Mama mwenye nyumba sijui ananitafuta nini jamani!

Mama mwenye nyumba sijui ananitafuta nini jamani!

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,756
Reaction score
2,309
Hapa napokaa mama mwenye nyumba ni Mama wa Nymbani tu ni mama wa Makamo kidogo, sasa anavituko juu yangu mpaka simuelewi!

Kwanza nikipata mgeni wa Kike tu atanuna vibaya hanisemeshi mpaka

akitoka utasikia ameanza kuniuliza huyo ndo mke wako?

Mara siku zingine anaingia kwangu na kanga tu eti anaomba dawa ya mswaki anataka akaoge!

Mara niazime sabuni ya Kuogea!

Akisikia tu naangalia Muvi Mpya tu anakuja kuazima!

Siku zingine huniomba Ufunguo nikitoka misele Nakuta Poti La Ubwabwa na Minofu Hasa siku za jumapili!

Huwa najiuliza sana aisee ukizingatia mme wake Soja yuko mkoa kikazi, Sasa huyu mama ananitafutia majanga mwenzenu Hata simuelewi kabisa!

Napata wazo La kuhama hapa Huwa Sina Michezo na Wake za Watu kabisa Akuu! Nisijefumwa nikapigwa Bastola bure!
 
yaani hama fasta maana 0713 ipo hatarini! halafu siku hizi si meno ya tembo tu yanauzwa hat ya bina damu yanayong'olewa bila ganzi ni malighafi na ngozi kwa ajili ya pochi na mikanda huko uingereza!
 
Jiandae kwa fumanizi la soja..ama Limbwata usilotarajia we mchekee tu utaona faida yake..nyama we, hivi mtu aanze tu kuniomba funguo wa chumba changu bila kumtengenezea mazingira? kweli tunatofautiana..doh
 
Mkuu mgonge mara moja mpigo wa kufa mtu ili kulinda heshima,tafadhali usicheze mechi peku,tumia zana muda wote
 
Fanya juhudi ujenge ya kwako maana kuhama tena hapo yani kuhamia nyumba nyingine tena ya kupanga si suluhu huenda ukakutana na zaidi ya haya.

JENGA YAKO hata kama ni kichumba tuuu
 
yaani hama fasta maana 0713 ipo hatarini! halafu siku hizi si meno ya tembo tu yanauzwa hat ya bina damu yanayong'olewa bila ganzi ni malighafi na ngozi kwa ajili ya pochi na mikanda huko uingereza!

Na hii ndiyo dawa ya wachangakia wake za watu...
 
Endelea kula hiyo minofu mpaka na wewe uliwe ndo akili itakukaa sawa
 
Fanya juhudi ujenge ya kwako maana kuhama tena hapo yani kuhamia nyumba nyingine tena ya kupanga si suluhu huenda ukakutana na zaidi ya haya.

JENGA YAKO hata kama ni kichumba tuuu

Niko najenga Zangu hukooo Kongowe Ntahamia tu, Uzuri hapa pazuri hapana Vurugu wapangaji tupo wawili tu Na Mama yetu mwenye Nyumba Na kila mtu ana Luku yake ila ntahama tu hamna jinsi
 
Mkuu mgonge mara moja mpigo wa kufa mtu ili kulinda heshima,tafadhali usicheze mechi peku,tumia zana muda wote

Siwezi maana nikionja tu ntanogewa na ubaya ubaya zaidi hataki mgeni wangu wa kike aje hapa sasa itakuwa balaa na mi nikapata Kidosho wa maisha
 
Jenga kamilisha uhame kimya kimya. Ila kama unahama siku moja kabla ndo unakula mzigo.
 
Siwezi maana nikionja tu ntanogewa na ubaya ubaya zaidi hataki mgeni wangu wa kike aje hapa sasa itakuwa balaa na mi nikapata Kidosho wa maisha
Nimekuelewa mkuu,kama ni hivyo mpotezee kwa kumpa laivu kuhusiana na mwenendo wake,Mweleze wazi kwa jinsi alivyokuzoea una wasiwasi mme wake anaweza kukutilia shaka.Mwambie apunguze mazoea ili mmewe awe na amani
 
Kumuelewa umemuelewa ila kuna kashetani kanakokuchelewesha kufanya maamuzi ili kakucheke baadaye,wee kachekee tuu!!!
 
Anakutega huyo, anakupa mitihani makusudi, haya akili kichwani mwako
 
Niko najenga Zangu hukooo Kongowe Ntahamia tu, Uzuri hapa pazuri hapana Vurugu wapangaji tupo wawili tu Na Mama yetu mwenye Nyumba Na kila mtu ana Luku yake ila ntahama tu hamna jinsi

Ukihama niunganishe nihamie kwenye hiyo nyumba please!
 
Na usile chakula utalishwa shuntama uwe kama zezeta
 
kijana huna kazi ya kukuweka busy ? mbona kama vile ninyi nyote ni watu wa kushinda nyumbani?

halafu na wewe umekuwa mkarimu sana kwake..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom