Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,097
- 43,309
Kwa watu wanaojua au hata wale ambao wanafuatilia siasa za visiwani humo ni rahisi kuona kuwa mgawanyo huu wa kijamii ambao unatokana na siasa unaweza kuwa na madhara makubwa zaidi visiwano humo labda kuliko mgawanyo mwingine wowote katika historia ya karibuni ya Zanzibar. Binafsi bado nafuatilia kwa karibu katika kusoma na kuelewa kile hasa kinachoendelea ama hadharani au nyuma ya pazia. Hata hivyo hofu yangu ni kuwa mgawanyiko huu mkubwa utakuwa na madhara makubwa sana Zanzibar na kurudisha jamii nyuma. Kinyume na kauli ya baadhi ya watu kuwa Wazanzibari katika kudai "Mamlaka Kamili" au "Serikali Tatu" wako wamoja ushahidi ni wazi kuwa hawana umoja huo... tafakari:
Mwana:
Amani Karume akiwa na viongozi wenzake ambao wanadaiwa ndio wadai wakubwa wa "Mamlaka Kamili" ya Zanzibar na hata kudai "Serikali Tatu" ambapo Zanzibar itakuwa na Mamlaka Kamili - whatever that means.
Siku si nyingi (nne tu) Mama amesimama na Wana CCM wenzake tena huko huko Zanzibar na kusema maneno mazito tu ya kudai mfumo wa Serikali Mbili huku akionya watu wanaotaka Serikali Tatu (in extension akiwemo mwanae)...
Nauliza tu: Nini kinaendelea?