Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,115
Mwanamke mmoja aitwaye Mwanaisha Matere (37) na Mtoto wake Baraka Maita mwenye umri wa miaka 7 Wakazi wa Kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wameuawa kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa viwiliwili vyao na vichwa huku chanzo kikiwa bado hakifahamiki.
Diwani wa Kata ya Milola lilikotokea tukio hilo Masoud Mohamedi ameiambia amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia November 24,2023 ambapo Majirani waliona damu zikichuruzika mlangoni na walipofungua mlango walikuta viwiliwili vya marehemu vikiwa havina vichwa.
Amesema katika nyumba hiyo walikuwa wakiishi na Mtu mmoja Mgeni ambaye alikaribishwa kama Mfanyakazi wa shamba lakini baada ya tukio hilo hakuonekana nyumbani hapo na wakati tukio linatokea Baba wa Familia hiyo alikuwa amesafiri na kuwaacha nyumbani hapo Mke, Mtoto wake pamoja na Mgeni huyo ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyewaua na kuwakata vichwa Mama na Mtoto kisha kuondoka na vichwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga , Julius Ningu amethibisha kutokea kwa tukio hili ambapo amesema jitihada zinaendelea za kumsaka Mtuhumiwa wa tukio hilo.
Chanzo: Millad Ayo