Mambo 12 muhimu kuhusu Abraham Lincoln

Mambo 12 muhimu kuhusu Abraham Lincoln

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,291
Haya ni baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani, ambaye ameacha alama kubwa kwa nchi hiyo na dunia kwa ujumla.
1.Abraham Lincoln wakati wa utawala wake alipinga biashara ya watumwa nchini Marekani.
2.Wakati wa utawala wake, Abraham Lincoln alikuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kuthamini haki za wanawake, na kuamini kuwa wanawake pia wana haki ya kupiga kura, ingawa mpaka anauawa aliacha bado wanawake hawaruhusiwi kupiga kura.
3. Abraham Lincoln alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani kutokea katika chama cha Republican, chama ambacho anatokea Rais wa sasa Donald Trump.
4. Abraham Lincoln hakuwa na elimu maalum, alikuwa akijisomesha mwenyewe nyumbani lakini alikuwa na uwezo mkubwa kwenye kujifunza (Kwa ufupi hakuwa na taaluma yoyote)
5. Lincoln aliuawa na muigizaji John Wilkes Booth ambaye pia alikuwa shabiki yake mkubwa, siku ya Ijumaa Kuu mwaka 1865 , alipoenda kuangalia onyesho lao kwenye theatre.
6. Mtoto wa Abraham Lincoln, Robert Lincoln aliokolewa kwenye ajali ya treni na Edwin Booth, ambaye ni kaka wa muuaji wa baba yake.
7. Mama yake Abraham Lincoln alifariki baada ya kunywa sumu aliyowekewa kwenye maziwa, wakati Abraham Lincoln akiwa na miaka 9.
8. Abraham Lincoln alikuwa na tatizo la msongo wa mawzo, hivyo alikuwa habebi vitu vya ncha kali, akihofia kujidhuru.
9. Abraham Lincoln hakuamini kuwa watu weusi wana haki sawa na watu weupe (Alikuwa mbaguzi)
10. Lincoln alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani ambaye sura yake iliwekwa kwenye sarafu (Ilikuwa kwenye sarafu ya senti 1)
11. Abraham Lincoln aliweka nyaraka zake muhimu chini ya kofia yake aliyokuwa akiipenda zaidi.
12. Kizazi cha Abraham Lincoln kimepotea kabisa, kwani watoto wake wake wote walishafariki, mtu wa mwisho wa kizazi chake alifariki mwaka 1985.
Chanzo: Eatv
 
Sawa na mimi nitakuja na sifa zangu japokuwa nyingi nimezipata Tandale
 
Alikuwa mbaguzi (9) aende zake kuleeeeee.
 
Baada ya kufariki roho yake ikaingizwa kwa John F Kennedy.

Hii ni kwa wale tunaoamini ukifa roho yako inapandikizwa anazaliwa mtu mwingine.
 
13 :Ni Rais aliyeelezea Democrasia kuwa " is the government of the people for the people by the people"
 
Nikiiangalia historia hii ninaona kuna laana iliyokuwa inawafatilia ndiyo maana waliandamwa na roho ya mauti
 
Mkuu radika...nina swali....
Lincon Ana fanana flani na Kennedy ...na mpaka majina ya masecretari wao yalifanana.inakuwaje?
 
Back
Top Bottom