Mambo 10 ya kustaajabisha kwenye uchaguzi huu

Mambo 10 ya kustaajabisha kwenye uchaguzi huu

18. Msaga sumu kutamba na kujulikana nchi zima baada ya kushusha song la kumsifu mzee laigwanani. Hapo awali alikuwa akijulikana pwani na uswahili kama manzese,kisarawe,buguruni etc

haha mzee wa vigodoro
 
Wewe kweli screpa unashangaa vitu vidogo kama hivyo badala ya kushangaa wizi wa kura watu kukamatwa na maboksi takwimu za kura kutofautiana za majimboni na zinazoletwa NEC, na mabomu yanayolindima kila kona baada ya wagombea wa UKAWA kushinda.

Unashangaa kurindima Kwa mabomu wakati wa uchaguzi?Mbona kawaida, na wapinzani kulalamika wameibiwa haijaanza leo
 
Kasoro Kuu Uchaguzi huu Wino vidoleni haufutiki....
 
Prophet TB Joshua kuja baada ya uchaguzi. Wakati akitia timu kwenye nchi basi ujue kuna.prayer crusade.
 
Uchaguzi huu umekumbwa na matukio mengi ya kustaajabisha kiasi kwamba yanaweza kukuacha mdomo wazi, haya ni baadhi ya mambo ambayo binafsi yamenishangaza sana;

1. Mama Anna Tibaijuka kuchaguliwa tena ubunge na wana Muleba

2. Wenje na Kafulila kukosa ubunge

3. Tume ya Zanzibar kulalamika uchaguzi haukua huru na wa haki (badala ya wagombea)

4. January Makamba kushangazwa na kinachoendelea Zanzibar

5. 'MAKAMANDA' wa CHADEMA kumkaribisha Lowasa kwenye chama chao na kumnadi kama mgombea wao wa urais (mtu waliyetuaminisha kwamba ni Fisadi Kwa miaka 8)

6. Wakazi wa Mwanza kudeki lami ili Lowassa apite ila cha ajabu kwenye sanduku la kura wamemuangusha na kumpa kura nyingi Magufuli

7. CHADEMA kumuona Lowasa kama mkombozi wao na Dr. Slaa kuitwa msaliti

8. Mgombea Maalim Seif kujitangazia matokeo kana kwamba yeye ni tume

9. Mbatia kutumia mda mwingi kuisemea UKAWA na CHADEMA kuliko chama chake

10. CCM 'chama dola' kulalamika kwamba kuna majimbo manne wameonewa
Nape kupata ubunge ni la ngapi?
 
Ujio wa prophet tb joshua. Na huku ikisemekana kuwa hakuhudhuria kuapishwa kwa rais.
 
15.Police kuingia hasara baada kujiandaa sana na kununua vifaa vingi sana then uchaguzi umekuwa wa amani na utulivu kuliko ata 2010.
 
sitasahau saut ya lubuva anasema hv ikumbuke saut yake,
"Ana Elisha Mgwira ACT 253 Sawa Na 0.6%
Chief Lutalosa Yemba ADC Kura 125 Sawa Na 0.3%
Dr John Pombe Magufuli Kura 32,510 Sawa Na 78%
Edward Ngoyai Lowassa CHADEMA kura 8,100 sawa na 16%"
 
11. Mawakala wa vyama vya siasa kama wawakilishi kuchelewa kufika na kwenda lunch na usiku kuondoka kwenda kulala na kuacha shughuli yao kwa wasimamizi wa tume

12. Majimbo ya mjini kwenye miundombinu yote kuchukua mpaka siku 3 kutangaza washindi na figisufigisu za kutaka kurudia kuhesabu ilhali usalama wa maboksi ya kura unatia shaka

13. Watangazaji matokeo kuchukua muda mrefu kutangaza wakijiua hiyo inazua sintofahamu kwa wapiga kura wanazi
14. Kuwatangazia wananchi matokeo ya uchaguzi halafu kuwapiga mabomu ya machozi wasishangilie ushindi.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Back
Top Bottom