Mama kabadili upepo. CCM wamegeuka wapinzani wa mama, na wapinzani wamegeuka kuwa wafuasi wa mama

Kwenye siasa kila kitu kinawezekana mkuu kwa hivyo hakuna la kushangaza. Mimi nasubiri nione msimamo wake kuhusu mafisadi na ulinzi wa raslimali zetu nyingi kabla sijaanza kumshangilia.

Na mwanasiasa anaweza kubadili gia angani wakati wo wote.

Hitimisho: Usiwekeze lo lote kwa mwanasiasa kwa sababu anaweza kukugeuka wakati wo wote...
 
Hapo ndo mlipoambiwa CCM itatawala milele na inawezekana. CCM wapo na mama bega kwa bega sema kwasababu wapinzani hawataki kuonekana wapo upande mmoja na CCM ndo mnalazimisha ionekane hivyo. CCM wamemaliza msiba wa JPM tayari wamekuwa wamoja. 99.9% ya wanaoongoza serikali wakiongozwa na Mama Samia ni CCM na mbaya zaidi 98% ni wateule wa JPM ,Sasa ukisema wapinzani wanaisapoti serikali ya Mama Samia lakini hawasapoti ilani ya CCM si utaonekana chizi!????... Tukubali tukatae wapinzani wa Tanzania hawajui wanataka nini na wanasimamia nini?, Wanaendeshwa na matukio tu. Mtu Kama Lissu alikuwa anapaishwa na Magufuli kuwa hai, baada ya JPM kufariki hana sera yoyote, ali survive kwa kumkandia JPM na serikali yake basi.

Panga maneno utakavyo, lakini kwa sasa mtafanya kazi za halali. Zile kazi za kuteka, kuua na kutishia watu sasa zimefika mwisho, maana boss wenu yuko motoni. Mungu kaamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika. Hivyo muone bashite akupe mafao yako, maana ukichelewa atakula hela zote muishie kuzinguana. Ccm muwe wamoja, muwe vipande is none of our business, tunachujua nchi hii haiko mikononi mwa yule mtu muovu tena fullstop.
 
Heshma kubwa kwa CCM
Uwekezaji wao kwenye rasilimali watu na ukomavu wao kisiasa wana uwezo wa kendelea kushika dola miaka mingine 100

Yaani hilo la kuwekeza kwenye raslimali watu, ukomavu wa kisiasa hilo unajua ww, sisi tunachojua muovu yuko motoni, saa hii tunaishi kwa amani. Tuna furaha sana maana nchi haiko mikononi mwa shetani tena fullstop. Hivyo utaamua utabaki na mavi yako nyumbani au utakuja nayo mjini, hilo halituhusu.
 
Hapo ndo mlipoambiwa CCM itatawala milele na inawezekana. CCM wapo na mama bega kwa bega sema kwasababu wapinzani hawataki kuonekana wapo upande mmoja na CCM ndo mnalazimisha ionekane hivyo. CCM wamemaliza msiba wa JPM tayari wamekuwa wamoja. 99.9% ya wanaoongoza serikali wakiongozwa na Mama Samia ni CCM na mbaya zaidi 98% ni wateule wa JPM ,Sasa ukisema wapinzani wanaisapoti serikali ya Mama Samia lakini hawasapoti ilani ya CCM si utaonekana chizi!????... Tukubali tukatae wapinzani wa Tanzania hawajui wanataka nini na wanasimamia nini?, Wanaendeshwa na matukio tu. Mtu Kama Lissu alikuwa anapaishwa na Magufuli kuwa hai, baada ya JPM kufariki hana sera yoyote, ali survive kwa kumkandia JPM na serikali yake basi.
Tunachojua Mungu amesikia kilio chetu ametuondolea kiini cha chuki
 
Panga maneno utakavyo, lakini kwa sasa mtafanya kazi za halali. Zile kazi za kuteka, kuua na kutishia watu sasa zimefika mwisho, maana boss wenu yuko motoni. Mungu kaamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika. Hivyo muone bashite akupe mafao yako, maana ukichelewa atakula hela zote muishie kuzinguana. Ccm muwe wamoja, muwe vipande is none of our business, tunachujua nchi hii haiko mikononi mwa yule mtu muovu tena fullstop.
Mkuu siku hizi umekuwa kama Minyoo,Ushuzi.1 na Mmawia. This is too cheap for you. Umekuwa mtu wa mipasho kama wamama wa uswahilini, uwezo wako na upeo ulioonekana nao huko nyuma ni tofauti na sasa. Nilichoongelea na unachoongelea ni vitu tofauti.. mada inahusu ccm soma tena labda utaelewa.
 
Umekuja na marking scheme nini? Pokea mrejesho wa mlichokuwa mmpeandikiza kwenye hii nchi. Hakuna kitu kinaitwa ccm nje ya madaraka ya urais. Ccm bila kuwa na mwenyekiti mwenye madaraka ya urais, ni kama kikundi cha ngoma tu.
 
Wasiomtaka mama ni CCM waamiaji kama Polepole au Slaa
Wenyewe kama Nape au januar makamba wako peace na SSH
 
Back
Top Bottom