Mkuu anachosema Winnie ni kweli kabisa, mimi ilinikuta kwa mke wangu mpaka niliamua kumuacha kwa sababu nilivumilia kama miaka miwili na kila siku alikuwa ndio anaongeza, hela ya matumizi nusu kanisani nusu mnakula ndani, hela ya watoto nguo ukithubutu ukamuachia itaenda kanisani. na kila kitu tulichokuwa tunataka kufanya mpaka baba mchungaji atoe baraka. kila ijumaa mkesha unamuona jumapili jioni. kila siku anapitia kanisani anakuja nyumbani saa tatu. Hii kitu isikie kwa mwingine.
Hii ni kweli kabisa...tuliwahi kumuuliza ndugu yetu mmoja, kuwa analifikiriaje suala la uangalizi wa watoto wake ambao walikuwa wadogo..tukajibiwa "Bwana atatenda"....