English Learner
JF-Expert Member
- Jan 1, 2012
- 366
- 453
Mpendwa Prof. Mama Ndalichako,
Salaam za heri na pongezi kubwa kwa kazi njema unayoifanya kuinusuru elimu ya Tanzania. Hizi pongezi unastahili na vile vile wewe pamoja na Mzee Magufuli mnastahili kuungwa mkono na kila Mtanzania Mzalendo.
Haka ka-barua kafupi nakuandikia kuhusu marejesho ya mkopo wangu niliochukua Bodi ya Mikopo kufadhili ka-Digrii kangu ka kwanza. Kwanza ninataka kukujulisha kuwa awali kwenye Serikali zilizopita zilizokuwa za majambazi na mafwisadi sikuwa na morali ya kulipa deni. Lakini kwenye hii Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk. Magu wala nisingehitaji kukumbushwa au kusubiri kuandikwa magazetini kama mdaiwa. Nilipanga kulipa TZS 3,500,000/= ka bhaa! kwa mkupuo. Nilipanga kulipa hilo deni kutokana na sehemu ya pensheni yangu mara tu baada ya kukabidhiwa na PPF. Niliacha kazi nikiamini pensheni yangu itakuwa mtaji wangu lakini kwa bahati mbaya haikuwa hivyo. Toka mwezi wa tano tarehe 21 PPF wananizungusha na mwisho wameniambia kuwa fao la kujitoa limefutwa.
OMBI:
Mama Ndalichako nakuthibitishia kuwa mimi nina nia ya kulipa deni. Hivyo nakuomba uende PPF uchukue kiasi cha pesa ninayodaiwa na Bodi na zinazosalia waache waendelee kunidhurumu tu.
Nazidi kukuombea afya njema wewe na Dk. Magu ili muendelee kuinyoosha Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Dk. Magu na Mama Ndalichako.
Wenu Mtiifu,