Mama Rwakatare aichongea JamiiForums

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale, Leo pia kapeleka swali lake Bungeni.

Waziri kaitetea JF na kuwashauri wabunge kuwa ni chombo cha habari cha kijamii.

UPDATE:

MHE. CYNTHIA H. NGOYE (k.n.y. MHE. MCH. DKT. GETRUDE P. RWAKATARE) aliuliza:-

Jambo Forum/Jamii Forum imekuwa ikisambaza habari za uwongo kwa watu mbalimbali bila kuchukuliwa hatua:-
Je, ni nani mmiliki wa Jambo/Jamii Forum?

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA Akajibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mch. Getrude Rwakatare Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo/Jamii Forum ni mtandao wa kijamii ambao haujasajiliwa Tanzania bali umesajiliwa nje ya nchi. Mmiliki wa mtandao huu wa kijamii anaweza kuwa Mtanzania au mwananchi yeyote ambaye siyo Mtanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA inatoa leseni mbalimbali za kusimamia mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na leseni ya huduma za matumizi ya mtandao (Application Service License) na leseni za Utangazaji (Content Service License)

Katika usimamizi wa TEHAMA, Mamlaka inatoa leseni inayotambulika kama leseni ya huduma ya mtandao kwa watoa huduma wakubwa na kuwawezesha kuhakikisha kuwa huduma ya mtandao inapatikana nchini. Wenye leseni za aina hii hutoa huduma ya kuhifadhi (hosting) mitandao mbalimbali ikiwemo ya kijamii.

Mhehsimiwa Naibu Spika, upatikanaji wa huduma za mtandao hupelekea watu mbalimbali kuanzisha tovuti za kijamii. Uanzishwaji wa tovuti za kijamii haulazimishi mtu kujisajili wala kujitambulisha na huanzishwa na mtu yeyote aliye popote duniani.

Kutokana na asili na miundo na Tovuti za kijamii, mamlaka haijasajili wala kutoa leseni kwa tovuti hizo, kimsingi maudhui yanayoandikwa katika tovuti hizo za kijamii ni maoni ya mtu binafsi na yasiyoangaliwa iwapo ni ya kweli au la.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE:
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri aliyoyatoa Naibu Waziri nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Kwanza kabisa tukubaliane baadhi ya ujumbe unaoandikwa katika mitandao hii kwa kweli ni maudhi, tena maudhi makubwa. Wakati mwingine ni matusi hata matusi ya nguoni ambayo ni kinyume kabisa na utamaduni wa Mtanzania.

  1. Je, Serikali iko tayari kuleta sheria hapa Bungeni ili kuweza kuwabana basi hao Watanzania ambao wanajitokeza kuandika maneno ya matusi na mengine ya uchochezi katika mitandao hii ili kukomesha tabia hii?
  2. Katika huduma za internet café ambazo zinatolewa hapa Tanzania nyingi zinaruhusu hata watoto wadogo kuingia kutumia internet café hizo. Kwa kiwango hicho basi huwa na access ya kuweza kusoma hata mitandao ambayo inafundisha ngono kabla ya wakati. Je, hilo nalo Serikali iko tayari kuleta sheria hapa ili kuelekeza wenye internet café kuangalia ni umri gani ambao unahurusu watu kuingia katika mitandao hiyo? ahsante sana. (Makofi)


NAIBU SPIKA:
Majibu Mheshimiwa Naibu Waziri ukizingatia swali la msingi hasa kuhusu Jamii Forum na matatizo yake makubwa. (Akapigiwa makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ngoye, kama ifuatavyo: kwanza kuhusu Sheria iko katika mchakato na imefikia katika ngazi ya juu ya kuweza kuleta Muswada wa Sheria ya Habari hapa Bungeni. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge awe amejiandaa na awe katika wakati mzuri wa kuweza kuangalia na kuchangia katika sheria hiyo itakayozungumzia mambo ya habari hasa hasa tukizingatia kwamba habari inapatikana mahali popote, habari inapatikana kwa television, habari inapatikana kwa radio, habari inapatikana kwa gazeti na habari inapatikana kwa mitandao. Kwa hiyo, tuangalia hizi media zinazoweza kutoa habari mbalimbali, kwa hiyo tuangalie ni kwa namna gani habari zote hizi zinazopatikana katika maeneo yote haya zitaweza kuleta tija katika taifa letu.

