Mama Rwakatare CCM amefikishwa Polisi kwa kosa la Kubomoa Nyumba

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
865
MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare amefunguliwa mashitaka katika Kituo cha Polisi Wazo Hill kwa uharibifu wa mali inayodaiwa ina thamani ya shilingi milioni 20.

Taarifa zilizopatikana katika kituo hicho zenye Jalada la Kumbukumbu WH/RB/9029/2014 UHARIBIFU WA MALI na kuthibitishwa na mlalamikaji aliyejitambulisha kwa jina la Grayson Justine, zinaeleza mchungaji huyo alivunja nyumba ya Grayson kwa greda hali iliyomfanya mmiliki huyo kuzimia na kulazwa Zahanati ya Mico iliyopo Wazo Hill baada ya presha kupanda.

Katika mahojiano na waandishi wetu katika Ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge, Dar wiki iliyopita, Grayson alikuwa na haya ya kusema:


"Kiwanja nilichojengea nyumba nilikinunua kwa Jumanne Rajab, Agosti 24, 2011 na makubaliano yalifanyika kwa kuandikishiana Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Bunju ‘B' na kila mmoja alikuwa na mashahidi wake.

"Kutokana na kuchoka katika kupangisha, niliamua kuchukua mkopo wa shilingi milioni 20 kazini ili nijenge haraka na kuhamia, ujenzi ulianza Septemba 21, mwaka 2013 mpaka kufikia mwezi huu (Novemba) nilibakiza kupaua na nilitarajia kuhamia mwanzoni mwa mwaka kesho.

"Baadaye nilikwenda Moshi kwenye msiba wa baba, niliporudi Dar nilimaliza siku moja tu, nikaripoti kazini. Nikiwa kazini Novemba 11, mwaka huu nikapigiwa simu na jirani kwamba nyumba yangu inabomolewa na greda, alifikiri kwamba nimeshaonana na Mchungaji Rwakatare na kukubaliana naye.

"Nilikwenda kule, kufika nikakuta hakuna jengo! Nilidondoka chini, sikujua kilichoendelea, nilipoteza fahamu, nilijitambua nikiwa Zahanati ya Mico.

"Kinachoniumiza sana ni kitendo cha kuvunjiwa nyumba yangu bila kushirikishwa, bora hata angenifungulia mashitaka kama anaona nilivamia kikwanja chake."

"Yeye ana uwezo, ana ghorofa ya zaidi ya shilingi bilioni moja iweje anionee na kunivunjia mimi maskini niliyejenga kwa fedha za mkopo?

"Kituo cha polisi nilifika karibu mara nne lakini mpaka leo hii sijapewa mpelelezi wala hawajafika eneo la tukio, nataka sheria ichukue mkondo wake."

Mwandishi alifika katika eneo la tukio na kushuhudia kifusi kinachodaiwa kuwa ni iliyokuwa nyumba ya Grayson iliyovunjwa na imezungushiwa ukuta na geti kupigwa kufuli.

Hata hivyo, Uwazi lilifika katika Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Bunju ‘B' na kuonana na mtendaji Abdallah Mkeyenge ambaye alikiri kuwepo kwa mvutano baina ya watu hao."Hii barua ya makubaliano ya kuuziwa Grayson kiwanja inaonekana imetoka ofisini hapa lakini mimi kipindi hicho nilikuwa sijahamia ofisi hii.

"Ninachokumbuka kuna kipindi Mchungaji Rwakatare alikuja na milioni tano kuwapa Grayson na mtu mwingine yaani kuwapoza lakini walikataa kuzichukua," alisema mtendaji huyo.

Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kuhusiana na madai hayo alisema yupo bungeni hivyo alimwagiza msaidizi wake, Jerad Abeid kuzungumzia sakata hilo ambapo alisema eneo hilo mchungaji analimiliki tangu mwaka 2005 na hati ziko ardhi Wilaya ya Kinondoni. Alibomoa nyumba ya Grayson akijua ni eneo lake la siku nyingi.

"Unajua katika maeneo hayo kuna watu walikuwa wakishirikiana na ofisi za mtaa kuuza kiwanja cha mchungaji kwa siri na tayari watu wanne walishauziwa lakini walikuwa hawajajenga, mchungaji aliamua kuwapoza kiubinadamu na wameshaondoka bado watu wawili akiwemo huyo Grayson," alisema Jerad
.

