Mama wakwe hebu kuweni na busara kidogo

Mama wakwe hebu kuweni na busara kidogo

katusyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
1,455
Reaction score
434
Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa amembeba mama mkwe kwenye kagari kake Eskudo, kamechokachoka, kushoto kwake amekaa mke wake, mama mkwe kakaa siti ya nyuma.

Wako kwa gari imeshika lami, si likawapita Cruza v8, mama uvumilivu ukamshinda si akaropoka eti 'mwanaume huyo anapita kweli huyu ni mwanaume',

Jamaa alivyofika nyumbani si akalianzisha kwa wife, 'ina maana wewe umefurahia kauli ya mamaako, mbona ulikaa kimya aliponitolea kashfa?' Binti wa watu akajitetea, jamaa akatoa maamuzi ya kutombeba tena mamamkwe kwenye gari lake.

Wamama wakwe, kuweni wastarabu kidogo. Mnaweza mkahatarisha ndoa za watoto wenu kwa kauli zenu.
 
Teh teh teh daaa nimejikuta nacheka tuuu bila kujijua...
 
Back
Top Bottom