Kuhusu internet café vile vile amezungumzia kuweza kuona vitu ambavyo tunadhani si maadili kwa watoto. Nizungumzie tu hili kwamba anayemruhusu mtoto na anayetoa hela kwenda internet café ni sisi wazazi. Kwa hiyo, ni wazazi sisi ambao tunaruhusu watoto wetu kwenda ku-access internet. Lakini internet siyo tu kwenye internet café, siku hizi simu zetu, IPOD zetu na laptop zetu katika nyumba zetu zinaweza kuchukuliwa na watoto wetu na wanaweza ku-access. Kwa hiyo, sisi Wazazi tuchukue wajibu wetu kama wazazi kuhakikisha kwamba tunawaelekeza watoto wetu waweze kuangalia vitu ambavyo vina maadili na vinajenga taifa letu.
 
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale,Leo pia kapeleka swali lake Bungeni,pia imeonekana mtandao huu ni wa CHADEMA..
Nawasilisha.....

ndio maana wanaomba viti maalum vifutwe? 330,000/= kuuliza mmiliki wa JF OMG!!!!
 
Mkuu karibu hapa JF, mimi naitwa only83..JF ni zaidi ya uijuavyo..hata mkuu wa kaya ni member hapa na uwa anafaidika na mawazo ya wanaJF.. wazo la kuwa JF ni ya CDM nadhani ni ule muendelezo wenu wa kutumia kufikiria kwa kutumia *Masaburi*

Kama vijana na wanachama wa magamba hawajui umuhimu wa kutumia mitandao kama sehemu ya kujijenga msisingizie JF kuwa ni ya CDM..Hakuna uhusiano wa JF na CDM isipokuwa member wengi wa JF wanaweza kuwa ni wanachama wa CDM, japo sina uhakika sana na hili.
 
Wana JF kutokana na mtandao huu wa kijamii kuibua na kueneza siri za Serikali Wabunge wa CCM wameridhia Mtandao huo ufungwe kama ilivyokuwa Ze Utamu na Mtoa Hoja ni Mchungaji Getrude Lwakatale,Leo pia kapeleka swali lake Bungeni,pia imeonekana mtandao huu ni wa CHADEMA..
Nawasilisha.....

Lwakatale ni tapeli, mwizi wa roho za watu wenye shida. Anawadanganya kuwa shida zao zitaisha. Ikitokea kuwa na forum za kumwambia ukweli anakuwa mbogo. Anawadanganya watu wasio na matumaini, kama waliokosa watoto/uzazi, mahanisi (wanaume, magonjwa yasiyotibika eti kwa kuwaombea watapona.

Uongo hakuna atakayezaa na umri wa miaka 60 mwanamke!!! anampa hope eti ana nguvu za kumwombea akazaa. Ukiwafumbua macho kwa uongo kama huo ndani ya JF tukufu, anapeleka bungeni ufungwe!1 Shame!!
 
JF Founder/team ilienda bungeni mwaka jana kama uzee haujafuta kumbukumbu zangu, huyo Mh Mchungaji Dr Mama Rwakatare siku hiyo hakuwepo bungeni?
 
Kama kuna siku magamba watakua wamekosea step ni kufunga JF maana kitakochokuja kitakuwa moto zaidi ya JF.

Kwa nini kitakachofuata kiwe moto zaidi? Ina maana JF ni kwa ajili gani au wengine hatujui? Mimi ninanvyojua JF upo kwa ajili ya ku-interchange views, kutoa mawazo yenye tija kwa maendeleo ya taifa na mambo mengine kama hayo. So naamini uamuzi wowote wenye kutaka kufunga JF utakuwa umefanyiwa tafiti za kutosha na kujiridhisha kuwa mtandao huu hauna tija kwa maslahi ya taifa.
 
Nahisi maamuzi ya kufunga jf hayatakuwa sahihi sana kwa sababu kwa kufanya hivyo kunapunguza fursa kwa wanajamii kutoa mawazo yao juu ya mambo mbalimbali yanayotokea ktk jamii.
 
Back
Top Bottom