Mama yako ni mke wa Mtu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
MAMA YAKO NI MKE WA MTU.

Na. Robert Heriel.

Moja ya mambo ambayo mwanaume anapaswa kujua anapokuwa kwenye ndoa ni kuwa Mama yake ni mke wa mtu. Anaweza kuwa Mke wa baba yako mzazi au mke wa Baba za wadogo zako. Au Baba tuu kama Baba aliyemuoa haijalishi hawajapata mtoto.

Tabia ya kulinganisha nguvu baina ya Mke na Mama mzazi ni tabia za watu wapumbavu na wajinga kifikra.
Unakuta mtu anakuuliza Ati kati ya Mama na Mke wako unampenda nani. Au ikitokea Mama yako anakuomba laki moja na hapo hapo mke wako anakuomba laki moja. Na mfukoni una laki moja. Je hiyo laki moja utampa nani.

Maswali hayo ni maswali ya kitoto na ya watu wajinga na wapuuzi.

Ni maswali ya kitoto na kipuuzi kwa sababu ni marahisi sana. Wala mtu mwenye akili hawezi uliza swali kama hilo.

Ndoa nyingi katika zama hizi zinaharibiwa na Mama wazazi na madada wa mwanaume. Ambao huwachanganya wanaume ambao ni watoto wao na kaka zao waliowapumbavu.

Mama zetu waliotuzaa lazima wajue kuwa wao ni wake za Baba zetu. Kamwe hawapaswi kutafuta upendo kwa Watoto wao zaidi ya Waume zao ambao ni Baba zetu.

Mama yako ni mke wa mtu. Jukumu la aliyemuoa ni kumpenda Mama yako. Mama yako kama anataka kupendwa anapaswa kudai upendo huo kwa Mume wake sio kwako wala kwa mtu yeyote yule.

Hii ni moja ya tabia ya kipuuzi ambayo imeleta athari kubwa kwenye ndoa nyingi.

Mama Zetu wamejifanya wao ndio wanastahili kupendwa kuliko wake zetu. Jambo ambalo sio sahihi kabisa.

Huu ni mpango wa kishetani kuharibu ndoa za zama hizi. Upendwe na mtoto wako kuliko anavyompenda mke wake ili iwe nini. Kwani Baba ambaye ni mume wako yupo wapi. Si udai upendo kwa Mume wake. Uache kusumbua watoto.

Wewe kama unataka kumpenda zaidi Mama yako basi Muoe ili awe mke wako kabisa ili tujue moja. Muache kusumbua watu hapa.

Na kama Mama unataka mtoto wako wa kiume akupende kuliko ampendavyo Mke wake basi nenda ukaolewe naye. Ili uwe mke wake usisumbue watu hapa. Wewe si unataka kupendwa. Basi kuwa mke ili yote yaishe.

Tabia hii imewagharimu wanaume bila ya wao kujijua. Ni tabia ya kipumbavu ambayo inatesa familia nyingi mno.

Nilikuwa nasoma katika mtandao wa Jamii Forum mdau mmoja aliuliza swali kuwa ati kama unagari, je ni yupi kati ya Mama au mk wako atakayekaa siti ya mbele pamoja na wewe?

Hili ni swali la kitoto na rahisi sana.
Jibu ni Mke atakaa mahali ambapo mume wake alipo kwa vile ni ubavu wake. Kama mume atakaa mbele basi mke atakaa mbele. Kama mke atakaa nyuma basi mke atakaa nyuma.

Mama atakaa nyuma na Baba. Kama Baba hatupo basi atakaa nyuma pekee yake au na wajukuu.

Unauliza swali hilo kama kichaa. Yaani uulize habari za Mama alafu umsahau Baba. Wakati Mama yako akikaa mbele na wewe Baba yako atakuwa amekaa nyuma na mkeo au.

Tufanye Baba amefariki. Lakini Baba akifariki Mama bado hachukui nafasi ya mke. Mama anabaki mama na ataheshimika kama Mama.

