Akiugua kadi ya bima inampeleka hospitali, risiti ya shule inampandisha daladala au gari la shule, akiwa na njaa anajilisha mwenyewe, nguo zikichafuka zinajifua zenyewe, ankiwa na njaa mchele, unga, mayai, n.k. ulivyopeleka vinajipika vyenyewe. Kwani Kutompa pesa ndio mnaona manafaidi sana? Mtoto akikuwa atasimuliwa na mama yake. ATAWACHUKIA TU.
dah resonable unayoitaka ww umeshajibiwa na lizzy.kama unataka mtoto alelewe kwa matabara ya kufua na kuanika ,kwa unga wa dona kama toto yenu sio gojwa gojwa hapo naweza kusema kwamba walau chenchi itabaki kidogo.
Nina kaka angu ameachana na mke wake anatoa hiyo laki saba kila mwenzi na bado mtoto akiumwa gharama juu yake na kumchukua mtoto haiwezekani causemtoto bado mdogo upo hapo kijana.
Kaunga umenitia kitanzini......nikijibu haya maswali niakuwa nimejimaliza........................kwa kifupi tu bila ya kumwaga mtama kwenye kuku wengi................maana hata yeye ni mwana JF...............kwa hiyo asije akajua udhaifu wangu a akautumia dhidi yangu ni kuwa...................I have a name to protect..........sleaze publicity will hurt my name........
Huyo mtoto wa maige....baba anajikamua kutoka laki saba na wewe unatumia kama zilivyo jamani na bado unataka zaidi....mwalimu anaishi na mtoto,mume na mdogo wake kwa laki na nusu na mtoto ana survive fresh....uko ni kukomoana...kwanza ni bahati kapata baba responsible hata baada ya ndoa kuisha mahakamani na kugawana vitu..
Ilitakiwa baada ya kugawana na bwana anasepa uone kama mtoto atakufa na njaaa....kukuta mwanaume responsible kama ruta....few in milion....wengine wameolewa na waume zao wana pesa lakini laki tatu kuona live ni ngumu...sebuse waishi mbali kudeka tu.
Ukute anakulipisha na uchakavu ('depreciation') uliomsababishia kwa kumzalisha. Kwa wengine kuzaa kunawachakaza kweli!
ruta wewe ni mwanamalenga?
JOJEETA....................mzazi mwenzangu anadai kuwa anataka kum'mwaga yule jamaa yake anirudie...lakini mimi sitaki kwa sababu naona hiyo ni vurugu........mtu akishaishia ni vyema aishie jumla.....................nikila matapishi yangu tena..........hata ardhi italaaniwa..........
Hii imetulia sana mkuu, naona mamake anageuza somo ahahaha, safi sana Ruta.
Rutashubanyuma ushauri wangu kwako ni kumuuliza listi nzima ya mahitaji ya mtoto na ujitoe mazima kununua each and everything mwenyewe kwani unalipia na shelter?
Kama hiyo ikishindikana omba ushauri kwa lawyer wako, uone hatua gani za kisheria unaweza kuchukua.
Hivi wanaume hawako protected kwenye mambo haya?
Heri sisi wa zamani
Haya ya kwenu jamani
yanatisha si utani
Laki saba mfukoni
Eti yafaa nini,
Hamna huruma jamani?
Ziwe ngapi ziwatoshe,
kulea mwana mmoja,
Tena msizikwepeshe,
Na hawara mkafuja,
Mkaja zua kasheshe
siku kunena kwa mja.
Pole Rutashubanyuma,
Kwani Lizy naye mama,
Atatetea hujuma,
Hata kama linazama,
Hao wana chao chama,
Kuhujumu kina baba.
lemonade huo muda uko wapi...........na isitoshe tuna makubaliano ambayo kila mwezi anatumiwa tatizo anadai hazitoshi ataka mara tatu yake......................
[MENTION]Kwakuwa unataka kuprotect jina lako inabidi uwe kondoo tu, labda ujaribu kurenagotiate.
Otherwise tazama jinsi ya kutumia intelejensia kwakuwa inaonekana wewe ni "mtu fulani" so utakuwa na maujanja ya kumbana
Haika..........mie siyo hit and run hata chembe kila kitu kilikusudiwa ni mtu baadaye kunibadilishia somo kinyume na makubaliano yetu ya awali...............ninajilaumu kwanini sikuyaandika...........
Kazi nzuri tuliifanya mimi na maama'ake
Matunda yake si khaba na mwana tukajaliwa
Ndoa kati yetu tuliiogopa kwani ni ndoana
Mwafaka ukafikiwa wa mgawanyo wa majukumu
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?
Mie jukumu langu lawa ni kubeba gharama
Mzazi mwenzangu kazi yake ni malezi tu..
Baada ya kipindi mwenzangu somo kageuza!
Akidai bila kumbeba na yeye malezi hayawezekani!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?
Bili ya mtoto yabebeka lakini kero za mama'ake zatisha!
Kwani mtoto hana makuu lakini mama'ake ataka mengi!
Mtoto yeye ni wa kulamba celerac lakini ya mama'ake!
Mama'ake ataka atunzwe akidai bila yeye hakuna malezi!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?
Baada ya purukushani na kasheshe kibao sasa..
Siri sasa yafichuka na mama'ake kashindwa uteja!
Kumbe mwenzangu ana dongo aona kadhulumiwa!
Anipasha khabari kuwa mtoto ni wa kwangu tu!
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?
Mama'ake apasua jipu kuwa jasho langu ni lake pia!
Adai kama tumeweza kuzaa kwanini tusile wote?
Mie simwelewi kwani mwafaka tuliweka sote.
Yawaje sasa anigeuzie kibao bila ya sababu?
Lakini matunzo ni ya mtoto na mama'ake atoka wapi?
lemonade huo muda uko wapi...........na isitoshe tuna makubaliano ambayo kila mwezi anatumiwa tatizo anadai hazitoshi ataka mara tatu yake......................
Mkuu mbona wapata shida na kuianika akili yako kirahisi hivi, gharama ya upendo mmejaaliwa MTOTO, Hasara ya chuki timiza wajibu mchungu. hatuung'oi mwiba kwa kuushindilia utokee upande wa pili wa mguu!