Mama mkwe amefanikiwa!

Mama mkwe amefanikiwa!

Powel Mizengo

Senior Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
126
Reaction score
24
Nakumbuka ni muda mrefu toka nilipoleta thread yenye Title "MAMA MKWE ANANING'ANG'ANIA". Kama wengi wenu mlivyonishauri,niliupokea ushauri nikachanganya na akili zangu na matokeo yake mi nikaamua kuchukua mdogo mtu!!!kwa sasa nipo naishi na huyo mdogo mtu!!!!Tatizo kubwa ambalo limenifanya nirudi tena kwenu wadau ni hili; Huyu binti imekuwa ni kawaida yake pindi naporudi toka kwenye matembezi yangu na hasa napokuwa nimerudi nimepombeka,yeye anazama kwenye Wallet yangu na kuchota kiasi cha pesa akidhani mi sina kumbukumbu ya kiasi nilichoacha!!!Ameshanifanyia mchezo huu muda sasa!!Si kwamba simwachii pesa za matumizi bali sielewi tatizo lake ni nini kunipekua mifukoni!!! Jamani wadau,huyu binti bado sijalipa mahali(Bride Price) Nilipewa ili kureplace dada mtu ambaye kisa chake nilishawaeleza!!!Na tayari tulikuwa na mipango ya kuoana mwishoni mwa mwaka huu yaani Desemba!!b. Sasa haka katabia kananitatiza!!!!Naomba mchango wenu wa ushauri manake sielewi kama anaweza badilika kweli!!!
 
Mbona hilo siyo tatizo?pesa si zenu wote?kuna shida akajichukulia?mxxxxiu
 
Ni mimi sielewi au wewe hueleweki?
Kwanza heading inamtaja mama mkwe then contect ni shemeji,sijui story yako na dada yake ila sielewi unapewaje mdogo mtu awe replacement. Hapo ana replace hisia zako kwa dada yake au uwepo tu wa mwanamke kwenye nyumba?
 
hazimtoshi unazompa na kusema hawezi.... soon ataanza kutoa gegedo apate nyingine... ila title na yaliyomo tofauti.....
 
Inaonekana story yako ipo ki episode zaidi so Funguka usaidiwe at least hata utoe intro kwa ufupi nini kilikupata na Dada mtu mpaka ukapewa shemejii a.k.a mdogo mtu alafu ndo ufunguke kulikoni na mamkwe .
 
Tukumbushe kwanza kisa cha dada mtu lol

Ni mimi sielewi au wewe hueleweki?
Kwanza heading inamtaja mama mkwe then contect ni shemeji,sijui story yako na dada yake ila sielewi unapewaje mdogo mtu awe replacement. Hapo ana replace hisia zako kwa dada yake au uwepo tu wa mwanamke kwenye nyumba?

MMU huwa ina vistori fulani hivi kama zile siriz za Kifilipino...

Hii ya leo huenda ni part II na baadaye tutaletewa episode nyingine tuburudike kina siye macho kodokodo...

Kwa umbea wa fasta fasta hebu piteni hapa muone wenyewe hii stori ilipoanzia...

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/601245-mama-mkwe-ananingangania.html
 
Ni mimi sielewi au wewe hueleweki?
Kwanza heading inamtaja mama mkwe then contect ni shemeji,sijui story yako na dada yake ila sielewi unapewaje mdogo mtu awe replacement. Hapo ana replace hisia zako kwa dada yake au uwepo tu wa mwanamke kwenye nyumba?

Kama hukusoma thread iliyopita itakuwa ngumu kuelewa hii!!!Hivyo pita ndg yangu kwani hutakuwa na cha kunishauri!!!Uzi huo ni kwa wale waliohusika kunishauri kwenye last thread!!!
 
Huyo ni mkeo tayari unaongelea ndoa gani! wakati uko naye na nyumbani kwao wanajua,vinginevyo umeshakula tunda umeona tofauti ya dada mtu na yeye unataka umuache, mwambie tu aache huo mchezo.
 
Ni mimi sielewi au wewe hueleweki?
Kwanza heading inamtaja mama mkwe then contect ni shemeji,sijui story yako na dada yake ila sielewi unapewaje mdogo mtu awe replacement. Hapo ana replace hisia zako kwa dada yake au uwepo tu wa mwanamke kwenye nyumba?
Huyu bwana namkumbuka alikuja hapa akasema ameachana na mpenzi wake ila mama mkwe ambaye ni mama wa huyo mpenzi wake alikuwa anamsihi amchukue mdogo wa huyo aliyekuwa mpenzi wake kwakuwa jamaa alikuwa mwema katika hiyo familia,jamaa ndo analeta mrejesho kwamba alikubaliana na huyo mama mkwe na kumchukua huyo binti sasa analeta maswahibu ya huyo binti kuwa anamuibia pesa hapo umeelewa mtiririko madam
 
Nashukuru kwa kunisaidia kuwaupdate!!!Manake nilikuwa napata tabu kuanza upya!!Nadhani umesomeka vema sana mkuu!!!Big up sana mkuu!!
 
malimwengu..........nisije nikabeua chai yangu ya tangawizi hapa
 
Back
Top Bottom