Feld Marshal Tantawi
JF-Expert Member
- Dec 24, 2014
- 609
- 1,007
Mambo 10 kuhusu hotuba ya Rais Samia leo;
1. Ametumia muda mwingi kuzungumzia Chadema kuliko kilichompeleka kwenye mkutano. As the result Chadema imekua agenda kubwa kuliko mkutano wenyewe. Hapa Chadema 3, Msajili 0.
2. Hana taarifa sahihi jinsi jamii inavyomchukulia. Namshauri aache kukumbatia "chawa" atumie vyombo vyake kujua hali halisi ilivyo mtaani. Ni tofauti kabisa na anavyojiaminisha. Watu wamemkinai mno. Kama "watu wake" wanampenda watamwambia ukweli ili wamsaidie kubadilika.
3. Anadai kuunda kikosi maalumu cha kufuatilia maoni mtandaoni na kuyafanyia kazi. Awamu ya 5 kilikuwepo kikosi kama hicho na tulishuhudia wakosoaji wakipotea, kukamatwa na wengine kuumizwa. Je anataka kuturudisha zama hizo za giza?
4. Anadai anapenda kukosolewa, lakini ukimsikiliza dhamiri inakataa. Angekua anapenda kukosolewa leo TEC wangealikwa. Lakini kwa sababu ya kukosoa mkataba wa bandari TEC wamepuuzwa. Unawezaje kupuuza Kanisa takatifu Katoliki la Mitume, lenye nusu ya Wakristo wote nchini?
5. Chawa wamemwaminisha kwamba wanaomkosoa wanamtukana. Hawawezi kutofautisha ukosoaji na matusi. Kupinga mkataba wa bandari sio matusi. Kutetea Wamasai wa Ngorongoro sio matusi. Kudai Katiba mpya sio matusi. Wapuuze wanaokuaminisha hivyo
6. Anasema uhuru wa maoni una mipaka, lakini anaamini yeye ndio mwenye kipimo cha kuweka hiyo mipaka. Kwahiyo wanaotoa maoni yasiyomfurahisha anadhani wanatumia uhuru wao vibaya 🤣. Funny but not funny.!
7. Waliomwambia JPM kuwa Katiba haileti maendeleo, huenda ni haohao wanaomwambia Samia kuwa Katiba inaweza kuwepo na isifuatwe. Ni aibu kiongozi aliyeapa kwa Katiba kutamka maneno haya hadharani. Kimsingi alitakiwa kuitetea sana Katiba maana hata Urais wake umetokana
8. Watanzania wanataka Katiba mpya sio elimu ya Katiba. Katiba ni vile jamii inavyotaka kujiongoza yenyewe. Watanzania wanajua wanataka waongozwe vipi. Walishatoa maoni yao kupitia Tume ya Warioba. Hawahitaji kufundishwa tena kuhusu hilo.
9. Mabalozi walioalikwa leo kuna jinsi wamebadili mtizamo wao kwa Rais Samia. Wengi wamekua "disappointed" na hotuba yake. Huenda hii ikawa hotuba mbovu zaidi tangu aingie madarakani.!.
10. Polisi wataitumia hotuba hii kama kigezo cha kuzuia mikutano ya kisiasa. So tusubirie zile ramli za MaRPC kwamba "Taarifa za kiitelijensia zinaonesha uvunjifu wa amani, hivyo mkutano wenu umezuiwa".
Kwa kifupi SSH ameturudisha zama za "jiwe" kwa muda mfupi sana. Hakuwa na pumzi ndefu kama tulivyodhani. Mwaka mmoja tu wa mikutano ya kisiasa tayari amechoka na anatamani kuifuta. Tuna safari ndefu kufikia demokrasia ya kweli.!.