Mama au Mke, "the vice versa of the Facts" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama au Mke, "the vice versa of the Facts"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Chapa Nalo Jr, Feb 12, 2011.

 1. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280
  Kuna thread inaendelea kwenye jukwaa hili yenye heading "Mama au Mke", sasa kutokana na changamoto za ulimwengu wa sasa pamoja na mabadiliko ya kimfumo, sasa naomba tujadili pia kwamba "mwenye mshahara na anaekwenda kusoma nje ya nchi ni mke badala mme"; tupate ushauri kwa upande mwingine.

  Ni vema ukasoma ile thread kwanza ndio uchangie na hii, kama jibu lako ni lilelile la kule, basi naomba msisitizo wako kwa pande hii please!!!
   
 2. LD

  LD JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Daa afu nilishakujibu kule kumbe umekuja huku kabisa bwana, haya lakini ukweli ni ule ule, hakuna siri kwenye ndoa na mshauri wako wa kwanza ni mume wako.Kwa sababu yeye ndo ubavu wako, haiwezekani mume wako akaombe pesa ya matumizi kwa mkwe wake, au asijue miradi ya mke wake. Yani vaisi vesa ni true.
   
 3. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280
  Kama yanatoka moyoni na wake wote ndio msimamo wao basi ni vema sana; nimeuliza hivi kwa sababu kuna malalamiko ya wanaume (hata hapa JF) kuwa wanawake kuiona hela yao au kuchangia hela yao ni mbinde

  Pili nilishakuwa na mjadala na dada mmoja mwanasheria na ameolewa. Hoja ilikuwa sheria ya ndoa TZ inasema ndoa ikivunjika basi mme ataendelea kutoa matunzo kwa mke mpaka atakapoolewa tena au vinginevyo(sic), lakini sheria haisemi chochote kama ndoa husika mwanamke ndio mwenye hela. Sasa huyo dada alipinga kabisa sheria hiyo kurekebishwa ili na mwanaume apewe matunzo na ex-wife, yaani hakutaka hata kutoa sababu. Je Ulimwengu kweli upo tayari kwa usawa unaopigiwa kampeini!!!?
   
 4. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ngoja kwanza nipate glass ya wine il be back
   
 5. LD

  LD JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Binafsi naamini, hakuna usawa utakao tokea duniani kati ya mwanamke na mwanaume. Mwanaume atabaki kama mwanaume na atamtawala mwanamke na tamaa yake itakuwa juu ya mwanamke!! (Biblia kitabu cha mwanzo). Lakini hamtuonea bila sababu kwa sababu tunapakusema na tunaweza kuongea sasa. Kwa hiyo mwanaume inabidi apigane na maisha kweli kweli. Kwa sababu kwa jinsi mlivyoumbwa mwanamke akiwa juu yako kidogo tu, hamwezi kuwa na amani wala uhuru nafsini mwenu.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama kuna USAWA kati ya mwanamke na mwanaume hiyo sheria irekebishwe!Na kama wanaume mtakua na amani kulishwa na mwanamke ambae hata mahusiano hamna!!Nwyz kuhusu mali mkiwa pamoja kuwa na siri sio sahihi!Iwe mwanamke au mwanaume ndo mwenye hela mwenzake ana haki ya kufahamu na hata kusaidia kama kuna miradi!Kuna mahali nilisema..kama MAWAZO YA MIMI..CHANGU VYANGU bado yamekutawala usioe wala kuolewa!Subiri mpaka utakapokua tayari kushea kila kilicho chako na mwenzako!
   
 7. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye redi, mbona wanawake wanalishwa kwa mujibu wa sheria na ma ex-husband wao, je wao wana amani? Kwa sababu katika hati za talaka wanawake huwa hawasahau ilo ombi la matunzo kupitia mahakama. Acha tu sheria irekebishwe ili mwanaume ataeamua kutodai sawa, ataedai sheria imlinde.
   
 8. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280
  Kama maandiko yangefuatwa kwa usahihi mbona mambo yangeenda sawa mno, lakini kuna watu wanachagua vifungu fulani tu vya maandiko na vingine hawataki hata kuvisema. Kuna members humu JF aliwahi puuza hata uwepo wa Mungu na akasema ni Mungu gani huyo eti anayezidiwa hekima ya usawa na binadamu!!. Naamini ndoa zinazofuata maandiko matakatifu kwa usahihi huwa hazikumbwi na dhoruba na kuvunjika.
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli na maisha ni kuchagua, inategemea maisha yako umeyajenga katikati misingi ya nini? Kama umeyajenga katika msingi wa kumwamini Mungu na kuifuata sheria yake na kuikana dunia, mazima yanakwenda kwa amani na furaha kabisa. Utakuwa na Neema ya Mungu maishani mwako ya kukuwezesha ktk mapito mbalimbali.

  Lakini umeichagua dunia, dunia haina jema, na kila lifanywalo duniani bila uwepo Mungu halina matokeo mazuri. Ni bora kuchagua kumheshimu Mungu, na sio lazima kujua na kuiga kila kitu hapa duniani.

  Hapa JF pia kuna watu wa aina tofauti, ni jamii kama jamii nyingine, kwa hiyo ukisoma huku unachanganya na zako kabla hujayafanyia kazi. Barikiwa.
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wanandoa hawana budi kuwekana wazi mambo yote hasa ya pesa. Unaficha ficha ili iweje sasa.
  Mkishaingia ndani ya ndoa ina maana mpo tayari kushare kila kitu. Huwezi ukasema ile nyumba yangu au gari langu, inabidi useme ile nyumba yetu au gari letu hata kama aliyenunua ni mwanamke/mwanaume. Hii inamaanisha ni watu wawili sasa mnaoshare.

  Mimi nafikiri watu wanatafuta pesa kwa ajili ya familia zao na si wao wenyewe. Kwa mtu mwenye mapenzi na familia yake utaona ni jinsi gani anahudumia familia yake na furaha yake ni kuona familia yake ipo salama. Bora yeye asile ila familia yake ile, kuna mambo mengi binafsi yatakayohitaji fedha atajibana ili familia yake isikose mahitaji muhimu.
  Kwahiyo hata kama mwanamke ndio naenda nje nitazingatia kuwa hicho kipato sio changu bali ni chetu (mimi na mume wangu). Kipato changu hakitakuwa na maana kama familia yangu haiishi vizuri. Sitopenda kula good time wakati huko nyumbani mume na watoto wanateseka. Ni aibu kama kipato changu kikubwa halafu nashindwa kumpendezesha mume na watoto wangu.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama tu kuoa mwanamke mwenye pesa zaidi ya mwanaume wengi wenu mnaona tabu kulelewa ndo itakua afadhali!!???:twitch:
   
 12. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,370
  Likes Received: 3,202
  Trophy Points: 280

  Kuna wale wenye "homoni za Kizaire Zaire" za kupenda kulelewa/kuwa na mwanamke mwenye pesa inabidi sheria iwepo na iwalinde.
   
Loading...