Mama bora kamwe hawezi taka kupendwa na mwanaye wa kiume kuliko Mkaza mwana wake. Kamwe hawezi.

Na Mume bora kamwe hawezi mpenda Mama yake kuliko anavyompenda Mke wake.

Unampenda sana Mama yako kuliko mke wako Umechanganyikiwa. Baba yako yupo wapi ambaye ndiye mwenye jukumu la kumpenda Mama yako. Au mume wa Mama yako yupo wapi ambaye ndiye walikubaliana na kupeana viapo vya kufa na kuzikana kipindi ukiwa haupo.

Leo kwa ujinga wako na upumbavu wako unaharibu familia yako kwa mambo ya kijinga. Kama unampenda Mama yako sana si umwambie unataka kumuoa ili uonyeshe mapenzi yako kwake.

Hujui unachokifanya kitakucost uzeeni. Hujui hilo. Kazi kufanya mambo kama mbuzi.

Usipoishi vizuri na mke wako tegemea kipigo uzeeni. Naye atajipendekeza kwa watoto kuliko atakavyojipendekeza kwako.

Atawagombanisha watoto wako na Bibi yao ambaye ndiye Mama yako. Hilo hulijui tuu umezubaa zubaa tuu.

Lakini ukimpenda mke wako kama mke wako kamwe uzee wako hautauchukia.

Wamama waache kujipendekeza kwa watoto wao kutafuta mapenzi ambayo walipaswa kupewa na Waume zao. Unataka kupendwa mwambie mume wako akupende.

Unataka kuhudumiwa mwambie mume wako akuhudumie. Kama ni mtoto wako atakuhudumia sio ukilinganishe na Mkamwana wako.

Ati mbona Mke wako umemnunukia kitenge mimi hujaninunulia. Mbona unampenda mke wako kuliko Mimi niliyekuzaa. Embu acheni hizo Jamani Mama zetu.

Unamuonea wivu Mke wa mtoto wako kama vile ni mke mwenza. Kama unataka upendo utafute kwa Mume wako sio kwa watoto.

Watoto watakupa upendo lakini sio kwa kiwango kile cha mke wake.

Nimalize kwa kusema, Na sisi Wanaume tutumie akili katika masuala haya. Kwa maana ukiyaendea kwa pupa unaweza piga dole chini. Pia sijatoa idhini ya kutowahudumia au kutowapenda Mama zetu waliotuzaa.

Tuwapende lakini sio kwa kiwango tunachowapenda wake zetu.
Mama kama anataka kupendwa aende kwa Baba. Huko ndio mapenzi yalipo.

Huwezi tumikia mabwana wawili. Huwezi mpenda mke na mama mzazi kwa kiwango sawa. Lazima mmoja umbwage chini. Na hapa lazima Mama ndio amwage tuu hakuna namna. Kwa kuwa yupo Baba wa Kumpenda. Lakini mwenye jukumu la kumpenda mke wako ni wewe mwenyewe.

Kuna mtu atasema kuwa Mama ni mmoja mke unaweza ukaoa na ukaacha na ukaoa hata mara mia. Upo sahihi. Lakini Elewa jukumu la kumpenda mke wako ni wewe mwenyewe. Hata uoe mara laki moja.

Oa mpende mke wako. Ukiacha ukaoa mke mwingine ukaoa mpende tena. Hivyo hivyo.

Alafu na ninyi Baba zetu ndio mnaosababisha Mama zetu watafute mapenzi kwa watoto wao. Wapendeni Mama zetu ili wasitusumbue kwenye ndoa zetu.

Nimefanya utafiti mdogo na kugundua kuwa, Wamama wengi. wasiopendwa na kupewa mapenzi na waume zao ambao ndio Baba zetu ndio huhangaika na kutaka kupendwa na watoto wao wa kiume.