Grayson aliyebomolewa nyumba!!.jpg Mama rwakatare.jpg . lwakatale.gif
 
Huyu mama hafai kuwa kiongozi wa umma wala wa dini sijui walimchagua kwa vigezo gani.nimefuatilia mambo yake Mara alitapeli vi wanja vya mjane sijui Ni mbezi beach ilikua Ile Kama sikosei.wajirekebishe kwa nafasi walizonazo katika jamii haya mambo Si mazuri kutajwa tajwa kwa sifa mbaya hata kidogo.
 
Kwa jinsi nnavyomfahamu Mama Rwakatale ni mtu mwema sana, Mungu akubariki akulinde zaidi na zaidi
 
Pamoja na watu kumponda na kumtukana huyo mama lakini lazima tukubali kuwa nchi yetu haina sera nzuri ya makazi...

Matatizo kama haya ya ardhi si aghalabu kuyapata mahali hadi mahali ndani ya nchi yetu na ndio chanzo cha makazi holela...

Kuna watu wananunua maeneo makubwa na wanashindwa kuyaendeleza, baadaye yanavamiwa na wenye shida za makazi na kuzua zogo...

Maeneo mengine hayafai hata kwa makazi lakini ndio wapata watu wamejenga holela...
 
Pamoja na watu kumponda na kumtukana huyo mama lakini lazima tukubali kuwa nchi yetu haina sera nzuri ya makazi...

Matatizo kama haya ya ardhi si aghalabu kuyapata mahali hadi mahali ndani ya nchi yetu na ndio chanzo cha makazi holela...

Kuna watu wananunua maeneo makubwa na wanashindwa kuyaendeleza, baadaye yanavamiwa na wenye shida za makazi na kuzua zogo...

Maeneo mengine hayafai hata kwa makazi lakini ndio wapata watu wamejenga holela...
watu8 ulichosema ni kweli na kama kuna idara inaongoza kwa kesi nyingi basi ni ardhi
 
Last edited by a moderator:
Kwa jinsi nnavyomfahamu Mama Rwakatale ni mtu mwema sana, Mungu akubariki akulinde zaidi na zaidi

Ni kwa vile tu JF ni uwanja huru na yeyote anaweza kupost chochote almradi tu havunji kanuni na taratibu, simhukumu mama Rwakatare lakini wema wake si wa kiwango hicho, na kumbuka Mungu huwa habagui kwenye kutoa baraka zake huwapa wema na wabaya pia
 
Huyu mama hafai kuwa kiongozi wa umma wala wa dini sijui walimchagua kwa vigezo gani.nimefuatilia mambo yake Mara alitapeli vi wanja vya mjane sijui Ni mbezi beach ilikua Ile Kama sikosei.wajirekebishe kwa nafasi walizonazo katika jamii haya mambo Si mazuri kutajwa tajwa kwa sifa mbaya hata kidogo.

walimpendea dhuruma. ccm ote wazurumaji
 
Unatetea ujinga.Huyo mama km kweli mtu mwema na wa mungu kwanini hawezi kukaa mezani na watu maskini kujadiliana nao.Huyo mama sijui anawaongozaje hao wenzake katika ibada ilhali anaonekana hana uvumilivu km aliokuwa akiutimiza yesu kwa kondoo zake.Mungu amlipe kwa lile analolifanya kwa maskini.Huyu mama hata kwao Mngeta wilaya ya Kilombero wanamjua vizuri tu mambo yake.Sijui km pepo ataweza hata kuinusa kwa staili hiyo.
 
Huyo mama asili ni mpogoro ila kuna eneo linaitwa Mngeta wilaya ya Kilombero ndio kwao sehemu wanakoishi kabila la Wandamba.Watu wanasema ni mndamba ila yeye anakataa kuwa yeye si Mndamba bali ni mpogoro.Kwahiyo nadhani kauli yake inaweza kuwa ndio ya kuishika kuwa mpogoro.Japo hawa Wanda
 
Wandamba w nikikabila kidogo sana hivyo wakitoka nje ya ifakara hujiita Wapogoro.Huenda kuwa ni sababu ya Mchungaji nae kujiita Mpogoro.
 
Back
Top Bottom