Mama Janeth Magufuli kama Abigaili leo, Mungu amuepushe na Akili za Mwendokasi

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,580
18,182
Honestly,Nampongeza Mama Janneth Magufuli kwa maneno mazito aliyoongea katika hotuba yake kwenye Ziara ya huko Ruangwa alipowahutubia wazee.Mwenyezi Mungu amuepushe na busara hewa na akili za Mwendokasi.

Ametoa hotuba ya kinyenyekevu na ya busara kuhusu umuhimu na mchango wa wazee kwa Taifa hili.

Nimeona pia misaada aliyotoa kwa Wazee.

Ni juzi tu Rais Magufuli alitoa lugha isiyofaa kuhusu wazee kuwa ni wala rushwa hivyo anataka vijana.Wengine tulilaani na kukemea kauli hii ya kibaguzi kabisa kabisa bila kutafuna maneno kuwa the statement was uncalled for,reckless and disguisting !

Sasa Hili la Mama huyu mnyenyekevu mwenyebusara Jane, limenikumbusha jambo moja tu kwenye biblia Kitabu cha 1 Samuel 25 juu ya Mwanamke mmoja mrembo sana na Mwenye Busara,mnyenyekevu na mwenye Upendo wa hali ya juu na Hofu ya Mungu .

Huyu ni Abigail aliyekuwa mke wa Nabal.

Abigaili aliepusha mume na familia au himaya yake kuingia katika matatizo baada ya mumewe aliyekuwa hajali na mwenye kiburi na dhihaka kuingia katika mgogoro na Daudi aliyewasaidia na kuwatunza vijana wake wachunga mifugo nyikani wakiwa na uhitaji lakini baadae Daudi alipopata shida na kuomba msaada kwa Nabali akajibiwa majibu ya ovyo,dharau na Nabali .Suala hili lilimkasirisha sana sana Daudi na kutuma jeshi lake la watu 400 kwenda kumuulia mbali Nabali na kuteketezea mbali himaya yake

Abigaili alipogundua kuwa Nabali katoa lugha chafu kwa Daudi basi akawaomba wajakazi wake wafunge vyakula na vinywaji na kuwapindisha juu ya Punda.Njiani akakutana na Daudi na Jeshi lake na Kuinama chini kwa Unyenyekevu mbele ya Daudi na kuomba radhi na kuinusuru familia yake na Mumewe ingawa Mungu alikuja kumuadhibu Mumewe

Naendelea kuasa wanasiasa vijana ambao hawajao ,tumuombe Mungu sana atupe Abigaili wetu lakini vilevile atuepushe na tabia za Nabali.

Ubarikiwe sana Mama Jannet kwa hili la leo.

Methali 9:10 inatuasa kumcha Mungu ndio chanzo cha busara na Maarifa.

Barikiwa sana Mama

Aluta Continua,Victory Ascerta....

Ben Saanane
 
Sikujua kama Ben nae ni mbumbumbu kiasi hiki!

Hivi hao wazee aliosema Magu ndio wale alioenda kuwaona mama Jane?

Acha upofu mkuu ushabiki utakuua....
Bora umemuuliza hilo swali. Wazee aliowataja Magu ni kama Lowasa, Chenge, Rugemalila, Reginald Mengi, Ndesamburo na wengineo wa aina hiyo ambao hawafai kabisa kupewa nafasi za kiuongozi kwa vile ni wapigaji
 
Mimi nimefurahishwa na pongezi zako kwa First lady
Ila kwa taarifa yako Wazee alio kuwa anawaongelea Magu ni wale walioko kwenye Ajira
Alitumia neno wazee, akimaanisha wale wanao karibia kustaafu au wale walio staafu wakaongezewa muda baada ya Kustaafu
(sijatetea kauli ya Magu au kuikanusha ila nilikuwa naweka tu kumbukumbu vizuri)
 
@Lizabon,

Unajua una heshima kiasi kidogo uliyobakiza hapa JF.Ilinde kaka

Hivi mimi kuonge ukweli kuhusu mazuri aliyofanya Mama J ndio ukasirike? Unataka nimponde?Siasa hazipo hivyo.Grow up!

Wazee ni Baraka na ubaguzi wowote tupingane nao .Kauli ya kibaguzi ya Rais ilikua haina tofauti na mtazamo wa wale wanaoua vikongwe kwa imani za kichawi.Alituma ujumbe hatari sana

Kuna wazee waliolitumikia taifa kwa uadilifu.Unapounga mkono lugha hii chafu kwa wazee kwa sababu ya ujana wako ukumbuke pia utakuja kuzeeka

Uzee si ugonjwa bali ni hatua ambayo ni kielelezo cha neema,Baraka na Utukufu wa Mungu
 
Bora umemuuliza hilo swali. Wazee aliowataja Magu ni kama Lowasa, Chenge, Rugemalila, Reginald Mengi, Ndesamburo na wengineo wa aina hiyo ambao hawafai kabisa kupewa nafasi za kiuongozi kwa vile ni wapigaji
Na yeye mwenyewe Magu mnafiki
 
Bora umemuuliza hilo swali. Wazee aliowataja Magu ni kama Lowasa, Chenge, Rugemalila, Reginald Mengi, Ndesamburo na wengineo wa aina hiyo ambao hawafai kabisa kupewa nafasi za kiuongozi kwa vile ni wapigaji
Hivi ukurupukaji wa mwendokasi ni Juu ya wazee tu!?

Ben ni levo ingine kumwelewa inakupasa ujiongeze. Pole
 
Back
Top Bottom