Lakini Wamama wanaopendwa na Waume zao ambao pia ni Baba zetu huwezi kuta anaingilia mapenzi ya Watoto wake wakiume ati ili apendwe yeye kuliko Mke wa Mtoto wake.

Baba zetu wapendi mama zetu wasihangaike kutaka kupendwa na kujaliwa na watoto zao.

Kama ulikuwa hujui kumpenda sana Mama yako ni kumfanya Mama yako amdharau Baba yako. Kuwapenda Mama zetu ni kuwafanya wawadharau Baba zetu.

Ndio maana mimi Mama yangu yeyote atakayetaka kumponda Baba zangu ili nimpende yeye huwa namjia juu kama moto wa petrol.

Mimi nitakupenda kama Mama. Lakini sitakupenda ati kwa sababu unamponda Baba. Au Baba hawajibiki.

Hii ni tabia za kina mama. Wao kuwaponda Baba zetu ili tuwaone wao ni bora kuliko Baba zetu. Na kama tutaungana nao ndio huendeleza dharau kwa Baba zetu.

Kumpenda Mama zaidi kuliko Baba anavyompenda ni kumtesa Baba. Pia ni kumuumiza Mke wako. Na kama Mke wako ataumi ni wewe ndiye unaumia. Mwisho ndoa inakuwa ngumu.

Hii ndio Sababu Wamama wengi wakiona Watoto wamekuwa wakubwa na kuanza kujitegemea huanza kumzingua Baba. Hata kama sio baba yako. Lakini ni Baba ya wadogo zako.

Wengine hukimbia nyumba yaani kwa Baba yako alafu anakuja kwako kukaa. Nawe kwa upumbavu wako unampokea. Unavunja ndoa ya Baba yako au Baba ya ndugu zako kisa umefanikiwa kupata maisha.

Mwambie Mama akae hapo kukusalimia arudi kwa Baba. Kama anataka kukaa muda mrefu. Muite na Baba ili akae naye hapo hapo.

Kama hataki mwambie huwezi vumilia mambo hayo. Mwambie hukunizaa ili nivunje ndoa yako. Hukunisomesha ili nivunje ndoa yako. Rudi kwa Baba. Mwambie kama hili ndio lilikuwa lengo la kunisaidia basi ningekataa huo msaada. Mwambie kama ndilo lilikuwa lengo la kunizaa ningekataa kuzaliwa.

Nimeshuhudia mambo haya kwa macho. Wala sijahadithiwa. Tupo kwa ajili ya kuweka watu pamoja na si kuwatenganisha.

Wanaume tuwapende wake zetu ambao ndio Mama wa watoto wetu ili wasitafute mapenzi kwa watoto badala ya kutafuta mapenzi kwa sisi tuliowaoa.

Kumpenda Mama zaidi lazima ujue ni mke wa mtu. Unamfanya amdharau huyo mume wake ambaye anaweza kuwa Baba yako au Baba ya ndugu zako.

Unakuta Mam anamsemea Baba yako. Mara anakunywa pombe,. Sijui Malaya. na makorokoro mengine. Nawe kama lofa unaacha kumtumia Baba yako hela kisa Mama yako kakuambia usimtumie.

Acha ufala. Watumie wote. Kama ni elfu ishirini. Mtumie Mama kumi na tano alafu Baba mtumie elfu tano.

Wanawake wanahitaji akili na mabavu ili wakae sawa. Usiogope maneno yao hiyo ndio kawaida yao. Ndivyo walivyoumbwa. Watakutisha na kukupa maneno ya hofu usiwajali sana ikiwa unatenda haki.

Ukijifanya unawasikiliza sana utaumia mapema na wao ndio watakuwa wakwanza kukulaumu yakuwa wewe ndio mwanaume ulishindwaje kuyajua matokeo hayo.

Kumbuka Mama yako ana mume.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Somo zuri kutegemeana na situation. Pia elewa hakuna anayeweza kukupenda kwa ukweli (True love) kama Mama yako!
 
