Mama,Mtoto na mjukuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama,Mtoto na mjukuu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Speaker, Sep 8, 2011.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  "Baba na mama nashukuruni sana kwa mda wote ambao tumekua pamoja,
  najua nimewakosea na kuwadhalilisha sana,ila pamoja na kuondoka kwangu naombeni mnisamehe.
  Nitawakumbuka siku zote ntakazo kuwa hai na sitasahau kuwaombea popote nitakapo kwenda."

  "Ondoka haraka sana,nikimaliza kula nisikukute hapa.Tena ilipaswa uondoke wewe na mama yako
  ukiendelea kupiga kelele hapa mtafuatana wote sasa hivi".

  "Tafadhali robi,ondoka mwanangu baba yako ataniua mimi"

  Ni maongezi yaliyo jaa huzuni,kati ya robi na wazazi wake mzee mghaka na bi.mukungu!
  Ni siku ambayo robi hata isahau katika maisha yake,kwani alipo gundulika tu ana dalili za ujauzito alio upata
  akiwa mdogo sana,tena akiwa darasa la sita katika umri wa miaka 15 alifukuzwa kijijini kwao kiabakari kwani
  katika mira ya wakurya ilikua ni aibu sana kwa mtoto kupata ujauzito akiwa nyumbani,achilia mbali umri wake mdogo.

  Pamoja na kulia machozi mengi sana na kuomba msamaha,robi hakusikilizwa!
  "Kana nke unguntuna ore mona,esi niche nkoghoghe uwe",....kusikia kauli hiyo ya mzee mghaka,akimaanisha
  "we mtoto unanitafuta nini lakini,nita kuchinja wewe",robi hakukumbuka hata kuchukua nguo yoyote ile ingawa hakua
  na nguo za kukusanya hata hivo tofauti na nguo ya shule na gauni jekundu alilo nunua baada ya kumsaidia bi.mukungu kuuza
  gongo mwezi mmoja uliopita.Ni hapo ndipo lilipo kua chimbuko la kufukuzwa kwake.

  Akiwa ameahidiwa kununuliwa nguo mpya,robi alifanya kazi kwa moyo wote kilabuni siku hiyo ili biashara iende vizuri
  na apate zawadi toka kwa mama yake.katika kutoa huduma mara akaingia kijana wa kisukuma aliye onekana mtanashati
  na ukizingatia ndio mara yake ya kwanza kufika kijijini hapo.

  "unaitwa nani dada",....aliuliza wilbad,"naitwa robi",robi alijibu kwa sauti ya uoga kwani hakuzoea kuongeleshwa
  na wateja kuhusu chochote zaidi ya "taongerya ichubha imwe",...wakimaanisha ongeza chupa moja ya gongo.
  "mbona nguo inechanika hapa,hebu chukua hii mia tano ukashone",...wilbad alijitahidi kumvuta robi kwa vijizawadi ili awe karibu naye.
  Siku iliyo fuata ilikua ilikua ni siku ya mnada,robi alinunua gauni alilo lipenda sana kwani watu wengi walikua wana yavaa kwa mda huo.
  Alipo maliza alienda kumsaidia mama yake kuuza gongo,ingawa siku hii ilipaswa kwenda kukusanya kuni.

  "Robi takora ongende kotenya",...bi.mukungu alimsisitiza robi asipende kazi ya kuuza pombe ila awahi akakusanye kuni.
  Hakukaa sana kilabuni,aliondoka na kwenda porini kukusanya kuni,kama ilivo ada aliongozana na wadada wengine wakubwa kwa wadogo.

  Mara nyingi kijijini pale,kama ilitokea kijana akamtaka binti kimapenzi basi sehem pekee ya kukutana ni either kaenda kukusanya kuni au
  ni zamu yake kwenda kuchunga.Huko ndiko ziliko gesti hausi zao.
  Wilbad alikua ametoka kisesa mwanza,kwenda kutafuta mkaa toka kwa ajili ya kuuza mwanza mjini.Biashara ilikua nzuri sana kwake na
  siku hiyo alikua ameenda kupakia mkaa porini akiwa na roli alilo kodi kwa kazi hiyo.

  "Oh,robi za toka jana?",...alimchangamkia robi baada ya kumuona porini kule bila kutegemea.
  "nzuri,shikamoo",..robi alijibu,kwa kiswahili chenye rafudhi ya kikurya.
  Wadada wengine waliendelea kukusanya kuni,robi akiwa amefunda hela yake aliyopewa kwenye kanga alifurahi kumuona wilbad
  siku hiyo kwani aliiona kama mzigo na mama au baba yake angemuona nayo basi angepata kipigo kwa mbwa mwizi.

  "kaka,asante kwa hela yako,hii hapa chukua.",...robi alitaka kumpa lakini wilbad alikataa katakata.
  "kwanini unarudisha,kwani hukushona nguo yako au haitoshi?",..alilalamika wilbad
  "hapana,nitapigwa na baba",...robi alisisitiza
  "usiogope,chukua na hii ufiche utatumia hata kwenye mnada ujao kidogo kidogo",...wilbad aliongeza sh.600 kwa robi.

  Kuona vile robi alibaki na kigugumizi,kama ilivo kwa wengi alidanganyika na ni siku iliyo badilisha maisha yake
  kuwa ya kuhangaika mji mmoja hadi mwingine.

  "niende wapi maskini,wilbad sijui ntampata wapi mimi jamani?,...robi aliwaza akiwa kichakani
  kando tu ya kisima wanapo chota kijijini hapo.
  Alikua na njaa sana,kulia sana kulimfanya asinzie kwa mda asio ujua.

  "hehehehe,uuuuuu",...ni vicheko alivosikia alipo situka toka usingizini.ni mabinti wenzake walio kua wakimuongea na
  kumcheka kwa kufukuzwa kwake.
  Alianza kulia kimya kimya hasa baada ya kutambua kwamba ni karibu kijiji kizima kitakua kinajua kuhusu hali yake
  ya ujauzito hivi sasa.

  "hivi ataenda wapi,sasa yule msukuma wa mwanza atafikaje huko?na hauli hana jamani,...heheheeeee akome
  alijidai mzuri sana kutuzidi wakubwa zake",...waliendelea kuongea wenzake.

  Robi alikaa kimya mda huu,..."hua anakusanya mkaa anapeleka mwanza,mwenyewe hua namchuna kweli ila sikubali
  kupewa mimba kizembe hivo.Tena akija ntaondoka naye maana mlembo wake hatakuwepo tena",....waisiko alisikika akijitapa.

  Robi sasa alijua kwamba wilbad anatokea mwanza,na kwamba kumbe mwanza ni mbali na anahitaji kuwa na nauli ya kumfikisha.
  *********************************************************************
  Robi atafika vipi mwanza?
  Atapata wapi nauli?
  Vipi wilbad,atakubali kubeba majukumu?,................,....tukutane toleo lijalo.
  ********************************************************************
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Tunakusubiria umalizie.
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante sana boss,ila ni ndefu mno naangalia jinsi ya kuifupisha isichoshe watu kusoma.
  Kwanini mama,mtoto na mjukuu?
  karibu tena
   
Loading...