kwake n.k.
2.KUDHIHIRISHA UPENDO
Unapoishi onesha kwamba una upendo na kila mtu,kwasababu mwanamke anahitaji amani na maelewano.Unapokuwa na sura pamoja na moyo wa upendo kila mtu anavutika nawe na anakupenda sio mwanamke tu peke yake, na wala watu hawatokuchoka.
3.KUWA MWEREVU
Hutakiwi kuwa mjinga mbele ya jamii.Unatakiwa kuishi ki-professional.Kwa sababu mwanamke anajivunia sana anapokuwa na mwanamume mwenye busara,anahisi ni wato-fauti.Jaribu kuwa mkimya usiwe unaongea ovyo,kuwa mtaratibu na usiwe unakimbilia kutoa hukumu kabla ya kufikiri.
Fikiria kwanza,Ongea maneno madhubuti. Mimi binafsi, kwenye miaka kama 5 iliyopita kuna mtu alikuwa anapenda sana kuniambia maneno haya "I like the way you are".
4.KUWA NA UVUMILIVU
Wanawake ni watu wenye vituko sana.Na muda mwengine huwa ni kama tabia kwao wanapokuwa wanaumwa ama wana stress zao tu ki-kawaida.Sasa unatakiwa ufahamu kwamba wewe ni mwanamume unatakiwa kuvumilia na hivyo vituko na maudhi yote hayo.Unatakiwa kuwa mkimya na uweze kudhibiti hasira zako.Mwachie mtu mpaka ajitambue mwenyewe kama ana makosa.
Kujifunza tabia hizi utakuwa umeuteka moyo wa mwanamke