MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA MPYA WA BARCELONA

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
HATIMAYE Barcelona wamemaliza kazi ya kumsaka atakayechukua nafasi ya kocha wao, Luis Enrique ambaye ameondoka kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Enrique ameiacha nafasi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na mchezo wake wa mwisho ulikuwa ni ule aliowachapa Alaves na kuchukua ubingwa wa Copa del Rey.

Kibarua chake kimetua mikononi mwa Mhispania mwenzake, Ernesto Valverde ambaye alikuwa akiinoa Athletic Club aliyodumu nayo kwa kipindi cha miaka minne. Hata hivyo, huenda kuna mengi hukuyajua kutoka kwa mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 53.

1. Valverde amesaini mkataba wa miaka mitatu na ataanza kazi katika benchi la ufundi la Barca wakati timu hiyo itakapokwenda Marekani kujiandaa na msimu mpya wa 2017-18. Ikiwa nchini humo, Barca itacheza mechi za kujipima ubavu na Real Madrid, Manchester United na Juventus.


2. Kocha huyo amehamia Barca akiwa na wasaidizi wake wawili ambao alikuwa nao Athletic. Kwanza, amehama Jon Aspiazu ambaye amefanya naye kazi kwa takribani miaka 15 na pia yupo na kocha wa viungo, Jose Antonio Pozanco.


3. Kabla ya kugeukia kazi ya ukocha, Valverde aliwahi kuichezea Barca kuanzia mwaka 1988 hadi 1990, kipindi hicho timu hiyo ilikuwa ikinolewa na Johan Cruyff. Hivyo, Valverde anakuwa ni mwendelezo wa utamaduni wa Barca kuajiri wachezaji wao wa zamani.


4. Huenda wengi wanaamini Valverde hana uzoefu lakini si kweli kwani alianza kufundisha soka tangu mwaka 2001 alipojiunga na Athletic Bilbao. Mbali na Athletic, amezinoa Espanyol, Villarreal na Valencia kwa kipindi kisichopungua miaka 10.


5. Valverde ndiye kocha wa kwanza kuipa Athletic taji baada ya timu hiyo kusubiri kwa kipindi cha miaka 31. Athletic ilitwaa taji la Spanish Supercopa mwaka 2015 baada ya kuwachapa Barca katika mchezo wa fainali.


6. Kocha huyo ambaye aliwahi kufanya kazi Ugiriki alikokuwa akiinoa Olympiacos, ni mume wa mwanamama Juncal Diez na ndoa ya wawili hao inatajwa kuwa na takribani miaka 20 sasa, huku wakiwa wamebahatika kupata watoto watatu.


7. Nje ya soka, Valverde ni mtaalamu wa upigaji picha. Aliipata taaluma hiyo katika chuo cha Institut d’Estudis Fotografics de Catalunya kilichopo Hispania.


8. Wakati akiwa na mastaa Gary Lineker, Ronald Koeman na Michael Laudrup kwenye kikosi cha Barca, kocha wa sasa wa Manchester City, Pep Guardiola, alikuwa kwenye ‘academy’ ya timu hiyo.


9. Sifa kubwa ya kocha huyo ni kuunda safu ngumu ya ulinzi. Alipokuwa Ugiriki mwaka 2009, Olympiacos yake ilishinda taji la ligi kuu ikiwa imefungwa mabao 14 pekee. Tangu aliporejea Athletic mwaka 2013, timu hiyo haijafungwa zaidi ya mabao 45 katika msimu mmoja.


10. Kabla ya Valverde kupewa mikoba, kibarua cha kuinoa Barca kilikuwa kikiwahusisha makocha Jorge Sampaoli, Ronald Koeman, Mauricio Pochettino na Laurent Blanc. Sampaoli alipewa nafasi kubwa kwani ndiye kocha aliyekuwa akiungwa mkono na staa Lionel Messi.


*Ramadhan Kareem*
 
Makocha waliokuwa wanapewa nafasi tangu mwanzo walikuwa 2 tu sababu kocha waliokuwa wanamtaka Barca awe na sifa ya kuwa na identity ya Barca

Eusebio sacristan na Valverde lakini Eusebio aliwatolea nje Barca sababu ya kitendo cha unprofessional alichowahi kufanyiwa na board ya Barca

Valverde anasifika kwa high pressing na Athletic ilikuwa Mara nyingi inafanya pressing high up the pitch huku mfumo anaoupenda ni 4-2-3-1 na mara chache alikuwa anatumia 4-3-3

Valverde amepandisha vijana wengi na kuwatumia kikosi cha kwanza Athletic Bilbao kama inaki Williams ,Boveda ,lekue ,arrizabagala ,merino ,San José nk
 
Back
Top Bottom