Bora nimpende mama yangu aliyenileta duniani kuliko kumpenda mtu ambaye sina guarantee ya upendo wake mambo yakienda mrama.
In short kila mmoja ampende mama yake.
 
Mimi nitampenda mama yangu kuliko mke wangu katika Maisha yangu yote

Mama kanibeba miezi 9,Mke tumekutana ukubwani

Miezi 9 ni kitu gani kulinganisha na anayekubeba kila siku..?

Anyway mwandishi ni WAPUMBAVU wale wanaolinganisha mama na mke, naungana naye kwa hilo.... sio kila kitu kina ulinganifu.
 
Huwa nakerwa sana na watu wanaofikiri mke na mama wanafaa kulinganishwa kwa namna yoyote ile. Labda tuwasaidie kuwatofautisha:
1. Mama yako anaweza kukuzalia mtoto?
2. Mkeo anaweza kukuzaa?
3. Unaweza 'kulala' na mama yako?
4. Mkeo anaweza kuwa mke wa baba ako nk nk.
Hawa wote wanaweza kuwa ni watu muhimu kwako ila kwa namna tofauti na wala hawafanani.
Watu na vihoja vyao vya kipuuzi eti mama kanizaa sijui kanilea na blah blah nyingi....mbona umetoka kwenda kuoa mtu mwingine kama unahisi mama ako anafit sehemu ya mkeo?
Mama ni mama na mke ni mke hawafanani kwa hiyo si busara kulinganisha vitu visivyo shabihiana kwa nafasi,majukumu na umuhimu.
Miezi 9 ni kitu gani kulinganisha na anayekubeba kila siku..?

Anyway mwandishi ni WAPUMBAVU wale wanaolinganisha mama na mke, naungana naye kwa hilo.... sio kila kitu kina ulinganifu.
 
Upendo na heshima havina ubaguzi wala ukomo.
Ukianza kuuwekea hadhi na madaraja upendo ndo hoja hizi zinakuja.
Gari ni gari na viti ni viti.
Ukivipa hadhi ndo mnaanza kupata shida.

Maisha ya nyumbani mnayapangia rank kama za kijeshi au kifalme.
Mama ni mama full stop. Ana haki zake na wajibu wake.
Mke naye ni mke. Ana haki na wajibu wake.
Hakuna siku haki zao au wajibu wao ukaingiliana labda kusaidiana tu.
Iweje mwingine awe zaidi au pungufu?
Mimi ni mke, na haipo siku nitaondoa role ya mama mkwe kwenye maisha ya mume wangu. Naye pia hawezi kuwa na nafasi yangu. Ya nini utupime kwa viti kwenye gari?
Mimi nina tofautiana hata na mwanae sababu misingi ya malezi tulopitia ni tofauti. Na pia mara nyingine mama na mimi tunamshangaa mwanae, wote tukiona hakubaliani na sisi. Ni mambo ya kawaida.
Vurugu mnazianzisha kwa hayo madaraja. Hakuna anayejisikia vizuri kunyang'anywa haki zake. Hizo hoja za viti zinakuwa hoja kukiwa tayari na shida. Jipangeni.

Mengine ni mambo ya tabia, mila na mazoea. Wanaume chagueni wake mnaweza kuhimili tabia zao.
 
Mke apendendwe na kujaliwa sana tu,Mama apendwe kiasi na kujaliwa sana tu.
 
KWA sisi wavuta misuba tuna amri

"muheshimu mama yako hata kama umemzidi umri "by snoopy dog

nyau😼
 
Una uhakika gani mama yako alikupenda ukiwa huko unakoita tumboni, unaweza kujua ni ‘attempts’ ngapi za kukunyofoa zilifeli...?
Hizo attempts hazijawahi kupangwa wala kufanywa..

Me n my mom love each other dearly
 
Back
Top Bottom