Mambo 20 muhimu anayoyaamini Donald Trump

Mambo 20 muhimu anayoyaamini Donald Trump

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2013
Posts
1,300
Reaction score
743
Donald Trump anaongoza katika kinyang?anyiro cha kumtafuta mgombea urais atakayewakilisha chama cha Republican katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Wajua sera zake na mambo anayoyaamini?

1. Waarabu-Wamarekani jimbo la New Jersey walishangilia shambulio la Septemba 11, 2001 liliotekelezwa. Hakuna habari za kuthibitisha haya.

2. Kunafaa kuwa na mfumo wa kufuatilia misikiti Marekani kama njia ya kukabiliana na ugaidi.

3. Marekani inafaa kutumia njia kali za kuhoji washukiwa katika vita dhidi ya Islamic State.

4. Trump amesema akiwa rais anaweza kuwaangamiza Islamic Static kwa mabomu na pia kuwazuia kupata mafuta.

5. Kuundwe mfumo rahisi wa ulipaji ushuru, watu wanaolipwa chini ya $25,000 (?16,524) wasiwe wakilipa ushuru wa mapato.

6. Watu wenye hazina za uwekezaji ng?ambo hawalipi ushuru wa kutosha. Lakini baadaye alibadilika na kusema watapunguziwa ushuru sawa na watu wa pato la wastani.

7. Anataka kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji kutoka Mexico.

8. Anawafurusha wahamiaji wote 11 milioni ambao waliingia Marekani kwa njia haramu.

9. Yeye na Vladmir Putin wanaweza ?kusikizana vyema?.

10. Ili kuzuia visa vya watu kupigwa risasi Marekani, nchi hiyo inafaa kuwekeza katika afya ya akili.

11. Uchina inafaa kuchukuliwa hatua kali katika masuala kadha ili kuhakikisha usawa wa kibiashara kati yake na Marekani.

[http://ichef]Image copyrightAFPImage captionTrump amekuwa akisema haja yake kuu ni kurejesha hadhi ya Marekani

12. Kundi la The Black Lives Matter ambalo hutetea haki za watu Weusi Marekani ni hatari.

13. Takwimu za sasa za Marekani ni za kupotosha. Anasema ukosefu wa ajira umefikia 20% kinyume na takwimu rasmi zinazoonyesha ni 5.1%.

14. Utajiri wake ni $10bn.

15. Mfumo wa kutoa huduma za afya kwa wanajeshi wa zamani unafaa kufanyiwa mabadiliko makubwa.

16. Mpango wa Obamacare ambao ulilenga kuongeza idadi ya Wamarekani wanaopata bima ya afya ni ?mkasa?.

17. Mabadiliko ya tabia nchi ni hali ya kawaida tu ya hewa.

18. Ulimwengu ungekuwa pahala pema pa kuishi kama Saddam Hussein na Muammar Gaddhafi wangekuwa bado madalakani.

19. Angewarejesha makwao wahamiaji kutoka Syria wanaotafuta hifadhi Marekani.

harusi ya wapenzi wa jinsia moja, hakufaa kazi hiyo.

20. Yeye ni ?mtu mzuri sana? na anataka sana kurejesha hadhi ya Marekani

1cf277e8e90cc0bb2b21ef12349818df.jpg
 
Mbona hujaweka ile aliyosema kuwa
Waafrika tunawaza kula na kukamua nyapu tu muda wote.
 
Sasa iyo namba 14 anaiaminije?
By the way mie namsapoti Dr Benjamin Carson
 
Binafsi jamaa huyu namkubali sana,pamoja na matani yake mengi lakini ni mtu mwenye akili sana na mpenda AMANI,hana inferiority complex ambazo zinamsumbua Obama anaye endeshwa na ma neocon na kuhatarisha amani Duniani,Obama ametekwa nyara na kundi hilo hatari - Dunia hisipo kuwa makini na mahamuzi ya kijinga ya Rais Obama anaweza kabisa kuitumbukiza Dunia kwenye vita ya tatu ya Dunia kutokana na ushindani wake wa kishenzi baina ya Merikani na Uchina na Urusi - nchi hizo zimekwisha jipanga kuipa fundisho Merikani ikithubutu kuzishambulia kwa kisingizio chochote kile,Obama ni kiongozi ambae amezidisha chokochoko Africa ya kaskazini, Mashariki ya kati na Ulaya ya mashariki bila ya kusahau Afghanistan -kwote huko ni vurugu tupu na hawajawahi kuleta amani ya kudumu katika sehemu hizo tajwa!

Trump ndiye atakuwa suluhisho la amani Duniani kutokana na Utajiri wake mkubwa hawezi kuwekwa mfukoni na ma neocon au wafanya biashara wenye viwanda vya kuhunda silaha hao ndio wenye ushawishi mkubwa kwa Viongozi wa Jeshi la Merikani kuanzisha vita kila pembe ya Dunia ili wauze silaha zao.
 
Hiyo namba 7 siyo sahihi! Tayari kuna ukuta tena wa chuma ktk mpaka wa US na mexico.
 
Donald trump hana tofauti na Eddy murphy wote ni standing comedians tu

ukitaka kuthibitisha hilo angalia point 11&12
 
Trump hajawahi kuwatukana Waafrika ni uzushi wa mtandaoni tu.
 
Trump hajawahi kuwatukana Waafrika ni uzushi wa mtandaoni tu.

Kuna watu wapumbavu sana.

Wao kila wasomao mtandaoni, ili mradi liwe limeandikwa tu, basi wanaamini mazima.

Ukiwauliza Trump aliwahi kusema hivyo lini na wapi, hupati jibu!
 
Back
Top Bottom