Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
MKE wa aliyekuwa mgombea urais kutipia vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA Regina Lowassa ameliongoza Baraza la Wanawake CHADEMA (Bawacha) mkoani Morogoro kufanya usafi katika Hospitali teule ya wazazi ya Mafiga.Mama Lowassa aliyeongonzana na Mwenyekiti wa baraza hilo taifa Halima Mdee pamoja na Mbunge wa viti maalum Devota Minja walifika katika hospitali hiyo majira ya saa tatu na kuanza kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kufeka nyasi.
Mara baada ya usafi huo ambao pia uliwajumuisha akinana wa CHADEMA katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Mama Lowassa aliwashukuru wanawake waliojitokeza kufanya usafi na kuwataka kuendelea kufanya hivyo kila mara.“Mwanamke anamchango mkubwa katika jamii nimeona ni jambo la bushara kujumuika na nyinyi katika Manispaa hii ili niweze kufaya usafi kwani kufanya hivyo ni kuonyesha umahili wa mwanamke katika jamii ya kitanzania”alisema Lowassa.
Mama Lowassa alisema kuwa kufanya kwake ufasi ni kuielimisha jamii kuwa mwanamke anamchango mkubwa hususani katika suala zima la utunzaji mazingira kwani kufanya hivyo kutasaidia kujiepusha na magonjwa ya milipuko.Aidha Mama Lowassa aliwatembelea wodi ya akina mama walijofungua na kuwapa pole ambapo pia alijionea changamoto mbalimbali katika hospitali hiyo na kuahidi kusaidia kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
Katika maadhimisho hayo kiongozi wa BAWACHA taifa Halima Mdee kwa kushilikiana na Mbunge wa viti maalumu mkoani hapa Devota Minja walitoa vifaa vya kuhudumia akina mama wajawazito vyenye thamani ya shilingi 5 Mln na elfu 20.Maara baadha ya tukio hilo Minja alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwani anatambua changamoto zilizopo katika hospitali nyingi hapa nchini ambapo alisema ataendelea kutoa misaada mbalimbali ili kutatua changamoto zilizopo hospitalini hususani kwa wanawake.
Aidha Minja alisema kuwa katika mahitaji ya hospitali hiyo ni pamoja na mashine ya Dropa ambapo alisema kuwa mashune hiyo kwa mkoa wa Marogoro imekosena na kuhaidi atainunua jijini Dar es salaam ili ailete hospitalini hapo.Sufuni Msuya ni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo amewapongeza viongozi hao wa CHADEMA kwa kitendo hicho ambapo amewataka kuendelea kufanya hivyo ili kunusulu maisha ya akina mama wakati wa kujifungua.