Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mke wa rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amevitaja vitu anavyovipenda kufanya akiwa nyumbani.
Akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa Clouds Media waliomtembelea nyumbani kwake kuelekea siku ya mama duniani, siku ya Jumapili, Mei 8, amesema, “Mimi ni mama wa watoto tisa, kulea watoto tisa haikuwa shughuli ndogo lakini nashukuru Mungu kwa baraka ya kuwapata watoto wangu. Watoto wangu wamekuwa wakisaidiana sana wakati wa kuleana na kushirikiana katika kila jambo. Ukiacha hao tisa nina watoto wengine ninaowasomesha nina watoto wengi sana, nawapenda sana wanangu naamini hata wao wananipenda pia.”
Aidha Mama Salma aliongeza, “ninapoona wanangu wanaandikwa vibaya kwenye magazeti, nachukizwa na jambo hilo kama mzazi, lakini natambua haya yanatokana na maisha tuliyoyachagua – maisha ya siasa, na hivyo ndio siasa ilivyo na la kufanya kama mzazi ni kumpa ushauri mzuri mwanangu katika kudili na jambo hilo.”
Mama Salma aliendelea kwa kusema kuwa anapenda kupika hata akienda jikoni hakuna atakayemuuliza kwanini ameenda huko kwa sababu anaenda kuwapikia watoto na mumewe.
Akijibu swali alilouliza Feza Kessy kuhusu anatumia jina gani wakati anamuita rais mstaafu Jakaya Kikwete, Mama Salma alijibu, “Huwa namuita mume wangu.”
Hata hivyo Mama Salma amezitaja kazi nyingine ambazo anazipenda kuzifanya akiwa nyumbani kuwa ni pamoja na kuandika kila kila kitu kinachotokea na kukaa na watoto na kuwafundisha na kuwaelezea vitu muhimu.
Chanzo: Bongo 5