Mama ni mama: Kwanini baba asihusishwe?

Anayemtunza na kumbiwa huyu ni mwanao ndiye baba
 
Hii ni kauli mbiu tu ya kumfanya mwanamke kuwa wa thamani machoni pa watu na si kama wewe unavyofikiria,ila ni ukweli mtupu mwanamke amepewa uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na bado akasema am okey,uvumilivu wake,upendo wake,huruma yake,heshima yake,busara yake ujasiri wake ingawaje anaonekana ni dhaifu,busara na hekima yake,maarifa yake japokuwa yaonekana ni madogo hakika hakuna kama mama,mama ni mama tu.

Hii kauli mbiu ilikuja kutokana na mama kutotambulika katika jamii,alikuwa anaonekana ni chombo dhaifu kisichofaa,hakuthaminiwa,alikuwa hana kauli yoyote katika jamii,alihesabika kama mtoto tu,Baba alikuwa anakula kwanza kisha mama ndiyo ale na wanawe,kulima ilikuwa ni kazi ya mama na wanae,kuangalia mazingira ya nyumbani na malezi ya watoto ni kazi ya mama,mama ahakikishe mumewe afurahi,watoto wafurahi,nyumbani kuna chakula cha kutosha,kwa haya yote haya kwanini wasiseme Nani kama mama,!!! Mama ni mama.
 
Kweli wapo tuliotokea familia ambazo tumeona upendo wa baba zaidi ya ule wa mama.. sikatai mama ni mama ila wapo wababa wenye mguso wa pekee kwa mtoto
 
Hakuna kama mama alikubeba tumboni miezi 9 akakuzaa kwa uchungu ,akakulea kwa uaminifu mkubwa na upendo usio kifani
baba ndio anapendwa na amechangia wewe kuwepo lakini jukumu kubwa la kuhakikisha upo ulivo leo ni yeye
hakuna kama mama
 
Siwezi kumbagua mmoja wao.Kila mmoja ana mema/udhaifu wake.Na wajukuu wao walifahamu hilo.
 
Mumy I love u, no ne like my mumy. never ever till the end of this world.
 

*upendo* sina hakika sana na neno hili litumikavyo. Anyway km ni kumwinua toka bondeni it is okey. Ningependa zaidi km wangeanza na kauli kuwa tumtambue mama na umuhim wake ktk jamii. Wengi wanafanya vzr kwa mengi.
Ila baba asibezwe pia.
 
Hakuna kama mama alikubeba tumboni miezi 9 akakuzaa kwa uchungu ,akakulea kwa uaminifu mkubwa na upendo usio kifani
baba ndio anapendwa na amechangia wewe kuwepo lakini jukumu kubwa la kuhakikisha upo ulivo leo ni yeye
hakuna kama mama

Dah, msifie na baba kwa mazuri yake. Alichangia sana kwenye maisha yako hadi Leo uko ivo....
 
Felix umemaliza kila kitu barikiwa zaidi hakuna ka mama jamani loh
 
Last edited by a moderator:
majibu rahisi kwa maswali magumu. what if baba ndio angekuwa anabeba mimba?

mara utasikia mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama hapo hapo sifa apewe mama.

ni sawa na kusema kichwa ndio bora kwenye mwili eti kwa sababu kina macho na ubongo. lakini tunasahau

baba ana role zake kibaiolojia na kijamii ambazo hazifanywi na mama. mama hawi special kwa kubeba mimba maana amekuwa designed kubeba mimba
 
*upendo* sina hakika sana na neno hili litumikavyo. Anyway km ni kumwinua toka bondeni it is okey. Ningependa zaidi km wangeanza na kauli kuwa tumtambue mama na umuhim wake ktk jamii. Wengi wanafanya vzr kwa mengi.
Ila baba asibezwe pia.

Hakuna anayembeza baba, mama anasifiwa kwa kuwa tumeona wakifa hata kwa ajili ya watt wao, atapigwa atateswa atatukanwa lakini kamwe hataacha watt wake lakini kina baba akipata mchepuko hata mtt aliyemzaa atamuona ni mbwa, mama akifa wengi wa akina baba hawajui kulea. Ukiumwa hospital uko na mama mara nyingi but naona dunia ya sasa kina baba wamepunguza ubabe nawaona wanalea watt vizuri sana hospital na mashuleni nawaona wakiwashika watt wao mikono.
Nimempenda sana baba angu na hata babu yangu ni wanaume wazuri sana nitawasifia mpk siku naingia kaburini.
Ili umuhimu wa bsba ujulikane be responsible maana hata kuzaa mbwa nae anazaa!
 
Huwezi mlinganisha mama na baba,baba kazi yake ni kupanda mbegu baada ya hapo biashara imeisha na walioko ni asilimia chache sana
 
hakuna kama mama jamani, mama ni mama tu.
Elimu ya mamaa, haina ada wala cheki, ila ni zaidi ya elimu ya chuo kikuu.
Si maneno yangu bali ni maneno ya mwanaume mwenzio christian bella.
 
Huwezi mlinganisha mama na baba,baba kazi yake ni kupanda mbegu baada ya hapo biashara imeisha na walioko ni asilimia chache sana

Too bias.... Open your eyes and see other things
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…