Kijana leo
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 2,860
- 812
Habari wana jf, nina tatizo na ninaomba msaada wako.
mimi nina mchumba wangu na ni mengi tuliyopanga ya hapo baadaye ili kutimiza azama ya mioyo yetu, lakini ninashindwa kumuelewa mama yangu anatatizo gani? Kwani kila niongeleapo habari kuhusu mchumba niliyenaye huwa mkari sana na anadai kuwa ninamzarau, kuna siku mtu wangu alipigwa na mdogo wa mama kwa madai kuwa eti hana hazi ya kuwa nami, mchumba niliye naye anadai kuchoshwa na tabia anayoonyeshwa na ndugu zangu wazi wazi kuwa hawamuhitaji tena hata mama yangu mzazi. Kweli nimeshindwa nifanye nini na ninampenda sana lkn anadai kuwa mzazi na ndugu zangu kama hawamtaki sasa hata nikija kumuoa ni nani atakaye kuwa karibu naye? Nimejaribu kumueleza lkn mama yangu anazidi kumuonyesha chuki dhahiri kuwa hampendi mchumba wangu.
Je, niachane na mchumba wangu kwasababu ya mama? Au niachane na mama yangu ili niendelee na mapenzi yangu kwa mwenzangu? Naomba msaada wako please.....
Baba yangu alikufa mwaka 2005 lkn kwasasa mama ameolewa kwa mara ya pili.
Hiyo ndo hasara ya wapenz wakike ku socialize na ndungu na wazazi wa mwanaume, mara nyingi msichana anapoanza kuwa karibu na ndugu wa mwanaume kabla ya ndoa haya hutokea ni vibaya sana tena sana, mm wifi zangu na mashemeji waliniona for the 1st time walipokuja kutoa mahari na baada ya hapo hatukuonana tena wala kuwasiliana mpaka siku ya sendoff ndo waliona tena ukumbini na kwa vile kabila lao haliruhusu wazazi wa mwanaume kuwepo cku ya mahari wakwe zangu waliniona kwa mara ya kwanza siku ya sendoff ukumbini
mama yako ni msichana?
kwasasa ana umri wa miaka 40
kwasasa ana umri wa miaka 40
Hiyo ndo hasara ya wapenz wakike ku socialize na ndungu na wazazi wa mwanaume, mara nyingi msichana anapoanza kuwa karibu na ndugu wa mwanaume kabla ya ndoa haya hutokea ni vibaya sana tena sana, mm wifi zangu na mashemeji waliniona for the 1st time walipokuja kutoa mahari na baada ya hapo hatukuonana tena wala kuwasiliana mpaka siku ya sendoff ndo waliona tena ukumbini na kwa vile kabila lao haliruhusu wazazi wa mwanaume kuwepo cku ya mahari wakwe zangu waliniona kwa mara ya kwanza siku ya sendoff ukumbini
Namuhurumia huyo binti
Heri akuache mapema
Maana mwanaume asiyekuwa imara ndugu watakuendesha kama gari bovu
Na kudhihirisha kuwa u dhaifu hadi wamempiga mchumba wako
Habari wana jf, nina tatizo na ninaomba msaada wako.
Mimi nina mchumba wangu na ni mengi tuliyopanga ya hapo baadaye ili kutimiza azama ya mioyo yetu, lakini ninashindwa kumuelewa mama yangu anatatizo gani?
Kwani kila niongeleapo habari kuhusu mchumba niliyenaye huwa mkari sana na anadai kuwa ninamzarau, kuna siku mtu wangu alipigwa na mdogo wa mama kwa madai kuwa eti hana hazi ya kuwa nami, mchumba niliye naye anadai kuchoshwa na tabia anayoonyeshwa na ndugu zangu wazi wazi kuwa hawamuhitaji tena hata mama yangu mzazi.
Kweli nimeshindwa nifanye nini na ninampenda sana lkn anadai kuwa mzazi na ndugu zangu kama hawamtaki sasa hata nikija kumuoa ni nani atakaye kuwa karibu naye? Nimejaribu kumueleza lkn mama yangu anazidi kumuonyesha chuki dhahiri kuwa hampendi mchumba wangu.
Je, niachane na mchumba wangu kwasababu ya mama? Au niachane na mama yangu ili niendelee na mapenzi yangu kwa mwenzangu?
Naomba msaada wako please.....
Ngoja kwanza....kupigana kati ya ma mdogo na fiancee wako kulisababishwa na nini? Nani alipigwa? Nawasiwasi mamayako alimchukia mchumbawako baada ya kupigana na dadayake
Me ni mtoto wa tatu kuzaliwa ktk familia ambayo mzazi mwenzie alimwachia.
Muulize kwanza mama yako nini kinamfanya amchukie huyo mchumba. Mwenye mapenzi haoni, na akiona chongo huita kengeza. Anaweza kuwa anamjua huyo mchumba wako "the other side", so usidharau. Waulize halafu lete hizo sababu watakazokuambia tuje tujadili hapa.