Tanzania ina eneo linalofaa kwa kilimo Hekta milioni 44 na linalofaa kwa umwagiliaji Hekta milioni 29, mpaka sasa zaidi ya 60% ya watanzania wameajiriwa katika kilimo. Biashara ya kilimo katika soko la Afrika inatarajiwa kuwa na Dola Trilioni 1 hadi kufika mwaka 2030. Mapinduzi yanayofanywa na Rais Samia katika sekta hii;
1.Serikali imefanikiwa kufungua masoko mapya ya mazao nje ya nchi hususan zao la parachichi katika nchi za India na Afrika Kusini baada ya kukidhi viwango vya ubora.
2.Serikali imefanikiwa kupata maghala ya kukodi nje ya nchi kwa ajili ya kuhifadhi nafaka yenye uwezo wa kubeba tani 5,000 nchini Sudan Kusini, tani 2,000 nchini Congo na jitihada hizi zinaendelea ili kufungua maghala mengine China, Vietnam na UAE.
3.Serikali imeweza kuongeza bajeti ya utafiti kutoka shilingi bilioni 7.35 hadi bilioni 11. Pia, serikali imeona umuhimu wa kugawa vipima udongo kwenye Halmashauri 143, simu janja pamoja na visanduku vya kutolea huduma 3,300.
4.Serikali imeweka nia ya kuwezesha upatikanaji wa Ithibati ya Ubora kwa ajili ya maabara yenye viwango vya ubora vya kimataifa kwa ajili ya Mamlaka ya mimea na viuatilifu, hatua hii itasaidia kuhakiki ubora wa mazao ya Tanzania.
5. Mwaka 2020, serikali ilifanya majaribio ya kutoa ruzuku za pembejeo kwa wakulima ambapo jaribiohilo limetoa matokeo mazuri hivyo Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia imeamua kuwepo na Mfuko Maalum wa Pembejeo ili kuwasaidia wakulima.
6. Serikali imeweza kuongeza bajeti ya huduma za Ugani kutoka TZS bilioni 17.7 hadi TZS bilioni 51.45, kuongeza fedha za uzalishaji wa mbegu kutoka TZS bilioni 5.42 hadi TZS bilioni 10.58, sambamba na kuongeza bajeti hiyo, tumewezesha NFRA na Bodi ya Mazao Mchanganyiko kwa jumla ya TZS bilioni 129 ili waweze kufanya kazi zao vizuri.
7. Serikali kupitia Benki ya kilimo Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) imeweza kuwa mdau mkubwa kuwezesha mabenki kutoa mikopo kwa wakulima, Hadi sasa benki zinazotoa mikopo kwa wakulima zimefikia 14. 8. Serikali imeelekeza kuanza kujengwa maghala maeneo ya vijijiji walipo wakulima ili wanapovuna waweze kuweka mazao yao ndani ya maghala ili kuondoa tatizo la upotevu wa mazao na ili mnunuaji anapokuja ayakute katika hali nzuri.
9. Serikali pia inalenga kuongeza thamani ya mazao yanayouzwa nje kutoka Dola za Marekani bilioni 1.2 hadi Dola za Marekani bilioni 5. Aidha, serikali ililenga kuongeza idadi ya mashamba makubwa kutoka 110 hadi 1,000.
10. Serikali imeendelea kuimarisha huduma za Ugani, ambapo kwa siku ya tarehe 4 April 2022 ziligawiwa pikipiki 6,700 ambapo pikipiki 300 zilishatangulia na kufanya jumla ya pikipiki kufikia 7,000 kwa Maafisa Ugani wote.
KILIMO NI AJIRA PIA KILIMO NI BIASHARA NA SIO UMASIKINI