MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,605


Huwezi kutaja majina ya watu kumi hata watan0 waliofanya mapinduzi ya kiteknolojia Duniani bila kumtaja STEVE JOB. Kuna somo la maisha katika maisha ya kila Mwanadamu mwenzako.
1:Huyu jamaa alikuwa ni MWARABU. Baba yake mzazi ni Abdulfattah Jandari Kutoka SYRIA.
Alikuwa adopted (fanywa kuwa mtoto kihalali kwa wazazi wasio wako) kwa familia ya wazungu kwa masharti lazima wamsomeshe japo alikimbia shule.
SOMO: MAendeleo ya mtu mmoja mmoja hayajalishi kama wewe ni yatima, mlemavu au umeumbwa kwa rangi gani (mzungu,mwarabu,mchina au mtu mweusi).
2:Baba yake aliyemchukua alikuwa ni fundi na designer wa vitu. Chochote kile ambacho kilihitajika nyumbani walikitengeneza . Walipohitaji Kabati walitengeneza. walipo jenga fensi alipewa nyundo kusaidia. Akiwa na Miaka kumi alikuwa tayari na hamasa ya KIELECTRONIKI na alikusanya majirani watoto wenye nia hiyo wakawa wanajaribu vitu mablimbali.

SOMO: Baba watoto wasikuone kama kituo cha polisi. Unanafasi kubwa kwa future ya mtoto wako hata akiwa angali mdogo. Mshirikishe katika vitu vingi utajua anakipaji gani. Kama ilivyokuwa kwa WAZAZI wa Bill Gate waliweka zawadi au adhabu kdg kwa kila kitu. kila kitu nyumbani ilikuwa ni shindano linalohitaji high performance.
3:Steve hakuwahi kuandika CODE hata moja. Kazi kubwa ilifanyika na rafiki yake STEVE WOZNIAK.

SOMO: Hii dunia sio lazima ujue kila kitu, unaweza kutumia wanaojua ukafanikiwa pia. Kwa sababu wapo watu wanamawazo makubwa waoga,masikini,wanadharau walichonacho etc. ukiungana nao mnaweza fanya kitu kikubwa maishani.
4

SOMO: Sio kila mtoto mvivu au mzito kuelewa hana akili. Kama mzazi unaweza kugundua vipaji lukuki ndani ya Mwanao. Usimkatishe tamaa.
5:Hadi anakufa 2011, alikuwa anahati miliki (PATENT) 141 za vitu alivyovivumbua.

SOMO:Kifo kiwe ndio mpaka wa kile unachotaka kufanya. hakuna kitu kama nimetosheka au nimelidhika wakati bado uko hai.
6:Sekretari wake alichelewa kazini siku moja, alipomuuliza kwa nini kachelewa akasema gari yake iligoma kuwaka. Badala ya adhabu yeye alimzawadia kali la mamillioni aina ya JAGUAR Ili asipate visingizio.

SOMO:KUwa na mahusiano mazuri na unaofanya nao kazi. Wakti mwingine fanya kitu kizuri ambacho hakuna mtu atakibashiri au kukitarajia kutoka kwako.
7:Ni Miongoni mwa watu wachache duniani ambao wameshiriki kuibadili dunia lakini hawakuwa elimu ya kiwango cha DIGRII hata moja. Wengine ni Henry ford,Abraham Linkoln, Mark Zuckerberg, Bill Gate,Thomas Edison etc.

Somo: Kutokuwa na elimu ya chuo kikuu kusikufanye ukajiona haufai au sio mtu wa heshima na msomi. Kinachokutofautisha na binadamu wengine duniani sio Elimu bali ni Thamani Unayoiongeza katika jamii kwa vipaji na uwezo wako.
8:Steve job alizikwa katika kaburi lisilo na alama yoyote wala jiwe, wala kaburi la kujengewa ni nyasi tu.

SOMO: Ukifa, unachokiacha katka maisha wa watu kina thamani zaidi hata ya mahala unapozikwa.leo bidhaa za huyu mtu zimetapakaa dunia nzima, usipomtaja yeye utataja Mac,Apple, ipad, ipod, softwares,iphone etc. Wekeza katika maisha ya watu.Pamoja na kuzikwa bila kaburi la manjonjo (kama mzoga tu bila jiwe la ukumbusho), lakini watu mashuhuri waliokuwepo na kutoa hotuba makaburini walikuwa ni Barack Obama na Bill Gate na wengine kibao.
9

Somo:Watoto wetu sio wa kuachwa wajitawale katika matumizi ya vifaa vya kimitandao hasa katika umri ambao hawajajitambua. kama wanaruhusiwa basi ni kwa utaratibu na uangalizi maalumu na ni kwa matumizi yenye tija.
SEMA CHOCHOTE KUHUSU MTU HUYU