Mama wa Kambo

Pole sana mkuu, kuna wazazi wengu huwanyima watoto wao malezi ambayo ni haki yao na huleta mapenzi kati ya mtoto na baba
 
Usiwe Mbishi! Hata sisi tunao ila kulea mtoto ambaye analelewa na mama wa kambo ni mtihani mkubwa hususan wa kiume akiwa mdogo. Atanyanyasika tu. Mtoto anatakiwa alelewe na mama yake mzazi, kinyume na hapo ni msala kwa baba. Inabidi iwe FBI maana mtoto anaweza akawa ana tabia mbaya kweli au mama wa kambo anamuonea!
 
Duh, ulikuwa jehanam! Na baba naye alikuwa ndezi! Sasa hivi umeshawasamehe?
 
Unavuojisifia hapa hujui tu wanao wanavyoishi na Mama wa kambo. Wewe ukirudi ukawakuta shwari basi unatulia na kuja kutype JF. Kuna mambo mengi hujui.
Upo sahihi! Kiuhalisia mtoto alelewe na biological father and mother. Kinyume cha hapo ni mateso kwa mtoto
 
Daaah mpaka nimehisi huruma..
Mambo ni mengi sana nakumbuka hata mimi niliwahi toroka nyumba kisa mama alitishia kuniua..

Ilikua hivi siku hiyo mama alimdaka mwanae ambaye tulikua tunasoma shule moja , akamleta shule.

Kufika shule yule mama akawa anawambia walimu kuwa mimi namfundisha mwanae tabia mbaya.

Walimu wakatuma wanafunzi waje nitafuta. Mimi kuona ule msala nikakimbia hapo mama akatuma watu kwamba akinidaka nitakiona..

Mkuu nilikuambia kusikojulikana mpaka inafika jioni nilikua nipo mazingira mbali na nyumbani. Hiyo ilikua forest ya zamani wanapaita kwa mabula maeneo ya mahakamani kule.

Usiku ukafika sijala cha maana hapo nikalala tu nje. Plass bardi la mbeya lile nipo na nguo za shule tu.
Hapo yanakuja majibwa yanabweka na kuondoka

Just imagine kama ingekua ni mwezi wa wapiga nondo sijui ingekuaje au wachuna ngozi..

Inafika asbhi nikasema hapa sirudi nyumbani naenda moja kwa moja kwa bibi. Huko kwa bibi ni iyunga ambako anakaa bibi mlezi wa baba yangu.

Nilitoka forest mpaka iyunga hiyo napita ndani kwa ndani kuanzia kadeghe, meta, simike nzovwe.. nashuka mtoni pale kwa shitindi mpaka naikuta iyunga..

Nilikua hoi sijiwezi kuna mda walikuta nimelala mtoni wakaniamsha ili nitoke maana mda ulikua umekwenda...

Nafika kwa bibi namueleza kuwa naogopa kurudi nyumbani mama atanichapa .
Wakiniulizwa kama nilikua nateswa mimi nilikua nakataa... Sijui kwanini sikusema.

Wakamuita baba, baba amefika alikua mkarimu sana pale akawa ananiambia "" mwanangu wewe ndo ulinishauri nioe shida nn"" hapo sikua na neno.

Baada ya hapo akaenda moja kwa moja na mimi polis post pale meta hospital
Kufika pale nikatishiwa tishiwa nahisi alilipoti kama nimepotea..

Kwa haraka nikajua baba tushamalizana.
Aiseee tunafika karibia na hom alinishusha mabao hayo..

Baba ana mikono migumu sijapata ona kwanza vile vidole sijui vilikua vyake au bandia.. alinizabua mpaka tunaingia ndani nilikua sielewi..

Kesho yake asbhi naambiwa kwenda madrassa kufika madrasa ndo ikawa ishu nyingine maana yule ostadhi kama aliambiwa na baba kama mimi nilitoroka.

Madrassa ilikua pale msikiti wa mahakama kuu..
Kuna msikiti kwa chini hapa kama ushafika mahakama mbele kidog ya mahakama kuna ofisi ya mkuu wa polisi hapo kwa chini ndo kuna msikiti.

Yule ostadh alinichapa mkononi sio kwenye kiganja ila ni maeneo ya saa inapovaliwa..

Alinichapa sana sana sana mpaka miaka mwaka wa pili mama anakuja anakuta alama alitaka aende kumshtaki yule shekhe
 
Kwanza mimi sibishani mkuu.
Na pia sipingani na haya unayo yasema.
Lakini kama niwewe ndie unasema kwamba mtoto anaweza akawa ndio shida, hapo tafasiri yake ni kosa lilianzia kwenye malezi ndio mana mtoto leo amekua ni changamoto (hapa wakulaumiwa ni baba).
Pia kama mama ndio changamoto maanayake wewe baba ndie baba moumbavu kwa kuoa mwanamke ambae haujamfaham uzuri, pili unapokua baba usie faham mambo yanayo jiri nyumbani kwako then wewe baba ndio shida.
Mwishi niseme kwamba, mtoto anapaswa kulelewa kwao (yaani kwa baba). Kama ulijua kumzaa basi kua tayari kumlea mazee, mimi nimelea watoto wangu watano mwenyewe hadi wamekua na ndipo nikaja nikaoa baadae sana
 
Hakuna mkuu hakuna...
kama wapo ni wachache sana aiseee
 
Unavuojisifia hapa hujui tu wanao wanavyoishi na Mama wa kambo. Wewe ukirudi ukawakuta shwari basi unatulia na kuja kutype JF. Kuna mambo mengi hujui.
Kabisa.mwanaume ukiwa na mtoto wa nje na unahitaji kuishi nae mpeleke kwa bibi yake lakini kwa mkeo huwezi kuyajua yote anayopitia mtoto.Na wanaume mkishapenda huwa hamuoni kasoro kwa wake zenu sijui mnalogwa hamuelew kabisa kitu chochote hata muambiwe kwa upanga.🙌🙌🙌Mungu awasaidie watoto wanaolelewa na wale wasio wazazi wao halisi.
 
Hata mimi huwa sikubali kitu inaitwa divorce kwa wanangu hasa wakishakuwa na Watoto! Mtoto ni baba upande wa kulia na mama upande wa kushoto
 
Ameeen..
Ni kweli mkuu tukishapenda huwa hatuelewi kitu na hii sio limbwata ila ni.ukweli kabisa
Wanaume inahitaji uwe na utimamu sana kuweza kubalance hii hali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…