Mama Dunia

Mama Dunia

God is Dead

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2019
Posts
1,313
Reaction score
1,531
Sasa ni Nini
Mbona Bado tunaamini
Katika Imani ya watakatifu waumini,
Mungu mmoja tangu lini
Pepo nnasikia ina walakini,

Sisi ni watu wa Dunia
Mama yetu aliyetuzaa Pia
Sasa amepoteza asilia
Kipindi anatuzaa alivutia

Leo tumekuwa watu wa mawingu
Kutwa Kücha kushinda na kiwingu
Tunayemkataa duniani ndie Mungu
Tunayemfata mbinguni ni ukungu

Dunia mama yetu,
Okoa vizazi vyetu,
Ili tupate kulinda asili yetu
Daima utabaki kuwa mama yetu

Ulipambana na njama
Kutoka kwenye ulimwengu mpana
Ukatuzaa na mwili wa nyama
Hatimae Leo wanyama tumesimama

Dunia umepoteza uzuri wako
Watu hawawezi kuona kama walitoka Kwako,
Wanaamini una baba Yako,
Eeh Dunia tukomboe sisi wajinga Kwako

Cha kushangaza Bado unazaa mimea
Wanyama bado unawalea
Licha ya kushindwa kukutetea,
Dunia mama tunayekutegemea,

Ndio ninakiri kamili
Tulisimama Kwa miguu mwili
Hatimae pua zikapoteza asili
Tumekuwa watu wa kutumia akili
Sisi wanyama jamii ya tumbili

Itaendelea

Written by Leto, learn engage teach organize
 
Back
Top Bottom