Mama wa Kambo

Shida ya kuwaachia watoto walelewe na mama zao ni kupata watoto walioharibiwa akili au mtazamo wa maisha. Yaani anakua sio mtoto anayeandaliwa kujali familia.
Labda huyo mwanamke hajielewi au wale wa mambo mengi na sidhan kama wote wanaolelewa na mama et hawajaandaliwa kujali familia Mimi Nina mfano hai wa kaka yangu mwaka. Anafunga 40 yupo nyumban Kwa baba na mama kazalisha watoto huko kawatelekeza huyo unamsemaje? Na yupo Kwa baba na mama
 
Naweza nisieleweke kwa urahisi kutokana na tafsiri ya kujali kuhusu familia. Ila tutolee mfano, msanii Diamond Platnumz, anavyoishi sasa unaweza sema ni matokeo ya namna alivyolelewa, mama alimjaza maneno, matokeo hata yeye Diamond alipofanikiwa bado amemkunjia baba yake, hajali kuhusu familia (yaani yeye mwenyewe kuwa na mama na baba) - hajali hilo.

Pili, namna anavyozaa na wanawake na kuacha walee watoto (labda yeye anatoa fedha), lakini unaona kabisa sio mtu wa kutaka kukaa na watoto home kwamba wawe chini yake awalee. Muktadha wangu ndio huo, kama nimeeleweka.

Kuhusu kaka yako, shida inaweza kuwa ilianzia kwa wazazi wenu namna walivyomlea
 
Mkuu afadhali wewe ulikua upo karibu na watoto wako..

Mzee wangu alikua hana habari na mimi..
Yeye akishakamilisha madaftari na peni hapo kuonana tena mpaka mwakani naingia darasa lingine.

Niseme kuwa baba angu alikua hazingatii kitu mpaka kuna kipindi nikawa nawaza au bana aliwekewa limbwata na yule MAMA
 
Taraka sio chap hivo mkuu...
Taraka zina sheria zake na taratibu zake au mybe sijui ila nasikia hutakiwi kutoa tatu kwa mpigo...

Kingine mzee wangu ni wale dini sana an yeye hana habari na ilm dunya...
Naposema dini namaanisha ni dini kweli..

Nilikua nipo tayari nitoroke shule niwahi madrassa ili tu kuepuka ile mikanda
 
Tukisemaga wanawake wana roho mbaya kwa wengine hasa watoto, mwanamke kuishi na mtoto wa mwenzake vizuri ni wachache sana katika 100 kumi haifiki
Ni kweli mkuu hii ni kweli.
Wewe kwa haraka haraka kama baba unaweza sema ni akili za mtoto kuhisi anaonewa ila deep down mama wa kambo ni complicated kinoma noma

Japo kwa miaka hii sijasikia hizi kesi japo ukipata hawa wamama wa huko kanda ya juu kusini walah utakubali show
 
Yapo mambo ya kinyama yanayotendeka sirini hujui tu na watoto ni ngumu kukwambia kutegemeana na biti wanalopigwa na mama yao.

Fanya uchunguzi kimya kimya utakuja kugundua kitu na utajilaumu kwa kuchelewa kujua mkuu.
Mkuu hivi ile hali ya uoga inakuaje sijui..
Maana uwezi funguka unahisi ukimwambia mzee,
Yeye atamface maza moja kwa moja na hapo watagombana alafu badae baba akiwa kazini show inarudi kwako.

Nakumbuka kuna kipindi mama mzazi alikuja nisalimia. Sasa kama unavyojua imefika asbhi nikasahau kumsalimia yule mama wa kambo..

Akaniambia wewe unisalimii kwakuwa upo na mama yako eeeeh haya tutaonana..

Na kweli tulionana mkuu hi siku ndo nilishikwa korodani nakubamizwa hovyo hovyo mbele ya wadogo zangu na hapa ilikua mda wa kula...

Me mpaka leo nina ule uwoga hata wa kupanda baskeli nahisi kama takalia korodani..
Jamni maumivu ya korodani yaacheni πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Mkuu Poor Brain pole sana. Wewe ni kati ya wengi wanaoteseka kwa sababu ya kuvunjika kwa mahusiano ya wazazi wao. Ndio maana zamani wanawake walikuwa wako tayari kufia kwa waume zao ili mradi tu asiache watoto wake kulelewa na mwanamke mwingine. Wanaume waelewe kuwa hakuna mwanamke mwenye utayari wa kulea mtoto wa mwanamke wanaechangia bwana
 
Unavuojisifia hapa hujui tu wanao wanavyoishi na Mama wa kambo. Wewe ukirudi ukawakuta shwari basi unatulia na kuja kutype JF. Kuna mambo mengi hujui.
Mateso ambayo watoto wa kambo hupitia chanzo ni baba zao mkuu, na wababa wasio jielewa ndio chanzo cha maumivu kwa watoto wao.
Kwahili mkuu mimi nasema wamama wema wapo na sana tu
 
Ubongo mbaya tunasubiri muendelezo

Au ndo unapiga yakuz yavuz?
Mkuu ngoja nendeleee...

Unajua baada ya kuja dsm nikagoma kurudi kwa baba..
Walilazimisha lakini wapi.

Kwa kipindi hiki nikaanza shule ya msingi majimatitu. Pale nilienda bila uwamisho sijui mama aliongea vipi na mkuu wa shule ila nikaanza rasmi darasa la tano.

Hapa sasa nikaanza kwa jina tofauti kutoka A mpaka M huu mda ambao niliona kumbe mi ni genius kabisa. Kwani nilikua ni miongoni mwa wanafunzi naefanya vzr japo watoto tulikua wengi yaan shule za dsm unakuta kuna A-G hivyo watoto wengi sana..

Nilisoma lakini hapa kati nitaruka kidogo maana hakuna la maana but end of the day nikahama dsm tukaenda lindi Mimi na mama mzazi.. huku napo nikaendelea na elimu yangu ya msingi mpaka nikamaliza..

Kimbembe kinakuja nafika secondary maza akabadili upepo kwa kuwa nishakuwa sasa sina budi kurudi kwa baba..
.hi kurudi kwa baba niliona sababu itakua ni pesa tu maana mama mwenyewe alikua sio mtu wa kukaa hom mara nyingi alikua anashinda shamba.

Mama angu ni mfanya biashara pia ni mkulima, alikua analima ufuta maeneo ya kilwa.

Niliwaza sana kurudi tena kwa baba daah but ukawa sio kesi maana nilikua tayari nipo form one

Safari ya kurudi kwa baba na mama wa kambo tena ikafika.. safari hii nipo understanding sio tena A mzembe mzembe sasa hvi narud kama M yaani nishakulia mazingira ya pwani sio mzembe mzembe kiufupi nilikua nipo vizr kichwani... Nilikua nina akili aiseee sio tu ya darasani hata ya kuchanganua mambo mbali mbali......
 
Mateso na visasi..
Mi mpaka umri huu yule mama sina mahusiano nae mazuri.
Kawalisha wadogo zangu maneno ya ajabu uwezi amini hawa wadogo zangu wananikataa kaka yao...

Wananiona ni mtu wa ajabu
 
Safi sana...
 
Sahihi kabisa mkuu. Eti mwanaume anakaa kizembe kwa kudanganywa na maigizo ya mwanamke kwamba anampenda mtoto wake.
Nasema nini....
Mwanaume anaeshindwa mkumbainimwanamke msanii, huyo ni mwanaume mpumbavu aiseee....
Na hili hutokana na sisi wanaume kuoa mwanamke pasipo mkufahamu vyede..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…