Mama wa Kambo

Pole mkuu. Nimeishi na mama wa kambo tangu nikiwa 4 years mpaka namaliza form six. Hakuwahi kunitesa kwa namna yeyote, in fact kwa kuwa nilikua mdogo kuliko watoto wake alinipendelea kama last born. Alinitetea dhidi ya makwezi ya hapa na pale ya mabro wakubwa (ambao ni watoto wake).

Mama sasa ni mzee sana kila akija dar hakosi kuja kwangu huku akinikumbusha jinsi nilivyo mtukutu! Alivyonipeleka shule etc. Nami tangu nipate kazi miaka 16 iliyopita sijawahi pitisha hata mshahara mmoja sijamtumia chochote.

N.b. Mama yangu yupo hai , walipeana talaka na mzee. Mama akabaki na watoto wa kike baba watoto wa kiume.
 
Daaah wewe mkuu uliinjoi ulikutana na mama wa kipekeee snaa na hongera kwa huyo mama aiseee...

Hao wamama sijui walikua wanapatikana wapi
 
Sio watoto wa kambo tu bali hata ndugu wa mwanaume. Kwa ufupi mwanamke hapendi kuishi pamoja na mtu yeyote wa upande wa mwanaume, si wakwe, si shemeji zake, si wifi zake, si watoto wa mume wake ambao hakuzaa na mumewe. Lakini kunyanyasika kwa ndugu wa mwanaume au mtoto wa kambo hutegemea sana na namna mwanaume anavyoishi na mwanamke.
 
Daaah wewe mkuu uliinjoi ulikutana na mama wa kipekeee snaa na hongera kwa huyo mama aiseee...

Hao wamama sijui walikua wanapatikana wapi
Yes wapo wachache sana. Nakumbuka tukiwa tunakula ugali kama maziwa yapo kidogo alikua akinipa mimi wengine wanakomaa na mboga tu. Sikumbuki kuwahi kunipiga (hata watoto wake hawapigi). Ana moyo wa kipekee.

Wanawake wengi mtoto kama sio wake inakuaga mtihani sana
 
Sijajua kwann wengi wana roho za ubinafsi kama hivi aiseeee
 
Mkuu huyo mama nina imani pia anapatana sana na mama yako mzazi 99% kama sikosei....
 
"Seriously niliweka chuki kwa baba,
Nilimchikia sana baba yangu, nilimchukia sana baba angu.. hii chuki mpaka leo inanitafuna niliteseka sana sana sana.."

"Nishawahi toroka hom"

Hahahaha umenikumbusha mbali sana tabora miaka hiyo usafiri ni treni tu. Hawa watu wasikie tu ila bado namshukuru sana Mungu kupitia hizo hustle ndiyo zilifanya kuwahi kuhitimu moja ya kozi ngumu sana. Mungu ambariki sana Mama hadi Leo sijaacha kumuita mama wala kumvunjia heshima.
 
Daaah mkuu show kali sana aiseeee...
Tupe kisa mkuu
 
Seriously niliweka chuki kwa baba,
Nilimchikia sana baba yangu, nilimchukia sana baba angu.. hii chuki mpaka leo inanitafuna niliteseka sana sana sana.😭
 
Seriously niliweka chuki kwa baba,
Nilimchikia sana baba yangu, nilimchukia sana baba angu.. hii chuki mpaka leo inanitafuna niliteseka sana sana sana.😭
Mkuu acha tuu..
Mungu atuepushe na haya majanga maana wazazi wetu ndo kila kitu
 
Ila kwa niliyopitia mimi Naomba Mungu anipe mke mwema ambaye huyo atakua mama wa watoto wangu milele.. kiufupi kuvunja ndoa hiki kitu kinaleta negative effects nyingi kuliko faida na ndio maana kwa uislam kuna vikwazo vingi kabla ya kumpa mke taraka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…