Mama Rada Bi Clare Short kupewa tuzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Rada Bi Clare Short kupewa tuzo

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Feb 24, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280
  Waziri wa zamani wa Uingereza wa ushirikiano wa maendeleo Bi Clare Short aka mama rada anatarajiwa kupewa tuzo mahsusi na kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu Tanzania [LHRC] kwa msimamo wake wa kupinga ununuzi wa rada.

  Bi Clare Short alianzisha mzozo wa kupinga ununuzi wa rada katika bunge la Uingereza,nchi ambayo ni mfadhili mkubwa wa maendeleo ya Tanzania,na hasa bajeti ya taifa ambayo zaidi ya 30% hutegemea wafadhili.Hoja zilizokuwa zikitumiwa na Bi Clare katika kupinga ununuzi wa rada ni pamoja na rada hiyo kuuzwa kwa bei ghali tofauti na thamani halisi lakini pia ubora wake ulikuwa wakutiliwa shaka.  Source:Raiamwema
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Ni kwani nini asipewe Andrew Chenge? Maana yeye ndiye MSHINDI katika sakata zima to the extent kwamba serikali ya Uingereza imeamua kurejesha "kick-back"!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,324
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Baba_Enock,

  Chenge anastahili kupelekwa segerea lakini muungwana anajua akimgusa lazima Chemkapa na system nzima itawajibika.

  Kwa kuanzia LHRC wamefanya jambo zuri sana kukumbuka mchanga wa mama rada raia wa Uingereza aliyekuwa na uchungu na fedha za Tanzania kuliko chenge mtanzania aliekuwa anawaza vijisenti
  .
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,115
  Likes Received: 2,412
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri kumtuza mama huyu. Ni watu wachache wenye moyo kama wake!
   
 5. d

  damn JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Tony blair na Mkapa Je? Wapewe zawadi ya sampuli ipi....?

  damn them!!!!!
   
 6. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mama Rada alijitahidi kututetea sana, kiburi cha Mkapa na misemo yake ya wavivu wa kufikiri viliishia kuitia nchi hasara ambayo mpaka leo bado tunailipia.

  Natamani siku ifike tumpandishe Mkapa Kizimbani kwa kuitia nchi hasara
   
 7. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anastahili kupata hii tuzo
   
 8. w

  wasp JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Che Nkapa amekwenda Iringa vijijini wiki moja iliyopita akaringa kwamba hajazomewa. Kumbe anapenda kuzomewa. Sasa mama Rada (Clare Short) anakuja ili tumpe tuzo kwa kuwajali na kuwasemea walalahoi wa Tanganyika walio fisadiwa fedha zao kwa kiburi cha Che Nkapa cha kusema watanganyika ni wavivu wa kufikiri kwa kutofagilia rushwa ya ununuzi wa rada.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...